Jumamosi, 19 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ukraine

H.  27 Rajab 1440 Na: 1440/02
M.  Jumatano, 03 Aprili 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Harari

Wajumbe wa Hizb ut Tahrir nchini Ukraine walizuru Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Uchina mjini Kiev

Mnamo Aprili 2, 2019, wanachama wawili wajumbe wa Hizb ut Tahrir nchini Ukraine walizuru Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Uchina mjini Kiev. Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kampeni ya kiulimwengu ya Hizb ut Tahrir kuwasaidia Waislamu wa Uyghur nchini Uchina wanaokandamizwa kikatili.

Lengo la ziara hii ilikuwa ni kufikisha ujumbe wa Hizb ut Tahrir kuhusu kuteswa kwa Waislamu nchini Uchina – Wauyghur. Maafisa wa ubalozi wa China walikataa kupokea ujumbe wa Hizb kwa sababu kwamba ziara kama hizo zinapaswa kujulishwa mapema, lakini walikubali kupokea ujumbe huo.

Ujumbe huo ulijumuisha kutoka taarifa kwa vyombo vya habari ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir kwa anwani “Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki Na kuwanusuru Uyghur kutoka kwa Ukandamizaji wa Kihalifu wa Uchina” kwa Lugha tano: Kiarabu, Kichina, Kiuyghur, Kiingereza na Kiukraine.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliorodhesha kwa ufupi uhalifu wa mamlaka ya Uchina dhidi ya Waislamu Wauyghur ambao ni majaribio ya kukandamiza madhihirisho yoyote ya Kiislamu, kufunga Misikiti, kukataza kutekeleza ibada, kuzuia kufunga katika Mwezi mtukufu wa Ramadhani, hadi uanzishaji wa vituo vya vizuizi vikubwa, vilivyo ficha nyuma ya kuta zake zaidi ya Waislamu milioni mojackwa lengo la “kuwasomesha tena upya”. Ujumbe huo pia ulisisitiza uangalizi juu ya ukweli wa msimamo wa kijinga wa waitwao watawala wa Kiislamu, wanaopuuza uhalifu wa Uchina dhidi ya Waislamu kwa sababu ya uhusiano wa kibiashara, sio msimamo wa Ummah wa Kiislamu. Badala yake, na Ummah wa Kiislamu unahasira kutokamana na uhalifu wa serikali ya Uchina na muda sio mrefu watavunja minyororo waliyofungiwa kwayo na watawala wa Kiislamu wa wakati huu, kuhami wanaokandamizwa.

Ujumbe huo ulimalizika na onyo kuwa muda sio mrefu Khilafah ya Pili ya Uongofu kwa njia ya Utume itasimama katika ulimwengu wa Kiislamu na Khalifah atakuwa na jukumu la kuwalinda Waislamu wote ikiwemo watu Wauyghur. Wakati huo mahusiano ya asili kati ya Ummah wa Kiislamu na Uchina yatakuwa sawia kama mahusiano ya Kiongozi shujaa Qutaybah bin Muslim, Kiongozi wa jeshi la Waislamu, aliye walazimisha viongozi wa Uchina wa wakati huo kutii maagizo ya Waislamu na kulipa kodi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu asitishe mateso ya Waislamu Wauyghur na kuwaunganisha Waislamu wote katika serikali moja chini ya Mtawala mmoja – Khalifah, ambaye atawahami Waislamu wote wanaokandamizwa ulimwenguni kote. Amin.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ukraine
Address & Website
Tel: 
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Urusi Yaendeleza Vita vyake dhidi ya Uislamu »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu