Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Rabi' I 1444 Na: HTS 1444 / 10
M.  Jumatano, 19 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Makundi ya Kiislamu Yanawezaje Kuunga Mkono Katiba ya Kisekula?!
(Imetafsiriwa)

Katika taarifa ya pamoja kutoka kwa Chama cha People’s Congress na Ansar al-Sunnah Muhammadiyah – Kituo Makuu, pande hizo mbili ziliunga mkono suluhu ya kisiasa kwa msingi wa kikatiba; iliyoanzishwa na kundi lililoandaliwa katika Baraza la Chama cha Mawakili, na walitoa wito kwa vikosi vyote vya kitaifa kuunga mkono suluhu hii. Katika taarifa yao, pande hizo mbili zilisisitiza kuwa uhuru na mashauriano ni kanuni zinazochochea ukuaji na maendeleo ya kifikra na kisiasa, na kwamba demokrasia ni mtazamo wa wastani wa makabidhiano ya madaraka kwa amani ambayo yanaruhusu uraia kwa watu wote wa nchi bila ya ubaguzi au tofauti.

Je, ndugu hawa waheshimiwa katika chama cha People’s Congress na Ansar al-Sunnah Muhammadiyah - Kituo Kikuu hawajui kwamba msingi wa kikatiba waliouunga mkono, na kuwataka wengine kuzunguka pambizoni mwa suluhu hiyo kwa msingi wake, ni katiba kamili ya kisekula? Msingi wake ni kutenganisha dini na maisha na siasa?!

Ikiwa hawajui, basi sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, na kama jambo la nasaha, tunaeleza mambo yafuatayo kuhusu katiba iliyotajwa hapo juu (Katiba ya Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mawakili):

Kwanza: Katiba hii haikuegemezwa juu ya msingi wa Aqiydah ya Kiislamu, ambayo ndio imani ya watu wa Sudan. Badala yake, ilitokana na msingi wa Kimagharibi katika kuandaa katiba. Ni kutenganisha dini na maisha, na kwa hivyo kuitenga kwake na siasa, na huu ni msingi batili, na kinachojengwa juu ya batili ni batili. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى تَقْوَى مِنَ اللَّهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَىَ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ وَاللَّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

Je! Mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalo burugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” [At-Tawbah 9:109].

Pili: Ibara ya 1 ya rasimu hii ya katiba imeeleza kuwa Sudan ni dola ya kidemokrasia ya kifederali ambayo ndani yake muna tamaduni, makabila, lugha, madhehebu na dini tofauti tofauti. Demokrasia ni nidhamu ya kikafiri, ambayo huufanya ubwana kuwa kwa watu na sio kwa sheria, hivyo ni haramu kuichukua, au kuilingania, na ni nidhamu iliyojengwa juu ya kuchua haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kutunga sheria na kuwapa wanadamu, kwa hiyo wanayatungia sheria yale ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuyaidhinisha! Sisi kama Waislamu tumefungwa na sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu anayesema:

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma’idah 5:50].

Kuhusu fikra ya federali, ni mashine ya kupasua ambayo kwayo Sudan inakusudiwa kuchanwa vipande vipande. Pia ilianza kwa kuitenga Sudan Kusini. Kanuni msingi katika mfumo wa serikali katika Uislamu ni kwamba ni mfumo wa umoja na sio mfumo wa kifederali, ambamo ubwana ni kwa Sharia na mamlaka ndani yake ni kwa Ummah.

Tatu: Pia imeelezwa katika Ibara ya Kwanza... Haki na majukumu zimewasilishwa ndani yake kwa msingi wa uraia. Haki na majukumu katika Uislamu huamuliwa na Sharia. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلالاً مُّبِيناً]

Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab 33:36].

Nne: Suluhu kwa msingi wa katiba hii ya kisekula inayotenganisha dini na maisha, inatumikia mradi wa makafiri wa wakoloni katika nchi yetu, na kutuzuia na Uislamu. Inatosha kwamba Amerika, Uingereza, Ufaransa na nchi nyingine za kikafiri na wafuasi wao ndani na nje ya nchi wanaunga mkono katiba hii na suluhu hiyo kwa msingi wake, ili kupitisha miradi yao; vita dhidi ya hukmu za sheria zilizosalia katika sheria na kanuni, kupitia kutia saini CEDAW, kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, kupora mali ya nchi, na kunyakua ardhi yake.

Kwa kumalizia: Uislamu umebainisha mfumo wa Khilafah na utaregea hivi karibuni, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda, na tunatoa wito kwa ndugu zetu washirikiane nasi ili kuusimamisha; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kukata mizizi ya makafiri, na kurudisha njama zao kwenye nyuso zao. Mtume (saw) alitoa bishara njema kwamba Khilafah itaregea kwenye uongofu baada ya utawala wa kutenza nguvu tunaoishi ndani yake siku za mwisho, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ»

Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo katika muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akanyamaza.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu