Jumamosi, 14 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  10 Rabi' I 1447 Na: HTY- 1447 / 04
M.  Jumanne, 02 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chuki na Uhalifu wa umbile la Kiyahudi mjini Gaza na Yemen
Haitakomeshwa isipokuwa kwa Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, Mlinzi wa Matukufu ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatatu, tarehe 01/09/2025, mazishi yalifanyika kwa miili ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi jijini Sana’a, Ahmad Ghalib Nasser al-Rahwi, pamoja na kundi la mawaziri: Jaji Mujahid Ahmad Abdullah Ali – Waziri wa Haki na Haki za Binadamu, Mu’een Hashim Ahmad al-Muhaqiri, Waziri wa Uchumi, Viwanda na Uwekezaji, Radwan Ali al-Rubai’i – Waziri wa Kilimo, Uvuvi, na Rasilimali za Maji, Jamal Ahmad Ali ‘Amir – Waziri wa Mambo ya Nje na Wageni, Ali Seif Muhammad Hasan – Waziri wa Umeme, Nishati na Maji, Ali Qasim Hussein al-Yafi‘i – Waziri wa Utamaduni na Utalii, Samir Muhammad Ahmad Baj’alah – Waziri wa Masuala ya Kijamii na Leba, Hashim Ahmad Abdurrahman Sharafuddin – Waziri wa Habari, Muhammed Ali Ahmad al-Muwallad – Waziri wa Vijana na Michezo, Muhammad Qasim al-Kubsi – Mkurugenzi wa Afisi ya Waziri Mkuu, Zahid Muhammad al-'Amadi – Katibu wa Baraza la Mawaziri; huku hatima ya mawaziri wengine waliokuwa kwenye mkutano haikutajwa, baada ya kulengwa mnamo siku ya Alhamisi adhuhuri, 28/08/2025, na uvamizi wa umbile la Kiyahudi dhidi yao katika mji mkuu Sana’a wakati wa mkutano, siku nne baada ya kulenga Kampuni ya Mafuta na Kituo cha Umeme cha Hazir.

Wale ambao Mwenyezi Mungu amewadhalilisha wasingeweza kukiuka ardhi zetu isipokuwa wakiwahakikishiwa uwepo wa watawala wa khiyana wanaowatengenezea njia, ndege zao zikiruka juu ya Bahari ya Nyekundu—huku Salman bin Abdul Aziz ikiwa kwenye mwambao wake wa kulia, na al-Sisi na al-Burhan kwenye mwambao wake wa kushoto, na kwa hakika wanarusha kutoka katika visiwa vyake na kutoka katika visiwa vya Yemen, ambavyo Imarati Muhammad bin Zayed ina kambi zao, na watawala wengine wa Waislamu na walio nyuma yao. Na wasingefanya uvamizi huo dhidi ya ardhi za Waislamu bila ya kushirikiana na watawala hawa, kuegemea kwao kwenye maisha ya dunia dhidi ya umbile hili myakuzi wa Palestina tangu mwaka 1948, kushindwa kwao kukabiliana nalo, na kusubutu kwao dhidi ya watu wao pindi wanapolaani juu yao uovu wa matendo yao machafu.

Kulengwa kwa Yemen na umbile la Kiyahudi kusingetokea isipokuwa kwa kukosekana utawala wa Uislamu, na kutabanniwa kwa sheria ya kimataifa inayowakilishwa na Umoja wa Mataifa na wale walio nyuma yake kama kibla chao, na malipo kama hayo ya kuacha kutawala na Uislamu ni matokeo ya kutarajiwa tu – hadi wanasiasa wa Yemen waregee kwenye fahamu zao na kuuweka Uislamu katika utabikishaji ndani ya Khalifah ya pili kwa njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Surat Ghafir: 51]. Na Mtume (saw) amesema:

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” [Musnad Ahmad 18406]

Khilafah inayotawala kwa Uislamu, inayounganisha ardhi za Waislamu, na kung'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake kwa msafara wa majeshi ya Waislamu, baada ya kuvamia mipaka yake kwa takriban miaka themanini, na sio tu kuilenga kwa makombora kutoka mbali! Bila hii, umbile hilo halifu litaendelea na vitendo hivi vya uhalifu.

Hakika Mwenyezi Mungu ametukirimu kwa Uislamu, na ametutukuza kwao, na akatuteremshia Sharia yenye kutatua matatizo yote ya dunia na kubainisha kwayo njia ya uongofu. Basi tunaibadilishaje kwa sheria ya dhulma iliyotungwa na mwanadamu (sheria ya Umoja wa Mataifa) ambayo kanuni zake zilitungwa na makafiri wakoloni?! Dunia leo inaturusha kwa upinde mmoja, kwa hivyo ni lazima tuzingatie yale aliyoyasema Mola wetu Mlezi na tutabikishe Uislamu kwa mapana, kikamilifu, na bila upungufu, na tuongoze watu wa Umma huu kuelekea ukombozi wa ardhi za Waislamu na wanadamu wote kutokana na dhulma ya ubepari. Na sisi katika Hizb ut Tahrir tunaendelea na kazi yetu ya kunyanyua utambuzi wa Ummah, tukitafuta nusrah kutoka kwa watu wenye nguvu na ulinzi, na kubeba mradi safi wa Kiislamu mpaka Mwenyezi Mungu atukirimu kwa ushindi na ufunguzi kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili juu ya njia ya Utume, na tunakulinganieni mushirikiane nasi ili kusimamisha faradhi hii kubwa.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surat Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu