Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 540
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kufuatia mashambulizi ya kikatili ya Gaza na umbile la Kiyahudi, umbile hilo lilipanua mashambulizi yake ya ardhini huko Gaza mnamo 20 Machi 2025. Wakati huo huo, viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Waislamu wanashughulika kumfurahisha Farauni wa Washington, Trump, na majeshi yetu yanatumiwa katika vita vya uasi. Tunaweza kuuliza majeshi ya Waislamu: Je, si ndugu zenu Waislamu ndio walioifanya Marekani ionje kushindwa nchini Iraq na Afghanistan?
Kufuatia kukiuka makubaliano duni ya usitishaji mapigano ya umbile la Kiyahudi mnamo siku ya Jumanne, 18/03/2025, na kuanza tena kwa mauaji ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao ni wanawake, watoto na wazee, Hizb ut Tahrir / Sweden iliandaa kisimamo katika robo ya Waislamu wa mji mkuu, Stockholm, chenye kichwa “Mauaji dhidi ya Raia mjini Gaza hivi sasa! Simama kwa Heshima!”
Televisheni ya serikali ya Pakistan ilisema mnamo 19 Machi 2025: “Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel.” Hivi ndivyo watawala wa Pakistan walivyolaani hujuma ya Mayahudi na jinai zake zinazoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza! Bila kusonga askari au kuinua silaha!
Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu, hasa zile zinazoizunguka Palestina: Je, kuna udhuru wowote uliobaki kwa wanaoomba msamaha? Je, kuna hoja yoyote iliyobaki kwa wanaolaani? Vipi mnaweza kuona na kusikia uvamizi na mauaji ya Mayahudi hali mmekaa katika sehemu zenu, bila kutikisika, badala ya kuelekea katika ardhi ya Al-Ribat, Palestine Ardhi Iliyobarikiwa, ili kurudisha uvamizi wa Mayahudi na kuliondoa umbile lao?
Enyi Majeshi “Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”
Maneno yanashindwa kuelezea uhalifu huu wa kutisha katika mwezi huu mtukufu. Mayahudi wa Netanyahu na Marekani ya Trump wanawaonea watu wasio na hatia huku wakiwa wamelala, wakitumia ndege 100, zikiwemo ndege za kivita za Marekani, kulenga mahema yaliyojaa raia, kwa kisingizio kwamba wapiganaji wachache wa upinzani wapo. Waliwafuatiulia huku kukiwa na udanganyifu waliouita "usitisha mapigano"!
Khilafah ni Izza na Njia ya Wokovu kwa Wanadamu! Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 104 H wa kuvunjwa dola ya Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab al-Muharram 1342 H sawia na 03/03/1924 M mikononi mwa wahalifu wa Kiarabu na Kituruki.