Jumamosi, 09 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Sweden

H.  29 Rabi' II 1443 Na: 1443/02
M.  Ijumaa, 05 Novemba 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kufukuzwa kwa Odiljon Jalilov Kunahatarisha Maisha Yake

(Imetafsiriwa)

Jioni ya mnamo Oktoba 29, Odiljon Jalilov, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Sweden, alipatikana na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi akisubiri maandalizi ya kuhamishwa hadi Uzbekistan.

Uzbekistan ina historia ndefu na inayojulikana ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa kisiasa, hata mbaya zaidi dhidi ya wapinzani wa Kiislamu, wanachama wa Hizb ut Tahrir. Wanachama wetu wameteseka kwa miongo mingi kutokana na vifungo virefu vya jela, mateso na hata mauaji nchini Uzbekistan. Vyanzo kutoka kwa familia ya Odiljon Jalilov nchini Uzbekistan vinasema polisi wamekuwa wakiwasiliana na familia yake na wamewafahamisha kuwa Odiljon Jalilov ataregea hivi karibuni. Kufukuzwa na kukabidhiwa kwa mwanachama wetu, Odiljon Jalilov, kwa serikali dhalimu ya Uzbekistan kunawakilisha tishio la kihakika kwa maisha yake ambayo mamlaka za Uswidi zitawajibika kwayo endapo uhamishaji huo utafanywa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uswidi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Sweden
Address & Website
Tel: 
https://hizb-ut-tahrir.se/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu