- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kipindi cha “Nampenda Muhammad” nchini India Chafichua Udhalilifu wa BJP Uliofinikwa na Imani ya Wengi
(Imetafsiriwa)
Kipindi cha “Nampenda Muhammad” kilichozuka kote Uttar Pradesh Septemba hii kimefichua tena utata wa kisaikolojia na kisiasa unaoendesha Chama tawala cha Bharatiya Janata (BJP) cha India. Kile kilichoonekana, juujuu, kuwa mzozo wa sheria na utaratibu kuhusu mabango ya kidini na machapisho ya mitandao ya kijamii, kwa kweli, kinaakisi wasiwasi mkubwa zaidi – udhalilifu unaojificha nyuma ya onyesho la imani ya wengi.
Katika miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kanpur na Bareilly, Waislamu walioonyesha mabango au kutuma ujumbe unaotangaza “Nampenda Muhammad” walijikuta wakikabiliwa na FIR, kuwekwa kizuizini, na vitisho vya kubomolewa nyumba zao. Serikali ya jimbo ilihalalisha vitendo hivi kama hatua za kuzuia machafuko yanayoweza kutokea. Lakini kutokuwepo kwa vurugu yoyote au maandamano yaliyopangwa kunaonyesha kwamba tatizo halikuwa kauli mbiu, ilikuwa ni utambulisho wa wale waliotoa sauti kwa ajili yake. Kwa upande mwengine, madhihirisho ya umma ya imani ya Kibaniani au yatra ya kidini yanachukuliwa kama ya kawaida na hata kusherehekewa. Unafiki huu unafichua wasiwasi na utata wa kisaikolojia wa muda mrefu wa BJP: siasa zinazodai kutawala lakini zinaendeshwa na hofu.
Wasiwasi wa BJP umefungamana sana na urithi mkubwa wa Waislamu wa India, ambao unaendelea kutawala mandhari ya kihistoria na uzuri wa nchi. Kuanzia ukuu wa usanifu wa Mughal – Taj Mahal na Ngome Nyekundu ya Delhi hadi uboreshaji wa ushairi wa Kiurdu na muziki wa kitambo, mchango wa Waislamu haupingiki na wa kudumu. Lakini ni mwonekano huu hasa unaochochea udhalili wa BJP. Kwa kuwa hawawezi kufuta urithi huu, BJP inajaribu kuubadilisha jina, kuubadilisha dura, au kuufunika kisiasa, kuipa miji majina mapya, kuandika upya vitabu, na kuhoji makavazi ya kihistoria. Kinachoonekana kama mwamko wa kitamaduni mara nyingi ni mapambano dhidi ya uwepo usioepukika wa historia ya Waislamu wa India - historia yenye ushawishi mkubwa sana kuukataa.
Ili kuelewa hili, mtu lazima arudi kwenye mwanzo wa fikra za BJP. Iliyozaliwa mwaka wa 1980 kutoka kwenye majivu ya Jana Sangh, chama kilibaki pambizoni hadi kilipogundua mvuto wa kihisia na wa uchaguzi katika harakati za Ram Janmabhoomi mwishoni mwa miaka ya 1980 na kubomolewa kwa Masjid Babri mnamo 1992 ilikuwa nukta ya mabadiliko ya kisiasa.
Hapa ndipo udhalili ulipochukua sura ya kitaasisi. Mradi wa BJP wa Hindutva, ingawa unaonyeshwa kama kufufuka kwa utamaduni, kimsingi ulikuwa wa kiutendaji – harakati isiyoainishwa na kile inachowakilisha, bali na nani inayempinga. Inaiweka historia kama simulizi ya unyanyasaji wa Kibaniani na utawala wa Waislamu, ikitafuta kubadilisha mizani ya usawa huo kupitia nguvu za kisiasa. Kila uthibitisho wa dhihirisho la Waislamu – iwe msikiti, kofia, au sasa kauli mbiu – inakuwa nembo ya ukumbusho wa udhalilishaji wa kufikirika.
Mzozo wa “Nampenda Muhammad” unaendana vyema na muundo huu. Mwitikio wa serikali ya BJP wa kupita kiasi haukuwa kuhusu kudumisha utulivu bali zaidi kuhusu kuimarisha uongozi. Kwa kugeuza kitendo cha kujitolea kuwa kitendo cha ukaidi, serikali iliimarisha ujumbe: kwamba madhihirisho ya kitambulisho cha Waislamu yatavumiliwa tu chini ya idhini ya wengi. Tingatinga, FIR, na majazi ya “kugonga-kupaka rangi” ya Waziri Mkuu yote yalitumika katika usanifisha mamlaka. Utendaji huu wa utawala, unaojirudia katika matukio mengi licha ya mauaji ya Waislamu ya Gujrat, unaficha udhaifu mkubwa zaidi – hofu kwamba kitambulisho cha Kibaniani kinahitaji ulinzi katika nchi ambayo Mabaniani ni karibu 80% ya idadi ya watu.
Hicho ndicho kitendawili cha BJP. BJP haiwezi kudumisha siasa zake bila mzozo kwani maelewano hayatoi ujira wa uchaguzi. Lakini bila ujira wowote maelewano ya ajabu kati ya Waislamu na Mabaniani yaliyodumishwa kwa karne nyingi katika bara hilo ndogo kwa sababu ya utawala adilifu chini ya kivuli cha Uislamu. BJP wala katiba ya kisekula ya India haiwezi kudhamini utulivu kama huo kwa sababu ya dosari kadhaa ndani yake na kwa vyama tofauti vinavyopigania madaraka lazima viwe vya kisekula ili kutawala lakini mara nyingi vinakuja pamoja ili kushinda jambo ambalo hugawanya jamii.
Mfumo wa uadilifu wa Uislamu kwa karne nyingi ulicheza dori kuu katika kudumisha maelewano katika bara ndogo kwa kuingiza uadilifu, uwajibikaji, na usawa katika utawala. Ukiwa na mizizi katika kanuni ya Quran kwamba wanadamu wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), watawala wa Waislamu walitarajiwa kutenda kama walinzi wa haki badala ya wamiliki wa madaraka. Mahakama mara nyingi zilijumuisha mila za ndani na sheria za Kibaniani kwa wasio Waislamu, ambazo ziliheshimu utofauti huku zikidumisha utulivu. Kwa mfano, chini ya utawala wa Mughal, mfumo wa qazi ulikamilishwa na panchayat za wenyeji, kuhakikisha kwamba jamii zinaweza kusuluhisha mizozo ndani ya miundo inayojulikana. Kodi kama vile jizya pia ziliambatana na dhamana za ulinzi kwa wasiokuwa Waislamu. Kimsingi, fiqhi ya Kiislamu nchini India ilifanya kazi kama muundo wa kuleta utulivu.
Kwa India, hii kwa mara nyengine tena ndio njia ya kusonga mbele, na sio siasa za mizozo.
Mwenyezi Mungu (swt) alimtuma Mtume Wake Muhammad (saw) kudhihirisha haki hii. Yeye (swt) asema:
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawbah 9:33].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Malik – Wilayah Pakistan



