Afisi ya Habari
Tanzania
H. 17 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: 1446 / 09 |
M. Alhamisi, 15 Mei 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bunge la Ulaya na Maazimio ya Ukoloni Mambo Leo
(Imetafsiriwa)
Wiki iliyopita Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) lilitoa mwito kwa Tanzania kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kutatua kesi waliyosema ina msukumo wa kisiasa ya kiongozi wa chama cha upinzani, kutoa uhuru zaidi wa kisiasa kupitia majadiliano, kufanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi,kuheshimu haki ya vyama kushiriki katika uchaguzi huru nk.
Aidha, Jumuiya hiyo kupitia Bunge lake hilo ikaitaka Tanzania kuacha kunyanyasa wanasiasa wa upinzani, watetezi wa haki za binadamu, watetezi wa mapenzi ya jinsia moja/ LGBTQ (ushoga na usagaji) , waandishi wa habari, jumuiya za kiraia nk.
Kufuatia maazimio hayo ya Jumuiya ya Ulaya, sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunasema haya:
Maazimio ya Jumuiya ya Ulaya yanaonesha ni kwa kiasi gani bado nchi za Ulaya zinavyoendelea na ‘ukoloni mambo leo’ kwa nchi changa ikiwemo Tanzania. Baadhi ya mataifa hayo pamoja na historia yao chafu ya kushiriki kwao katika ukoloni mkongwe ulioacha madhara makubwa, bado wanaendelea na uchu wao wa kuingilia kati mambo ya nchi changa, kiasi cha kuzifanyia kadhia za nchi nyengine changa kuwa ni ajenda katika vikao vyao na kutoa maagizo kwa nchi hizo. Ni lini mabunge ya nchi changa yamewahi kuketi na kutoa maazimio na kuagiza nchi zao?
Amma mwito wa Jumuiya ya Ulaya juu ya ‘uhuru wa kisiasa, chaguzi huru, mabadiliko ya sheria za uchaguzi na kuachwa manyanyaso kwa upinzani, sisi Hizb ut Tahrir Tanzania pamoja na kuwa hatukubaliani na mfumo batili wa siasa za kidemokrasia, bali pia kwa misingi ya kibinadamu hatukubaliani na manyanyaso dhidi ya raia wengine, wawe wanasiasa au raia wa kawaida. Hata hivyo, iwe bayana kwa Jumuiya ya Ulaya kuwa manyanyaso ya wapinzani, hadaa, udanganyifu, dhulma nk. hayo ni tabia ya kimaumbile ya mfumo wao wa kidemokrasia ambao wa EU ndio wadau, vinara washika bendera wanaoulazimisha kwa nchi changa. Vipi mfumo uliojengwa juu ya msingi wa ‘maslahi’ utakuwa na uadilifu, usawa na haki ilhali unazingatia kitu kimoja tu, nacho ni uwepo wa maslahi tu?
Kuhusiana na mwito wao wa kuunga mkono utetezi wa mapenzi ya jinsia moja (ushoga na usagaji) hiyo ni dalili ya kufilisika kwa mfumo wao wa kidemokrasia kwa namna mbili: Kwanza, mfumo wao huo unapingana na maumbile ya mwanadamu. Pili, unamfanya mwanadamu kuwa uwanja wa majaribio ya kimaadili, kwa kuwa awali walikuwa wakipinga vitendo hivyo vya ushoga na usagaji, lakini sasa wanaunga mkono na kuvipigia debe. Aidha, suala lao chafu la mapenzi ya jinsia moja kupata upinzani ndani ya Afrika na sehemu nyengine ni dalili ya kutokubalika mfumo wao wa kidemokrasia, kwa kuwa miongoni mwa nguzo za mfumo huo ni ‘uhuru wa kibinifasi’ ambao ndio unaohamasisha matendo hayo.
Tunaiuliza Jumuiya ya Ulaya, kiwango cha utu kinawashughulisha zaidi na kadhia ya Tanzania kuliko mauaji ya halaiki ndani ya Gaza? Nani asiyejua kuwa nchi zao wanatoa kila aina ya msaada wa kimada, kisiasa, kidiplomasia nk. kwa kijidola bandia cha Israel ili kufanikisha mauaji ya halaiki. Ni aina gani ya utu huo wa Jumuiya ya Ulaya kama sio unafiki na kuwa na sura mbili?
Mwisho, lazima ieleweke kuwa mfumo wa Jumuiya ya Ulaya ni ubepari, mfumo wa ukoloni na unyonyaji, na dhana yao ya kisiasa ya demokrasia ni udanganyifu na khiyana tu. Kupitia uwongo wao huo (demokrasia) wako tayari kumuunga mkono yeyote atakayedhamini maslahi yao bila ya kujali utu, uadilifu wala wanachokiita haki za binadamu.
Kwa hakika imetosha kwa kila mtu makini kujitenga mbali na mfumo huo wa uwongo wa demokrasia na kuchukua mfumo mbadala wa Kiislamu unaosimamia haki na uadilifu kwa wote, bila ya kuzingatia dini, rangi au mahala.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |