Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 7 Jumada I 1447 | Na: HTS 1447 / 47 |
| M. Jumatano, 29 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mtu Anayehusika na Usalama wa Watu Anawezaje Kukimbia Akitafuta Usalama?!
(Imetafsiriwa)
Sudan News ilinukuu Darfur 24 katika ripoti moja yenye kichwa: “Kujiondoa kwa Uratibu au Kuanguka?! Makamanda na Maafisa wa Jeshi na Vikosi vya Pamoja Waondoka Al Fasher Siku Mbili Kabla ya Kuanguka Kwake,” ikisema: “Vyanzo viwili kutoka Darfur Kaskazini viliifichulia Darfur 24 kwamba makamanda wa jeshi, pamoja na wanachama wa vikosi vya pamoja, gavana wa Darfur Kaskazini, Al-Hafiz Bakhit, na wanachama kadhaa wa serikali yake, waliondoka Al Fasher siku mbili kabla ya Vikosi vya Msaada wa Haraka kutangaza udhibiti wao kamili wa makao makuu ya Kikosi cha 6 cha Wanajeshi Wapiganaji.” Ripoti hii inathibitishwa na kile kilichosemwa katika hotuba ya Burhan: “Kila mtu anafuatilia kilichotokea Al Fasher. Uongozi huko, ikiwemo kamati ya usalama, ulitathmini kwamba walilazimika kuondoka mji huo kutokana na uharibifu wa kimpangilio na mauaji ya kimpangilio ya raia. Waliamua kuondoka jijini na kwenda mahali salama ili kuwaokoa raia waliobaki na wengine mjini humo kutokana na uharibifu”!!
Kwa hivyo nini kilitokea?! Je, waliwaokoa watu kutokana na mauaji ya kimpangilio baada ya kujiondoa huku?! Jibu, ambalo ulimwengu mzima ulishuhudia kupitia video zilizorekodiwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) wenyewe, ni kwamba mauaji halisi ya kimpangilio yalianza baada ya makamanda wa jeshi, vikosi vya pamoja, na maafisa kujiondoa. Habari kutoka Al Fasher ziliripoti kwamba RSF ilifanya mauaji mengi ya uwanjani katika moja ya vitendo vikubwa zaidi vya kulipiza kisasi ambavyo Sudan imeshuhudia wakati wa vita hivi vilivyolaaniwa. Hata wanawake na wazee hawakusazwa. Ripoti za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa zilisema kwamba takriban raia 1850 waliuawa Kaskazini mwa Darfur, wakiwemo angalau 1350 huko Al Fasher pekee. Inapaswa kukumbukwa kwamba idadi hii haionyeshi idadi halisi ya waathiriwa kutokana na mawasiliano duni.
Ripoti pia zinaonyesha kuuawa kwa raia waliojaribu kukimbia, pamoja na ushahidi wa nia za kikabila za mauaji hayo, pamoja na kulengwa kwa watu ambao hawashiriki tena katika uhasama. Video nyingi zilizopokelewa na Umoja wa Mataifa zilionyesha wanaume kadhaa wasio na silaha wakipigwa risasi, au wamelala wamekufa, wakizungukwa na wanachama wa RSF.
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunawawajibisha viongozi wa Vikosi vya Msaada wa Haraka na askari wao waliotekeleza ukatili huu kwa kitendo hiki kiovu, na tunawakumbusha maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):
[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]
“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisa: 93].
Pia tunaiwajibisha serikali kwa kuchelewa kuwasaidia watu wa El-Fasher na kuondoa mzingiro dhidi yao, na wanao uwezo wa kufanya hivyo, lakini kuna wale wanaofunga mikono yao na kuwazuia kufanya hivyo, hadi El-Fasher ikanguka!!
Amerika ilikuwa ikisubiri El-Fasher ianguke. Ilitoa ruhusa kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuzingira mji na kuushambulia kwa zaidi ya majaribio 268 hadi hatimaye ulipoanguka. Mshauri wa Trump wa Mashariki ya Kati na Afrika, Massad Boulos, alitoa maoni kuhusu kilichotokea El-Fasher, akisema, “Kilichotokea hakishangazi!” Tunawaambia kwamba kiongozi hatoroki kwa ajili ya usalama, akiwaacha nyuma watu wasio na ulinzi wale ambao usalama wao ni jukumu lake. Viongozi na maafisa wanawezaje kujiondoa, wakiwatelekeza wapiganaji na raia kwenye mishini ya mateso na mauaji wanayoijua vizuri? Historia ya RSF imefunganishwa na mauaji, uunguzaji moto, ubakaji, na kila aina ya ukatili popote wanapoenda. Wanawezaje kuwatelekeza watu huku wakijua hatima yao?
Kiongozi katika Uislamu hatoroki kamwe; hivi ndivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyotufundisha, naye ndiye mfano bora zaidi:
[لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّهَ كَثِيراً]
“Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.” [Al-Ahzab: 21].
Siku ya Hunayn, Mtume (saw) alisimama imara, akisonga mbele na kukabiliana na hatari kwa ujasiri mkubwa, wakati ambapo vita vilizidi na Waislamu wakaanza kukimbia vita. Yeye (saw) alisimama wima, akiwaita hadi waliporudi na wakawa washindi.
Enyi watu wa El-Fasher, na watu wote wa Sudan, hakika, enyi Waislamu kila mahali:
Tunahitaji kiongozi anayefuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kutuongoza kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw) ili kuhifadhi maisha yetu na kulinda heshima yetu. Hili litatokea tu ikiwa tutafanya kazi kumpata, kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



