Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  25 Rabi' I 1443 Na: HTY - 1443/03
M.  Jumanne, 02 Novemba 2021

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Kwa Wanazuoni Waliokusanyika jijini Sana’a
(Imetafsiriwa)

Kongamano moja lilifanyika jijini Sana'a tarehe 28/10/2021, lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanazuoni wa Yemen na Mamlaka Kuu ya Wakfu chini ya kichwa "Umoja wa Kiislamu... Fursa na Changamoto". Kongamano hilo liliandaliwa kwa njia ya matangazo ya satelaiti huku washiriki wakiwa kutoka Palestina, Iraq, Lebanon, Algeria na Iran. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

 [إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ]

“Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.” [Fatir: 28] Na yeye (saw) amesema:

«الْعُلَمَاءُ وَرَثَةُ الأَنْبِيَاءِ» “Wanazuoni ni warathi wa mitume” [Imepokewa na Abu Dawud na Tirmithi kutoka kwa Abi Adardaa‘ (ra)].

Tulipenda tuanze na aya hii tukufu na hadith hii tukufu ili kubainisha hadhi ya mwanachuoni mwenye manufaa katika elimu yake, mkweli katika kazi yake.

 [قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ]

“Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.” [Az-Zumar: 9].

Mnajua kwamba Mtume (saw) alitumwa na Qur’ani Tukufu, si kwa ajili ya kusomwa kwa ndimi tu, bali itumike juu ya watu duniani, ili (saw) awe na dola itakayoweka mipaka yake, kutekeleza hukmu zake, pigana nayo katika haki ya jihadi, kusimamisha uadilifu na kueneza kheri duniani kote. Haya yanadhihirika kwa uwazi katika Seera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), alilingania kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa utambuzi mjini Makka al-Mukarramah, na akaomba nusra kwa makabila na watu wenye nguvu mara kumi, mpaka Mwenyezi Mungu Mtukufu alimnusuru kwa maanswari wa Madinah al-Munawwarah, na kukawa na hijra na kusimamisha dola, kisha ufunguzi na uenezaji Uislamu kupitia dawah na jihad.

Kwa kuwa anwani ya kongamano lenu lililofanyika jijini Sana'a ilikuwa ni: “Umoja wa Kiislamu… Fursa na Changamoto”, ilistahiki kwetu kukuelezeni kwamba umoja wa Waislamu hautapatikana isipokuwa chini ya kivuli cha dola moja kwa Waislamu inayotawaliwa na Khalifa mmoja na kwa njia halali katika kusimamishwa kwake ambayo Bwana wetu Muhammad (saw) aliifuata.

Kufanya kazi ya kuunganisha Umma wa Uislamu kwa kusimamisha Dola ya Khilafah si suala muhimu kwa sababu ndio chimbuko la fahari ya Waislamu, na siri ya nguvu zao na kutoshindwa, bali pia kwa sababu ni faradhi ya kwanza na ya mwisho na sio faradhi yoyote, ndiyo inayotabikisha Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akimwambia Mtume wake (saw):

 [فَاحْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ عَمَّا جَاءَكَ مِنَ الْحَقِّ]

“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Al-Ma‘ida: 48]. Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ وَلا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Al-Ma‘ida: 49].

Kutawalisha Uislamu hakutapatikana chini ya dola inayochanganya kati ya Uislamu na usekula, kati ya mfumo wa utawala katika Uislamu na mfumo wa kijamhuri wa kidemokrasia wa kirasilimali, kati ya mfumo wa uchumi katika Uislamu na mfumo wa uchumi wa kirasilimali mikono yake ikiwa ni Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Baina ya dola inayolifanya fungamano la kitaifa kuwa ndilo linalowafunga raia wake na kujifunga na mipaka iliyochorwa na Kafiri Magharibi, na kati ya dola inayoufanya mshikamano wa imani ya Kiislamu kuwa ndio msingi na isiyofungwa na mipaka ya kitaifa, bali inafanya kazi kuziunganisha nchi za Kiislamu, baina ya dola ambayo katiba yake ni ya kisekula, inayotoka Ufaransa, na dola ambayo katiba yake inatokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume Wake (saw).

Uislamu bila ya dola hauwezi kutabikishwa kikamilifu, kwa sababu hukmu zake haziwezi kutabikishwa bila ya Khalifa, hivyo mipaka haidhibitiki na ufunguzi haufunguki, na heshima ya Uislamu haihifadhiwi isipokuwa na imamu, yaani Khalifa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema kweli: «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo” Imepokewa kwa Itifaki.

Umuhimu wa dola kwa Uislamu ulidhihirika mbele ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwani Amiri wa Waumini Omar, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, alipowakusanya ili kuchagua tarehe ambayo kwayo wataiandika historia na kuifuata kama kalenda, wakajadiliana wao kwa wao kutafuta tukio kubwa la kuanzia tarehe, kwa hivyo kuzaliwa kwa Mtume (saw), ujumbe wa Mtume (saw) na tukio la hijra. Akasema Ali (ra): “Tusemeni tangu tarehe ya Hijrah, kwani ndani yake kulikuwa na dola ya Waislamu, na nguvu yao... Hivyo basi Maswahaba wakapitisha hilo, ingawa kuzaliwa kwa Mtume (saw) lilikuwa ni tukio kubwa, na utume wa Mtume (saw) pia lilikuwa ni tukio kubwa vilevile. Lakini, maswahaba walichagua hijra, na kuasisiwa kwa dola ya Kiislamu kuanza kalenda ya Hijri kutokana nayo.

Hizb ut Tahrir - ilioanzishwa mwaka 1953 jijini Jerusalem - ilitambua kwamba Khilafah ni kadhia ya hatima kwa Waislamu, na kwamba kusimamishwa kwake ni faradhi, na kwa hivyo imefanya kazi ya kusimamisha Khilafah, na kwa zaidi ya nusu karne, wafanyakazi wake wamekabiliwa na madhara, kukamatwa, kufungwa gerezani na kuteswa, jambo ambalo lilipelekea baadhi ya wafanyakazi wao kuuawa shahidi katika baadhi ya nchi za Kiislamu. Licha ya haya, ilibakia thabiti katika haki, bila ya kuogopa lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake, mkweli na mwenye ikhlasi kwa idhini yake, Aliyetakasika, mpaka ikafanikiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, katika kuifanya Khilafah kuwa rai jumla miongoni mwa Waislamu, na hitajio hai kwao licha ya upotofu wote wa Makafiri, vibaraka wao, na mipango yao ya hila.

 [وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ]

“Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibraheem: 46]

Msilifanye kongamano hili kuwa ni nakala ya makongamano mengine kama hili ambayo yalifanyika hapo awali na kisha kumalizika. Kauli mbiu za kishindo zilitolewa katika kongamano kama vile "Ukombozi wa matukufu uko mikononi mwa waumini walio huru hivi karibuni" na "Kongamano hili ni nukta kianzilishi cha kufikia umoja wa Umma wa Kiislamu chini ya bendera ya Uislamu," wakati anwani ya kongamano hairegelei njia halali kutoka kwa Uislamu. Au hata mpango wa kufikia umoja wa Umma wa Kiislamu, na anwani hiyo inazungumzia fursa zilizopo ambazo washiriki wa kongamano wanaweza kuzifuatilia, pamoja na changamoto ambazo wanapaswa kuziepuka. Kwa hiyo je, mtu anayeutekeleza mfumo wa kirasilimali unaoongozwa na Amerika, inayoupiga vita Uislamu na watu wake, ambayo iliutangaza kwa kauli mbiu ya wazi tangu mwaka 2001 katika vita dhidi ya Uislamu kwa jina la “ugaidi”, anaweza kuwaunganisha Waislamu na kuutabikisha Uislamu?!

Wale wanaolingania kuunganishwa kwa Waislamu wanapaswa kutumia juhudi zao katika kutoa wito wa kusimamisha umwagaji damu katika mapigano ya wana wa Umma wa Kiislamu wao kwa wao na kuokoa nishati hiyo ili kupigana na maadui halisi Makafiri. Ni lazima wanyanyue bendera ya “La ilaha illa Allah (Hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu)” wakielea juu ya vichwa vyao na wasishikamane na mfumo wa kijamhuri au kauli mbiu zake, na wafanye kazi ya kuikata mikono ya Makafiri na mashirika yao… na kuifukuza Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na kukataa mikopo ya wazi inayotokana na riba inayotolewa na wao, na wanapaswa kulingania Uislamu, si Umoja wa Mataifa, mfumo wa kimataifa wala balozi wa Amerika kuhusu Yemen.

Nji ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika kusimamisha dola ya Kiislamu na kutawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu iko wazi na isiyo na utata, na haibadiliki kwa kubadilika kwa mahali au zama. Ilianza kwa ulinganizi wa Uislamu na ikamalizika kwa kusimamishwa kwa dola mjini Madina. Ilijitokeza katika hatua tatu zilizowakilishwa katika kuundwa kwa kundi ambalo linaichukulia imani ya Kiislamu kama msingi wa kifikra na uongozi wa kifikra, linalofahamu fikra na hukmu za Uislamu, na halichukui njia nyingine isipokuwa Uislamu ili kufikia kusimamisha Uislamu. Dola ya Kiislamu. Hivi ndivyo Mtume alivyowalea maswahaba zake mjini Makka katika nyumba ya Al-Arqam bin Abi Al-Arqam, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na shakhsia za Kiislamu zikatoka humo. Na kisha kuingia katika mvutano wa kifikra ili kukabiliana na fikra zote za Urasilimali zinazopenya kwetu leo hii, kuzifichua na kuziweka wazi na kuziweka fikra za Uislamu mahali pake, na mapambano ya kisiasa ya kufichua njama za Kafiri Magharibi zinazoanguliwa leo kama zilivyoanguliwa jana dhidi ya Uislamu na Waislamu, na kuomba nusra kutokwa kwa watu wenye nguvu miongoni mwa Waislamu, kisha kuchukua utawala wa kusimamisha dola ya Kiislamu kwa ajili ya kutawalisha Uislamu, kisha kuzijumuisha nchi zote za Kiislamu chini ya bendera ya Uqab, bendera ya Muhammad (saw).

Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu huwafichua wale wanaolingania utabikishwaji Uislamu kwa njia ya Kimagharibi kwa kisingizio cha wastani, wanaodai kufanyia kazi usuluhishi wa Uislamu na kuziunganisha nchi za Waislamu kwa vitendo vinavyoepukana haki na kilicho sahihi.

Magharibi ya kirasilimali, inayoongozwa na mhalifu Amerika  na Uingereza yenye hila, itaendelea kucheza karata anuwai ili kuzuia kudhihiri ukweli, hadi pale Mwenyezi Mungu atakapoidhinisha kudhihiri kwake na kuwateremshia ushindi na nusra yake Waislamu wakweli. Hizb ut Tahrir - kiongozi asiyewadanya watu wake - inakualikeni kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Yeye (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” [Imepokewa na Ahmad kutoka kwa An-No‘man ibn Basheer (ra)]. Mwenyezi Mungu (swt) pia amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu