Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Kongamano la kila Mwaka la Khilafah: “Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah”
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir/Wilayat Tunisia ilifanya kongamano lake la kila mwaka la Khilafah mnamo siku ya Jumamosi, 26 Aprili 2025, katika ukumbi wa mikutano kwenye makao makuu ya Hizb katika makutano ya barabara ya Sakra katika mji mkuu, Tunis, chini ya kichwa: “Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah” Kumbi mbili zilizotengwa kwa ajili ya wageni zilijaa idadi kubwa ya wanaume na wanawake waliofika kwenye kongamano hilo kutoka pande zote za ardhi ya kijani ya Tunisia.