Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ukraine

H.  2 Safar 1442 Na: 1442/01
M.  Jumapili, 20 Septemba 2020

Katika Mapambano Yake Dhidi ya Uislamu, Urusi kwa Mara Nyengine Tena Imeonyesha Udhaifu Wake wa Kifikra

(Imetafsiriwa)

Mnamo Septemba 16, 2020, Mahakama ya Kijeshi ya Wilaya ya Kusini ya Shirikisho la Urusi huko Rostov-on-Don ilitangaza uamuzi dhidi ya Waislamu 8 kutoka Crimea katika kile kinachoitwa "kesi ya pili ya Bakhchisaray ya Hizb ut Tahrir". Watu 7 walihukumiwa vifungo kuanzia miaka 13 hadi 19. Kesi na mashtaka ya korti hudumu kwa miaka mitatu.

Marlen Asanov, Memet Belyalov, Timur Ibragimov, Server Zekiryaev, Server Mustafayev, Seyran Saliev na Edem Smailov walipatikana na hatia katika kuandaa na kushiriki katika shughuli za kigaidi. Ernes Ametov hakupatikana hatia na aliachiliwa huru katika chumba hicho cha mahakama.

Kwa mara nyingine tena tulishuhudia kesi nyingine ya uongo na hukumu iliyotarajiwa, wakati wabebaji safi wa dawah, ambao wanaishi kulingana na Uislamu walituhumiwa vitendo vya kigaidi.

Kama ilivyokuwa zamani, katika nyakati za Tsar na Ukomunisti, mamlaka za Urusi zilifanya shambulio jingine kali hadharani kwa Waislamu wa Crimea, wakitaka kuwakandamiza na kuvunja matakwa yao. Kwa mfano Urusi inateua sehemu changamfu zaidi ya Waislamu wa Crimea kama wahalifu, na kuwafanya wengine kuwa vibaraka wake, wakijaribu kupata udhibiti kamili juu ya Waislamu

Kwa mara nyingine tena, serikali ya Urusi imewahukumu Waislamu wa Crimea, kama ilivyofanywa kwa Waislamu wa Caucasus na jimbo la Volga kwa vifungo visivyo ingia akilini isipokuwa kwa kusema kwao tu "Mola wetu ni Mwenyezi Mungu" pekee, wakati wabakaji, wauaji wa wanawake na watoto, watu hatari ambao ndio tishio halisi kwa jamii wakipokea vifungo vya vidogo.

Upuuzi wa hukumu hii iliyolazimishwa ni kwamba kwa kweli msingi wa tuhma katika "kesi hii ya ugaidi" sio kupanga, kuandaa au kutekeleza vitendo vya kigaidi, bali ni kufanya mkutano wa hadhara (suhbet) katika msikiti huko Bakhchisarai, ambao ulihudhuriwa na makumi ya watu. Pia, Waislamu waliohukumiwa wanashtakiwa kwa kusoma vitabu vya Kiislamu na mazungumzo kuhusu Uislamu.

Hukumu hii ya kisiasa na sio ya kimahakama iliyopitishwa na mfumo potovu wa haki wa Urusi pia inafichua kufilisika kwake kutokana na ukweli kwamba simu, hard-drive, tablet, kipakatalishi na keyboard vinatambuliwa kama vifaa vya uhalifu katika uamuzi huu wa mahakama!!!

Hakuna ramani, hakuna michoro iliyo na mipango ya mashambulizi ya kigaidi, hakuna silaha, hakuna vilipuzi, hakuna hata mazungumzo ya kupanga chochote kinachohusiana na vurugu kama ushahidi katika vifaa vya vya kesi hii.

Waendesha mashtaka na majaji wamethibitisha mara kwa mara katika vikao vya mahakama kutokuwepo kwa dalili hata kidogo za shughuli za kigaidi kwa upande wa washtakiwa, wakimaanisha tu uamuzi mbaya wa Mahakama ya Upeo ya Shirikisho la Urusi wa 2003. Hati hii ya kimahakama ambayo haikutabanniwa kwa maslahi ya jamii ya Urusi ambayo sehemu yao kubwa ni Waislamu, bali ilipitishwa kwa maslahi ya serikali ya Urusi. Mnamo 2003 Mahakama ya Upeo ya Urusi ilithibitisha uamuzi hadaifu ambao uliyatambua mashirika kadhaa ya Waislamu kama ya kigaidi, hili lililenga kufikia malengo kadhaa katika sera ya ndani na nje.

Sura mbili na kutokuwa na hali ya kudumu kabisa kwa "uamuzi huu wa mahakama" ilithibitishwa na vitendo vya mamlaka ya Urusi vyenyewe, ambapo ilikaa kwenye meza ya mazungumzo na mashirika yaliyotambuliwa katika uamuzi huu kama ya kigaidi, iwe ihwan al-Muslimina au harakati ya Taliban.

Washiriki wote wa jinai wa muungano huu, iwe ni wachunguzi wa FSB (Huduma ya Usalama ya Shirikisho), waendesha mashtaka, majaji au wamiliki kutoka afisi za juu wanaosimama nyuma yao wanajulikana vyema - kinachotokea sio chochote isipokuwa ni uadui wao kwa Uislamu, ambao unachochewa na homa ya manjano na hofu isiyo na msingi na wakati mwingine na chuki ya kimfumo. Kwa kuwa wao wenyewe wamekubali mara kwa mara kwamba Hizb ut Tahrir haina uhusiano wowote na vurugu na ugaidi.

Lakini, watu na mashirika ambayo hayana uhusiano wowote na ugaidi na shughuli za kigaidi kwa wakati mmoja waliteuliwa kuwa wahalifu na magaidi.

Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu cha kimataifa ambacho kinazifunga amali zake kwa kazi ya kifikra na kisiasa pekee. Jaribio lolote la kuituhumu Hizb ut Tahrir kwa ugaidi linavunjwa na historia ya miaka 60 ya kazi Hizb katika nchi zaidi ya 40 za ulimwengu.

Kukataliwa kwa uamuzi huu na kukamatwa kwa watu wengi kulionekana katika majibu ya watu wengi na kuonyesha mtazamo wao na Waislamu wa Crimea. Maelfu ya Waislamu walishiriki katika mikutano kadhaa ya Waislamu (dua) ambayo ilifanyika kila pembe ya Crimea katika mkesha wa siku hiyo, ambapo waliswali katika kuwaunga mkono ndugu waliohukumiwa, wakimwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuawaachiliwa kwao huru haraka na kuwaandikia barua za kuwaunga mkono.

Kwa kuongezea, siku ya uamuzi, zaidi ya Waislamu 600 walielezea kutokubaliana kwao kwa kufika kortini huko Rostov juu ya Don na Simferopol, ambalo lilikuwa tukio lisilokuwa la kawaida katika zile zinazoitwa "Kesi za ugaidi". Kwa kweli mahakama hazikuweza kukubali watu wengi sana.

Hii ndio tathmini ya kweli ya Waislamu wa Crimea kwa vitendo kama hivi vya uhalifu vya mamlaka za Urusi, kivuli ambacho hakiwezi kuwatupa wasaliti wachache katika safu ya kile kinachoitwa Kurugenzi ya Kiroho ya Waislamu wa Crimea chini ya uongozi wa Emir Ali Ablaev, Wakiimba nyimbo za sifa kwa serikali ya Urusi wanaolenga kufikia ukiritimba wa kidini na kung'ang'ania nafasi za maimamu misikitini. Hawajali kuhusu vifungo na machozi ya watoto ambao baba zao wamefungwa.

Ukweli wa kuachiliwa kwa ndugu yetu katika imani Ernes Ametov bila shaka unaamsha furaha katika nyoyo zetu na nyoyo za Waislamu. Tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa kumrudisha Ernes kwa familia yake na watoto wake.

Lakini, hakuna haja ya kuwa wajinga hapa, tukiamini kuwa kuachiliwa kwa Ernest ni ushindi wa haki na ishara ya kutokuwa na upendeleo kwa mahakama za Urusi, kwa sababu mamia ya Waislamu, ambao vilevile hawana hatia na hawajafanya uhalifu wowote, wanaendelea kuchunguzwa au kutumikia vifungo vyao katika magereza na makoloni ya serikali hii ya kihalifu ya KGB.

Bila shaka, uongo na hila ambazo mamlaka za Kirusi zinasuka leo dhidi ya Uislamu na wafuasi wake yatakataliwa kabisa na Waislamu wa Urusi na Crimea.

Bila shaka, ukweli hauwezi kufichwa na uongo, hata ikiwa wanajaribu kuuficha kwa idadi kubwa ya kesi za jinai, hukumu ndefu na ripoti kadhaa zilizoagizwa kutokakwa majukwaa ya vyombo vya habari yanayounga mkono serikali.

(وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ)

“Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ukraine
Address & Website
Tel: 
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Urusi Yaendeleza Vita vyake dhidi ya Uislamu

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu