Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Rajab 1444 Na: HTS 1444 / 29
M.  Jumatatu, 06 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Umekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Sudan
(Imetafsiriwa)

Ndani ya wigo wa kampeni ya Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ya kupambana na mihadarati, ujumbe kutoka kwa hizb, ukiongozwa na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) - Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akiandamana na Ustadh Abdul Qadir. Abdul Rahman - Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, na Ustadh Abdullah Abdul-Rahman na Ustadh Khalid An-Nur - Wanachama wa hizb, walikutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Sudan, Dkt. Saad Ahmad Saad, katika afisi za Jumuiya hiyo jijini Khartoum leo, Jumatatu asubuhi, 15 Rajab 1444 H, sawia na 6 Februari 2023 M.

Mwanzoni mwa mkutano, Mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Abu Khalil, alizungumzia madhumuni ya mkutano huo na kufafanua kuwa suala la dawa za kulevya sio tu la wauzaji, wapigiaji debe na watumiaji wa dawa hizo pekee, bali suala hilo ni kubwa zaidi kuliko hilo, kuijaza Sudan kwa dawa za kulevya kunachukuliwa kuwa ni vita vya kizazi cha tano vilivyoanzishwa na makafiri wakoloni, kwa lengo la kuharibu akili za vijana na kutia sumu kwenye miili yao. Kwa sababu vijana siku zote ndio chachu ya mabadiliko.

Ustadh Abu Khalil pia alionyesha hali ya serikali kutojali katika kupambana na dawa za kulevya, akitoa mfano wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Jenerali Al-Burhan, ya Waziri wa Mambo ya Nje wa umbile la Kiyahudi; kijidola hiki kidogo kinaunajisi Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, kinaua watoto, wanawake na wazee nchini Palestina. Pia kinaijaza Sudan kwa dawa za kulevya, kwani uhusika wa umbile la Kiyahudi uligunduliwa katika matukio mawili ya mwisho wakati dawa za kulevya zilipokamatwa zilipoingia Sudan. Pia, kwamba vita hivi vichafu vinavyoongozwa na makafiri vinahitaji dola ya kimfumo inayosimama dhidi yake. Dola hii ni dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kisha Dkt. Saad Ahmad Saad - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Sudan, akaukaribisha ujumbe huo, na akathamini juhudi za Hizb ut Tahrir, na akasema: "Tumefurahishwa sana na mkutano huu, na Hizb ut Tahrir ni mfano unaopaswa kuigwa katika ulinganizi." Kisha akataja kuwa Jumuiya hiyo inaandaa nyaraka za namna ya kutokomeza dawa za kulevya. Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kwamba ni lazima kuwasiliana katika kila jambo linalohusu nchi na wananchi.

Ustadh Abdul-Qadir Abdul-Rahman - Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan alimkabidhi Ndugu Dkt. Saad baadhi ya machapisho ya chama yayohusiana na mada hiyo, pamoja na matoleo ya Jarida la Ar-Raya linalotolewa na Hizb ut Tahrir.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu