- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kutoka Pakistan hadi ash-Sham: Je, Kweli Tulimshinda Bashar au Tulimbadilisha tu kwa Nakala zake?!
(Imetafsiriwa)
Kutoka Pakistan, tulifuatilia kwa karibu mapinduzi yaliyobarikiwa ambayo yalilipuka huko ash-Sham zaidi ya miaka kumi na tatu iliyopita. Tulifurahishwa na ishara za kheri na alfajiri ya Khilafah, tukitarajia kwamba yataleta kila lililo jema—hasa pale watu wa ash-Sham walipoinuka wakiimba, “Hatuna mwengine ila Wewe, Ewe Mwenyezi Mungu,” na “Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu... ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,” na “Umma unataka Khilafah ya Kiislamu.” Nyoyo zetu zilikuwa zimeshikamana hasa na ash-Sham, kwani Mtume (saw) aliisifu katika Hadith nyingi, zikiwemo Hadith zake:
«عَلَيْكُمْ بِالشَّامِ، فَإِنَّهَا صَفْوَةُ بِلَادِ اللهِ يَسْكُنُهَا خِيرَتُهُ مِنْ خَلْقِهِ» “Ni lazima muende katika ardhi ya ash-Sham, kwani ndio bora zaidi ya ardhi ya Mwenyezi Mungu; waja wake wema wanaishi humo.” (Imepokewa na al-Tabarani)
Wakati miji yote ilipokombolewa kutoka mikononi mwa dhalimu wa ash-Sham, Bashar, tulifikiri ushindi ulikuwa umefika. Tuliamini kuwa wakati umefika wa kusimamishwa Khilafah kwa njia ya Utume—hali ile ile iliyobashiriwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)—ambayo itatawala kwa Qur’an na Sunnah na ilionekana iko tu kwenye kona. Walakini, kuvunjwa moyo kulilingana na ukubwa wa mihanga, na usaliti ulifuata takriban miezi sita baada ya wanamapinduzi kuingia Damascus kwa takbira na shangwe za ushindi. Usaliti ulikuja kutoka kwa wale tuliotarajia wangejenga upya juu ya magofu—sio kujisalimisha kwao!
Tulitarajia wanamapinduzi, baada ya kuuangusha utawala wa kihalifu wa Ba’ath, wangesimamisha dola inayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt), kuinua bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na kuichukua Qur’an na Sunnah kama katiba na njia yake. Dola ambalo watu walijitolea muhanga—sio tu kwa miaka kumi na tatu, lakini tangu utawala wa Ba’ath uwanyonge kwa zaidi ya miongo mitano. mihanga ilitoka ndani ya Syria na kutoka kwa mujahidina waliokuja kutoka duniani kote kusaidia ndugu zao—si ili mfumo ule ule wa kisekula waliouasi urudishwe tena, wakati huu kwa sura mpya na lugha ya udanganyifu!
Badala ya kutangaza waziwazi kwamba walikuwa wakifanya kazi ya kusimamisha utawala wa Uislamu, bila ya kumuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt)—kama tulivyowajua kuwa walikuwa katika miaka ya jihad na mapigano. Tuliwaona viongozi wa makundi na vyombo vya kisiasa katika maeneo yaliyokombolewa wakikimbilia kujenga madaraja na tawala za kihalifu zisizo chini ya kiuovu kuliko Bashar. Walikwenda kwa utawala wa kihaini wa Uturuki, ambao uliiuza Aleppo bila kusita, mara kwa mara wakasaliti Idlib, na kushirikiana na Urusi na Iran chini ya miundo ya Astana na Sochi.
Kisha tuliona mikono ikinyooshwa hadi Marekani kupitia ziara rasmi na uratibu wa kisiasa. Tuliona hata wawakilishi wao wakishiriki katika makongamano yaliyofadhiliwa kimataifa, wakitoa kauli za kusifu "uhalali wa kimataifa" na taasisi zake! Hakukuwa na dhalimu duniani au dikteta miongoni mwa watawala wa Kiarabu—ambaye dhulma, njama, na pesa chafu ziliwatesa watu wa ash-Sham—ambaye hakutembelewa na kukumbatiwa kwa uaminifu. Hata wale waliomlipa Trump mabilioni kwa udhalilifu, wakitoa punguzo la saba kwa ash-Sham!
Usaliti haukuishia kwenye mipaka ya ash-Sham. Ulizama chini sana kiasi kwamba kimya kilidumishwa mbele ya jinai za umbile la Kiyahudi huko Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hata mashambulizi yake ya mara kwa mara katika eneo la Syria yalipuuzwa—kana kwamba utukufu wa mujahid haukuwa na maana tena! Kibaya zaidi, sauti kutoka ndani ya utawala na vyombo vyake zilianza kutaka kuhalalishwa mahusiano na umbile la Kiyahudi—wakati mwingine kwa jina la “uhalisia wa kisiasa,” na wakati mwingine chini ya pazia la “kujadiliana ili kuregesha Milima ya Golan”, au kujiunga na miradi ya usaliti kama Makubaliano ya Abraham. Hizi ni njama za Marekani za kulioanisha kwa nguvu umbile la Kiyahudi ndani ya mwili wa Mashariki ya Kati mpya!
Kwa hivyo, ni utawala wa aina gani huu, ambao hauhisi ulinzi kwa damu, heshima, na ardhi ya Waislamu? Je, ni uhalali gani uliobakia kwa utawala uliouza dini na njia yake, na kuasi kanuni za Kiislamu ambazo kwa ajili yake watu wenye ikhlasi walijitolea maisha yao? Iko wapi adhabu ambayo dada zetu waliofiwa na wajane huko ash-Sham walitamani sana baada ya kuwapoteza watoto wao, kufanywa wajane, kufanywa mayatima na kuvunjiwa heshima yao? Iko wapi haki kwa wahalifu?! Mwenyezi Mungu (swt) Mtukufu asema:
[وَمَن قُتِلَ مَظْلُوماً فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَاناً فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ إِنَّهُ كَانَ مَنصُوراً]
“Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.” [17: 33].
Na Yeye (swt) asema:
[وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ]
“Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.” [2:179].
Ama kuhusu katiba, badala ya kuwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw), walianza kushindana katika kuandaa nakala zinazofanana na katiba za kisekula za Magharibi. Kibaya zaidi, walishiriki katika sura ya kuandika katiba mpya chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa-kana kwamba mapinduzi hayakuibuka ili kuuangusha utawala wa kitaghut (kibabe), bali tu kuubadilisha kwa utawala mwingine dhalimu katika nyuso mpya! Je! ni ushindi wa aina gani unaogeuza damu ya mashahidi kuwa biashara? Ni aina gani ya utawala muongofu unaosimamiwa kutoka vyumba vya kijasusi vya Uturuki na Marekani?
[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ]
“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [5:50]
Umma haukutoa mhanga mali na maisha yake ili nakala mpya ya utawala wa Bashar iregeshwe—iwe na ndevu au isiyo na ndevu! Damu ya watoto wa Ghouta, waliohamishwa kutoka Daraya, na mujahidina huko Idlib bado wanapiga kelele: "Iko wapi dola muliyotuahidi?!" Umma ungali unawangoja wenye ikhlasi—wale waliosimama imara juu ya maadili, ambao hawakuuza dini yao au damu ya watu wao, wanaokataa kujisalimisha kwa mfumo fisadi wa kimataifa, na ambao wanaamini kwamba wokovu wa kweli uko tu katika kusimamisha dola ya Kiislamu: Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume.
Enyi wenye ikhlasi katika ash-Sham: Njia ya mapinduzi imepotoka na kuingia katika dimbwi kubwa, na ni lazima irekebishwe kabla ya kuchelewa—kabla majuto hayajafaa kitu. Kinachohitajika ni uongozi wenye fahamu, wenye ikhlasi unaonyenyekea kwa Mwenyezi Mungu (swt), unaochukua uongofu tu kutoka katika Shari’ah Yake, unaokataa udhalilifu katika Dini yake, na hautalegeza msimamo katika lengo la kusimamisha utawala wa Kiislamu na kung’oa mifumo yote ya ukafiri—pasi na kujadiliana nao au kutegemea msaada wao. Hii hapa Hizb ut Tahrir—kiongozi mwaminifu asiyewadanganya watu wake—fanyeni kazi pamoja nayo na muipe nusra yenu. Ubadilisheni uongozi wa sasa uliofeli kufikia yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake, na waumini, na ambao umeshindwa sana kuheshimu mihanga yenu mikubwa. Mapinduzi hayapaswi kuishia kwenye milango ya Marekani na vibaraka wake. Kwa kweli, hayajakwisha. Mapumziko ya shujaa yamechukua muda mrefu sana – ni wakati wa kuregesha mapinduzi kwa njia yake sahihi. Basi simameni, enyi wenye ikhlasi, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu (swt) huwanusuru wanaomnusuru, na mwisho mwema ni kwa wacha Mungu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [8:24]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal al-Muhajir – Wilayah Pakistan