Jumatano, 09 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  5 Rabi' II 1447 Na: HTY- 1447 / 06
M.  Jumamosi, 27 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Msimamo kwa Sherehe za Maadhimisho ya Mapinduzi Mawili ya Septemba
Moja yaliingiza Usekula nchini Yemen na Mengine Yalitoa Wito wa Kuuimarisha!
(Imetafsiriwa)

Katika mwezi wa Septemba wa kila mwaka Yemen ina matukio mawili; la kwanza mnamo tarehe 26 Septemba 1962 ambayo ni kumbukumbu ya kupinduliwa kwa mfumo wa kifalme nchini Yemen Kaskazini, na la pili mnamo tarehe 21 Septemba 2014 ambayo ni kumbukumbu ya kuingia kwa Mahouthi jijini Sana’a ambayo ilisababisha udhibiti wao wa mikoa ya kaskazini.

Tukio la kwanza linachukuliwa na kile kinachoitwa uhalali – haswa Chama cha Congress, chama cha Jumuiya ya Mageuzi ya Yemen, na vyama vyengine washirika – na wasemaji wake kwa vyombo vya habari na wafuasi, kama chanzo cha kushambulia vuguvugu la Houthi na kuwaita watu kusimama dhidi yake, ikizingatiwa kuwa ni upanuzi wa utawala wa Uimamu kabla ya 1962. Kitendawili cha ajabu ni kwamba Mapinduzi ya 1962 hayakuwaokoa watu wa Yemen lakini badala yake yaliwasalimisha kwa makafiri wa Magharibi. Kuhusu tukio la pili; kumbukumbu ya kuingia kwa Mahouthi jijini Sana’a, ambayo wamekuwa wakiadhimisha kila mwaka, hayakusababisha utabikishaji wa Uislamu bali yaliendelea kwenye njia ya mtangulizi wake katika kutekeleza mfumo wa jamhuri wa kisekula, na kuubeba Uislamu kama kauli mbiu tu chini ya jina la maandamano ya Qur’an! Na katika matukio haya mawili kelele za vyombo vya habari hupanda, ambazo vumbi lake sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Yemen lazima tuliondoe kwa watu wa imani na hekima. Mapinduzi hayo mawili yanaungana katika nini, na yanatofautiana katika nini?

Mapinduzi hayo mawili yanaitukuza mipaka ya Sykes-Picot, iliyochora na kukitisha mizizi mipaka kati ya Yemen na Hijaz na Sham na Iraq na Iraq na Misri na Algeria, nk ya ardhi za Waislamu, ambazo zilibakia chini ya bendera moja ya Waislamu licha ya kiwango cha dola ya Khilafah ambayo ilifika na kuitwa mgonjwa. Yaani, walilitukuza lile fungamano duni la kitaifa ambalo lilimeuchana Umma vipande vipande na leo hii unalipinga, ndani ya kivuli cha mauaji na umwagaji damu, kuwapa ushindi watu wake katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Leo Ummah unatamani kuwang'oa Mayahudi, na kinachouzuia ni mipaka hii ya kitaifa ambayo makafiri wa Magharibi waliipanda baina yake.

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]

“Hakika Waumini ni ndugu …” [Al-Hujurat: 10]. Na Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha mifarakano baina ya Waislamu, akasema (swt):

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aal-e-Imran: 103]. Kwa hiyo sisi ni Ummah mmoja tofauti na wanadamu, na fungamano ambalo lazima litufunge ni Aqida (itikadi) ya Kiislamu chini ya dola moja na mtawala mmoja.

Pande zote mbili za mapinduzi hayo mawili zainua bendera ya Sykes-Picot, kuitakasa na kuitukuza, na zinatumikia ukoloni, iwe wanajua au hawajui, na wanamfungulia mashtaka anayeitupa chini, na ni sheria ya kikoloni ya Magharibi. Na bendera hii ambayo pande zote mbili zinaitakasa ni bendera ya jahiliyyah (kabla ya Uislamu), kiupofu, kikabila, ambayo haiwawakilishi Waislamu na haitoki katika Aqidah ya Kiislamu. Badala yake pande zote mbili zilifanya kazi ya kupanda utakatifu kwa ajili yake miongoni mwa vizazi. Kwa hivyo Waislamu nchini Yemen lazima watambue kwamba bendera ya Sykes-Picot ni bendera ovu ya kikabila ya kijahiliya kutoka kwa mabaki ya ukoloni. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitutahadharisha dhidi ya kuinyanyua na kuilingania, akasema (saw): «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Iacheni kwani hakika ni uvundo.” [Sahih Muslim 2584]. Mtume (saw) amesema: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ» “Si miongoni mwetu anayelingania `asabiyyah (ukabila).” Na kinyume chake dola ya Kiislamu ina Liwa’a na Rayat (bendera); Liwa’a ni nyeupe na imeandikwa “La ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah” juu yake kwa maandishi meusi, «إِنَّ النَّبِيَّ ﷺ دَخَلَ مَكَّةَ يَوْمَ الْفَتْحِ وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضُ» “Mtume (saw) aliingia Makka siku ya ufunguzi wake na bendera yake ilikuwa nyeupe.” [Ibn Majah kutoka kwa Jaber]. Na Raya ni nyeusi na imeandikwa “La ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah” kwa maandishi meupe. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَأُعْطِيَنَّ الرَّايَةَ غَداً رَجُلاً يُحِبُّ اللهَ وَرَسُولَهُ، وَيُحِبُّهُ اللهُ وَرَسُولُهُ، فَأَعْطَاهَا عَلِيّاً» “Kesho nitampa bendera mtu ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda, basi akampa ‘Ali.” [Bukhari na Muslim]. Je, Mtume (saw) alimpa Ali bendera ya Sykes-Picot?!

Mapinduzi ya kwanza yalitenganisha dini na maisha, na ya pili yalidumisha utenganishaji huo, na hayakuregea kwenye asili ya Uislamu, Dini isiyotengana na dola. Badala yake waliifanya nchi kuugua chini ya uzito wa Umoja wa Mataifa, mfadhili wa mfumo wa kisekula. Ali Saleh aliyefariki alitia uziwi masikio yetu, na leo kile kinachoitwa uhalali pamoja na makundi yake yote, kwa kufanya kazi na hati za Umoja wa Mataifa. Na kile Al-Alimi alichosema katika hotuba yake mnamo Alhamisi, 25/9/2025, kwenye Umoja wa Mataifa, “…Kwa pamoja, tuliahidi kwamba taasisi hii itasimama kama mlinzi wa utu wa binadamu, wa haki ya watu ya kupata maisha ya staha, usalama, maendeleo, na amani…” na akaongeza: “Natoa wito leo kwa ajili ya kuanzishwa kwa muungano madhubuti wa kimataifa... kuikomboa nchi yetu kutokana na msiko wa mashirika ya wanamgambo na magaidi ya kila aina.”

Kwa hayo aliusifia Umoja wa Mataifa huku akijua kuwa ni mshirika wa jinai katika maafa yote yaliyoikumba Yemen na maeneo mengine ya ardhi za Waislamu na yanayojiri leo mjini Gaza. Na kinyume chake Mahdi Al-Mashat alisema mnamo Jumanne, tarehe 17/06/2025: “Hakuna mkataba wa kimataifa unaomruhusu mtu yeyote kumwachilia mbwa wake mwenye kichaa kwa yeyote amtakaye, kwani Mkataba wa Umoja wa Mataifa ni mkataba wa udhibiti wa mahusiano ya nchi na hatutaruhusu uvunjwe.” Huu ni wito, mwaliko ulio wazi wa kuitupa Shariah ya Mwenyezi Mungu nyuma ya migongo yao, na kuhukumu kwa utwaghuti ambao Mwenyezi Mungu amesema kuwahusu:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنْزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنْزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيداً]

“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa Taghut (njia ya upotofu), na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [An-Nisa: 60]. Na ilitosha kwake kujibu kauli ya Mwenyezi Mungu:

[وَالَّذِينَ اجْتَنَبُوا الطَّاغُوتَ أَنْ يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوا إِلَى اللَّهِ لَهُمُ الْبُشْرَى فَبَشِّرْ عِبَادِ]

“Na wale wanao jiepusha na Taghut, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja wangu.” [Az-Zumar: 17].

Uislamu ni Aqida (itikadi) ya kweli iliyo wazi: “La ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah,” ambayo kwayo huchipuza mfumo unaopanga nyanja zote za maisha – kisiasa, kiuchumi, mahusiano ya kimataifa, nk – na bendera yake ni Al-‘Uqab. Na dola ya Uislamu ilijumuisha Najd, Hijaz, Yemen, Iraq, Misri na ash-Sham, na ikaenea mpaka ikafika Andalus upande wa Magharibi, Indonesia upande wa Mashariki, Chechnya na Crimea upande wa Kaskazini, na Sahara Kubwa upande wa Kusini, ikivuka mifungamano duni ya kitaifa, kikabila na rangi. Mafungamano yote hayo yaliwekwa ili kuwafarakanisha Waislamu na kuwazuia wasikusanyike chini ya uongozi wa Khalifa mmoja. Mtume (saw) amesema: «إِذَا بُويِعَ لِخَلِيفَتَيْنِ فَاقْتُلُوا الْآخِرَ مِنْهُمَا» “Ikichukuliwa ahadi ya utiifu (ba’yah) kwa makhalifa wawili, basi muuweni wa pili wao.” Na ubwana lazima uwe kwa Shari‘ah, na mamlaka kwa Ummah, ukiyaweka mkononi mwa yule ambaye unampa bay‘ah kutawala kwa Uislamu chini ya Khilafah Rashida wa pili kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu amesema:

[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ]

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Ghafir: 51].Na Mtume (saw) akasema: «ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»“…Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Basi jihadharini, enyi watu wa Imani, na kuwafuata wanaopiga kelele.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu