Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  15 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: HTS 1445 / 46
M.  Alhamisi, 23 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala Anataka Kuipeleka wapi Sudan?!
(Imetafsiriwa)

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, alisema kuwa vita vya Sudan bado viko katika hatua za awali. Al-Burhan, wakati akitoa salamu za rambirambi kwa mauaji ya afisa mmoja wa jeshi la Sudan, aliapa kuviandama Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na kuregesha haki za watu wa Sudan. Aliongeza, "Vita ndiyo kwanza vinaanza, na hatutampa adui nafasi ya kupumzika hadi ushindi upatikane na yote ambayo wananchi wamepoteza yaregeshwe." (Al Jazeera; Sudanese Press, 22/05/2024)

Je, watu wa Sudan hawajateseka vya kutosha kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi miwili, muda wa vita hivi vilivyolaaniwa na visivyo na maana, kwa mauaji, ubakaji, uporaji wa pesa na mali, kuwahangaisha watu wenye amani, na kuwahamisha kutoka kwenye makaazi yao? Nusu ya wakaazi wa Sudan wamekuwa ima ni wakimbizi wa ndani, wengi wao wakilala ardhini chini ya anga bila maji, chakula, au dawa, au wakimbizi katika nchi jirani, wanaoishi kwa udhalilifu na fedheha. Baada ya miezi yote hiyo mirefu, huku watu wakiwa na matumaini ya kukomesha vita hivyo na kukomesha mateso yao pamoja navyo, kamanda wa jeshi na mwenyekiti wa Baraza Kuu la Utawala anawavunja moyo na kupanda ukataji tamaa na hofu nyoyoni mwao kwa kuonya kwamba vita hivyo ndio kwanza vinaanza?!

Kwa hiyo furahini, enyi watu wa Sudan, katika mauaji zaidi, ukiukaji, uhamisho, uharibifu, na maangamivu kwa miaka ijayo!

Mtume wetu (saw) amesema: «بَشِّرُوا وَلَا تُنَفِّرُوا وَيَسِّرُوا وَلَا تُعَسِّرُوا» “Toeni bashara njema wala musiwafukuze watu; na fanya wepesi na wala musiyafanye mambo kuwa magumu.” Hata hivyo, viongozi wa nchi yetu hawajali yale aliyosema Mtume (saw) kipenzi, wala hawajali maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Lau wangeshikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw), vita hivi havingeanza, na kusingekuwa na nafasi ya uingiliaji kati wa kafiri mkoloni Magharibi, pamoja na Marekani na wengineo.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, katika kukabiliana na tishio hili, tunawaambia: Mcheni Mwenyezi Mungu kuhusu familia zenu na watu wenu, regeeni katika fahamu zenu, acheni umwagaji damu huu, na muinusuru Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyedanganya watu wake, ili kutimiza bishara njema ya Mtume (saw) kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu akukubali toba yenu; Hakika Yeye ni At-Tawwab Ar-Rahim (Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu).

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu