Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  24 Rabi' II 1443 Na: 1443 / 01
M.  Jumatatu, 29 Novemba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

MIAKA 60 YA UHURU BADO UMEME NA MAJI YA MGAO

Tarehe 9 Disemba, Tanganyika / Tanzania itaadhimisha miaka 60 ya uhuru iliyoupata kutoka kwa Uingereza 1961, baada ya awali kuwa chini ya ukoloni wa Ujerumani kabla ya nchi hiyo kushindwa katika Vita vya Kwanza.

Pamoja na kupata kinachoitwa uhuru, bado Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo inayoendelea sasa ya uwepo mgao wa umeme na maji, vyote viwili vimejiri kwa sababu kadhaa ikiwemo athari ya ukame kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ni jambo lisiloingia akilini mpaka leo hii, tatizo la umeme ni kubwa baada ya viwango vya maji katika mabwawa mengi ya mitambo ya umeme kupungua. Hali hiyo imeathiri uzalishaji umeme katika baadhi ya vituo kama Kihansi, Kidatu na Pangani. Hali iliyopelekea nakisi / upungufu katika gridi ya taifa kwa karibu megawatts 345, sawa na asilimia 2.  Zaidi ya yote hayo ni asilimia 15 tu ya raia ndani ya Tanzania ndio wanaotumia huduma ya umeme.

https://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/kenyaa/428.html

Kuhusiana na upungufu mkubwa wa maji hususan katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam ambalo zaidi hutegemea Mto Ruvu, mto huo umekuwa chini ya uzalishaji wa viwango vya kawaida vya lita 270 milioni kwa siku, kukiwa na upungufu wa lita milioni 70.

Suala la mabadiliko ya tabia nchi kweli halikwepeki. Lakini kuna sababu nyengine nyingi zinazosababisha kadhia hii, ikiwemo usimamizi mbovu, kukosekana uoni mpana hususan katika suala la umeme, kwa kutowekeza  zaidi  katika  vyanzo anuwai vya uzalishaji nishati ya umeme, na badala yake kuwekeza nguvu zaidi katika miradi inayozalisha umeme  usiotosheleza.

Ni zaidi ya aibu kwamba Tanzania inakabiliwa na tatizo la maji na umeme na mengine mengi kwa zaidi ya nusu karne tangu kupata uhuru wa bendera, ukijumlisha pamoja na uwepo kiwango kikubwa mno cha rasilmali mbalimbali ikiwemo kiwango kikubwa cha gesi asilia inayokadiriwa kuwa trilioni 57 cubic feet. Jumla ya uzalishaji wa bilioni 110 cubic feet kwa mwaka kutoka katika visima vitatu vilivyopo kusini ya Tanzania. https://www.tanzaniainvest.com/gas

Pia Tanzania ina madini mbali mbali ikiwemo kiwango kikubwa cha dhahabu, kiasi cha kuwa nchi ya tatu katika uzalishaji dhahabu katika Afrika, nyuma ya Ghana na Afrika ya Kusini. Bila ya kusahau uwepo wa kiwango kikubwa cha madini ya urani (uranium). Kwa mujibu wa kampuni ya Uchimbaji Madini ya Australia, Tanzania ina kiwango kikubwa cha madini ya urani kuweza kuwa miongoni mwa nchi tano bora barani Afrika.

Na kwa upande wa rasilmali ya maji, Tanzania ina vyanzo vikubwa vya maji kama Bahari ya Hindi upande wa mashariki, Ziwa Victoria ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa ulimwenguni likiwa limetanda katika mita za mraba wa 65,583 (sq mi) ambapo Tanzania pekee ina sehemu ya 49% ya 33,700 ya kilomita mraba. Sehemu kubwa zaidi ukilinganisha na majirani zake (Uganda na Kenya).

Bila ya kutaja uwepo wa Ziwa Tanganyika, ziwa la pili kuchukuwa ujazo mkubwa duniani, na kuwa na kina kikubwa katika Afrika, likiwa na ujazo mkubwa zaidi wa maji mwanana na baridi.

Chanzo cha madhila, umasikini na kukosa maendeleo ndani ya Tanzania, Afrika na nchi zote changa ni kutokana na unyonyaji na uroho wa mfumo wa kimagharibi wa ubepari, nchi hizo kukosa uhuru wa kweli wa kujiamulia mambo yao pia nchi changa zinakosa uoni mpana kwa kule kukosa nguzo thabiti ya kimfumo kuwaongoza katika mambo yao.

Muda umeshawadia kwa watu wa nchi changa ikiwemo Tanzania kuamka kwamba Ubepari kamwe hautosita ajenda yake ya kinyonyaji kwa nchi changa.  Njia pekee ya kujivua na hali hiyo ni kung’oa mfumo muovu wa kibepari, na kuweka mfumo mbadala wa Uislamu unaotokamana na wahyi. Chini ya dola yake ya Khilafah itaukomboa ulimwengu na ubinadamu jumla kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo na kuondoa moja kwa moja minyororo yote ya unyonyaji.

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu