Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  22 Safar 1440 Na: 1440/02
M.  Jumatano, 31 Oktoba 2018

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waacheni Huru, Wao si Magaidi!

Ni mwaka mmoja sasa tangu wanachama wetu watatu wa Hizb ut Tahrir / Tanzania: Ustadh Ramadhan Moshi (39), Waziri Suleiman (31) na Omar Salim Bumbo (49) kutekwa nyara na kutuhumia kirongo kwa madai ya 'njama za kutekeleza ugaidi' na 'kufanya vitendo vya kigaidi'.

Kwa mwaka mzima huu wakiwa kizuizini, mbali na kuwa mbali na familia, jamaa, marafiki zao na kusimamisha shughuli zao za kiuchumi, pia wanapitia kifungo cha kinyama katika mazingira machafu yaliyo kosa huduma za kijamii kwa jumla. Fauka ya hayo, inaumiza moyo kuwa kesi yao inaendelea kutajwa kila baada ya wiki mbili, bila ya kuanza kwa kisingizio cha kutokamilika kwa ukusanyaji wa ushahidi kwa mwaka mzima!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania tunasisitiza kwa nguvu kuwa wanachama hawa hawana hatia pasi na shaka yoyote, na hii ndio sababu mpaka sasa hakuna imani wala hamu ya kuanzisha usikizaji wa mashtaka yao. Pia tunasisitiza kuwa tangu Hizb ut Tahrir iasisiwe mnamo 1953 ulinganizi wa Uislamu umeshikamana kisawa sawa na njia ya Mtume Muhammad (saw) ambayo inahitaji mtu kujifunga katika njia ya kifikra na kisiasa pasi na kutumia nguvu au ghasia. 

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania kwa mara nyengine tena tuzitaka taasisi za utekelezaji sheria nchini Tanzania kuwaachilia huru wanachama wetu hawa. Vilevile tunayaomba mashirika ya haki za kibinadamu, viongozi wa jamii, wasomi, wanahabari na ummah kwa jumla wakiwemo wanachama wa jamii ya Waislamu kunyanyua sauti zao katika kutafuta kuachiliwa huru kwa ndugu zetu hawa, na kupinga kwa nguvu Sheria ya kimapendeleo ya Kupambana na Ugaidi ambayo ililazimishwa na dola zenye nguvu na inatumika kugandamiza, kutesa na kuteka nyara watu kote nchini nk.

Tunazikumbusha taasisi za Tanzania za utekelezaji sheria, kuwa huku Tanzania ikiendelea kuwakamata kwa dhulma mamia ya Waislamu katika kuitimiza Sheria ya Kupambana na Ugaidi, nchi jirani kama Kenya, Uganda na Ethiopia zinaendelea kuwaachilia huru washukiwa kama hawa. Sasa ni wakati wa Tanzania wa kupata funzo kutoka kwa majirani zake.

Masoud Msellem
Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu