Jumanne, 01 Rabi' al-thani 1447 | 2025/09/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 36
M.  Jumamosi, 20 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari yenye kichwa:
“Taarifa ya Quad na Ubwana Uliopotea”
(Imetafsiriwa)

Mnamo Ijumaa, 20 Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 12 Septemba 2025 M, mawaziri wa mambo ya nje wa kile kinachoitwa Quad, yaani Amerika, Saudi Arabia, Imarati, na Misri, zilitoa taarifa kuhusu Sudan. Vipengee vikuu zaidi ndani yake vilikuwa:

1. Mkataba wa miezi mitatu wa kibinadamu wa kuwezesha kuingia kwa misaada ya kibinadamu, ambayo itasababisha mara moja usitishaji wa kudumu wa mapigano.

2. Kuzinduliwa kwa mchakato wa kina na wa uwazi wa mpito, unaohitimishwa ndani ya miezi tisa, kuelekea kuanzishwa kwa serikali ya kiraia inayofurahia uhalali.

3. Utawala wa mustakabali wa Sudan utaamuliwa na watu wa Sudan kupitia mchakato mpana wa mpito wenye sifa ya uwazi na sio chini ya udhibiti wa upande wowote kwenye mzozo.

Ikizungumzia taarifa ya Quad, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan mnamo Jumamosi tarehe 21 Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na 13/09/2025 M, ilitoa taarifa ikisema: “Serikali ya Sudan inakaribisha juhudi zozote za kikanda au kimataifa zinazosaidia kumaliza vita... Serikali ya Sudan haitakubali uingiliaji wowote wa kieneo au kimataifa utakaokosa kuheshimu ubwana wa serikali ya Sudan na taasisi zake halali, ambazo zinaungwa mkono na watu wa Sudan, au haki yake ya kulinda raia na eneo lake. Pia inakataa jaribio lolote la kuiweka kwenye usawa na wanamgambo wa kigaidi.”

Wanaofuatilia suala la Sudan na mapambano makali ya kimataifa juu ya ardhi yake wanajua vyema kwamba vita hivi vinaendeshwa na Marekani ili kung'oa ushawishi wa Kiingereza na kuichana Sudan kwa kutenganisha Darfur, na kwamba hatua zote za kisiasa zinazofanywa na Amerika au vyombo vyake nchini Sudan zinalenga kuondoa juhudi zozote ambazo zingewarudisha watu wa Uingereza kwenye mandhari. Kwa hivyo hatua ya Quad wakati huu ilikuja dhidi ya historia ya watu wa Uingereza kuhamia Tume ya Muungano wa Afrika ili kuanzisha tena “Somoud” kwenye mandhari; Vyanzo vya habari vilifichua kuwa Muungano wa Afrika (AU) ulialika vikosi vya kitaifa vinavyounga mkono jeshi la Sudan na muungano wa “Somoud” kuhudhuria mikutano ya mazungumzo ya Wasudan kwa Wasudan mnamo tarehe 6 Oktoba jijini Addis Ababa, ambako watu wa Uingereza wanafanya kazi, hasa katika Tume ya AU, kurekebisha Somoud. Vile vile, Kamishna wa AU Mahmoud Ali Yusuf alikutana mnamo Ijumaa, 12/09/2025, jijini Abu Dhabi na Abdullah Hamdok, mkuu wa Somoud, na kiongozi mkuu katika muungano wa Somoud aliiambia ‘Sudan Tribune’ kwamba mkutano huo ulijadili dori ya Muungano wa Afrika katika kutatua mzozo huo na kukubaliana juu ya mchakato wa kuaminika wa kisiasa unaoongozwa na Wasudani chini ya mwavuli wa Muungano wa Afrika. Kwa hivyo, Amerika ilihamia kupitia Quad iliyo tabanni ramani ya utendakazi ya tarehe 10/03/2025 iliyowasilishwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa, Al-Harith Idriss, kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na Amerika inataka kuifanya taarifa ya Quad ambayo ni ramani ya utendakazi iliyowasilishwa na serikali ya Sudan yenyewe, kuwa ndio msingi wa suluhisho kati ya serikali ya Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka pindi mapishi yake yatakapoiva.

Huu ndio uhalisia wa kisiasa nchini Sudan – kwa hivyo iko wapi dhana ya ubwana katika ukumbi huu wa kipuuzi?

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunafafanua ukweli ufuatao:

Kwanza: Vijidola vidogo vya Sykes-Picot ambavyo Magharibi mkoloni kafiri iliviunda juu ya magofu ya Khilafah Uthmani, ikiwemo Sudan, ni dola za kiutendaji zilizokoloniwa na kupiganiwa na wakoloni; vyombo vyao katika hilo ni viongozi wa majeshi, mavuguvugu ya waasi, na mazingira ya kisiasa ya kisekula ya dhahiri au ya siri. Vyombo hivi vya kikoloni havina ubwana juu yao vyenyewe iweje basi nchi zao zimiliki ubwana?!

Pili: Udanganyifu ni silaha hatari zaidi ya mkoloni na washirika wake; wanamfanya adui aonekane rafiki anayeingilia kila undani wa serikali na maisha ya watu, na kumfanya ndugu kuwa adui anayelengwa na mashini ya kuua. Hivyo basi wajumbe na mabalozi wa maadui wanakanyaga uwanja wa nchi kwa kisingizio kwamba wao ni marafiki wanaojali maslahi ya nchi na watu!

Tatu: Je, mtu mwenye akili timamu anawezaje kuzungumzia ubwana wa nchi hii huku matatizo yake yakijadiliwa katika vyombo vyote vya Umoja wa Mataifa, hususan Baraza la Usalama, Muungano wa Afrika, Ligi ya Waarabu, IGAD, Quad, dola jirani, na muungano unaoongozwa na Kundi la ALPS; kila marais wawili au mawaziri wawili wa mambo ya nje wakikutana wanazungumza kuhusu Sudan na matatizo yake, kisha tunazungumza ubwana? Je, hakuna mtu mwenye busara miongoni mwenu?

Nne: Kwa kukosekana kwa dola ya Waislamu Khilafah dhana ya ubwana ilitoweka katika ardhi zetu na ikawa inatumiwa tu na vyombo vya wakoloni (watawala na wanasiasa) kuzuia miradi ilio kinyume na maslahi ya mabwana zao; hivi wanaita “ubwana” ili kuzuia baadhi ya miradi, na pindi mradi wa kihalifu ukitoka kwa bwana wao wanaupitisha wakidai ni marafiki wanaolinda nchi na maslahi ya watu!

Tano: Makafiri wakoloni, hasa Marekani dola kuu katika ulimwengu huu wa kibepari huchochea vita katika nchi dhaifu na kisha kutumia usimamizi wa vita hivyo kama chombo cha kutambua maslahi yao wenyewe, na si yale ya watu wanaokandamizwa. Hivyo ukoloni unazingatia na kuzigawanya dola. Kwa hiyo, yeyote anayetoa wito wa kutaka kumruhusu kafiri mkoloni au vyombo vyake kutoka dola za eneo kuingilia kati ni msaliti kwa watu wake, kumtegemea mgeni ni kujiua kisiasa.

Sita: Je, mahusiano ya kimataifa hayakujengwa juu ya usawa na maelewano? Iko wapi hiyo katika miamala ya serikali zetu nchini Sudan na dola ambazo zina wajumbe wanaokuja kujadili mambo yetu ya ndani zaidi chakula, dawa, elimu, kuzingirwa kwa El-Fasher na kila kitu? Kwa mfano, Sudafax mnamo tarehe 10/09/2025 ilinukuu mkutano mmoja kati ya Kamel Idris na mjumbe wa Uingereza Richard Crowder: “Crowder alisisitiza kwamba vipaumbele vya nchi yake kwa sasa vinalenga katika kufikia usitishaji vita huko Al-Fasher na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia raia bila vikwazo, na kuthibitisha uungaji mkono kamili wa amani wa London nchini Sudan.” Tumezoea kusikia habari kama hizi na hazipingwi katika mazingira ya kisiasa; wengine huona kama kupenya na mafanikio. Lakini je, Al-Burhan anaweza kutuma mjumbe kujadili matatizo ya ndani ya Uingereza na Waziri Mkuu wa Uingereza?! Hili linaonyesha hitaji letu la dola iliyo huru kweli kweli, si unafiki.

Saba: Amerika inahama wakati wowote inapohisi upande fulani unaipinga katika faili la Sudan; hivyo ikatoa taarifa ya Quad na kutuma mjumbe wake kwa Muungano wa Afrika. Al Jazeera Net mnamo tarehe 18/09/2025 iliripoti Masud Pauls, mshauri mkuu wa Rais wa Marekani kuhusu Afrika, akisema Quad ni “jukwaa linalounga mkono mipango mingine, si badali,” akisisitiza AU inasalia kuwa upande mkuu katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan. Alisema Quad inafanya kazi pamoja na majukwaa mengine na imepata matokeo chanya, hasa baada ya kutangaza ramani ya mageuzi yenye ratiba zilizo wazi. Inawezekana Amerika itazuia mazungumzo baina ya Wasudan na Wasudan ambayo Waingereza wanataka kutumia kama farasi wa Trojan kuwatambulisha watu wao katika Somoud kwenye uwanja wa kisiasa wa Sudan. Tovuti ya al-Muhaqqiq iliripoti Dkt. Tijani Sisi, mkuu wa Viguvugu la Majeshi ya Kitaifa, akisema ni vigumu kwa vikosi vya kitaifa kushiriki katika mikutano ya maandalizi ya mazungumzo ya Wasudan kwa Wasudan yatakayofanyika Addis Ababa mnamo tarehe 6 Oktoba chini ya mwavuli wa AU; Sisi alisema vikosi vya kitaifa vina dukuduku na mwaliko huo na jinsi ulivyowasilishwa na AU. Hii ni nchi yetu uwanja wa mapambano ya kimataifa!

Enyi waheshimiwa katika duara za kisiasa na vyombo vya habari:

Ni lazima turudishe upya mfumo wetu kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida, ambayo itasafisha mandhari ya kisiasa ya wanafiki na vibaraka na kung'oa ushawishi wa makafiri wakoloni wa Magharibi kutoka katika nchi yetu, kanuni zake za kibepari na fikra za kimatumizi, ili tuweze kupumua harufu ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu pekee na kuishi chini ya ubwana wa kweli wa Shariah inayoongozwa na watu wenye kurudisha heshima na hadhi yetu, ili turudi kuwa umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu. Basi kuweni, enyi ndugu, miongoni mwa wafanyao kazi, linganieni na mtoe bishara njema, kuna kheri katika dunia hii na akhera.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfāl: 24].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu