Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 6 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: HTS 1446 / 66 |
M. Jumatatu, 02 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yahuisha Ibada ya Takbira Katika Mwezi wa Dhul-Hijjah kwa Matembezi ya Kishindo katika Soko Kuu la Port Sudan
(Imetafsiriwa)
Baada ya swala ya Alasiri mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 6 Dhul-Hijjah 1446 H, sawia na tarehe 2 Juni 2025 M, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walihuisha ibada ya takbira katika mwezi wa Dhul-Hijjah. Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alihutubia waumini katika Msikiti wa Ibn Mas’ud katika soko kuu la Port Sudan baada ya Swalah ya Alasiri, akiwakumbusha juu ya ubora wa siku hizi zilizobarikiwa za Dhul-Hijjah, na jinsi Maswahaba – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – walivyozitukuza siku hizi kwa takbira na tahleel. Kisha akaanza kupiga takbira, ikifuatiwa na dua. Baadaye wote wakatoka kwa matembezi ya kishindo wakiwa wamebeba Rayah (bendera) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na alama kubwa isemayo: "Kuhuisha Ibada ya Takbira katika Mwezi wa Dhul-Hijjah."
Matembezi hayo yalitembea sehemu za soko hilo huku sauti zikivuma kwa takbira na tahleel. Kisha wakarudi kwenye eneo lililo karibu na msikiti, ambapo Ustadh Abu Ayman aliwaombea waliokuwepo na Waislamu wote – kwamba haja zao yatimizwe, kwamba Mwenyezi Mungu atuondolee dhiki za dhahiri na zilizofichika, na aipe ushindi Dini hii kupitia utekelezaji wa Shariah yake duniani chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, huku waliokuwawepo wakiitikia Amin.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah of Sudan
https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/4700.html#sigProIdf36c8183a5
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |