Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hotuba ya Nne Katika Kongamano: ‘Vijana Waislamu …Waanzilishi wa Mabadiliko Msingi’

Msimamo Mpya na Mwamko wa Vijana

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

الحمدُ للهِ الذي هدانا إلى صراطِهِ المستقيم، والسيرِ على هَدْيِ سيدِ المرسَلين. وَالصَّلاَةُ وَالسَّلاَمُ عَلىَ رَسُوْلِ اللهِ، وَعَلىَ آلهِ وَأَصْحَابِهِ، وَمَنْ دَعَا بِدَعْوَتِهِ، وَالْتَزَمَ بِشَرِيْعَتِهِ، وَبَذَلَ جُهْدَهُ لِإِقَامَةِ الْخِلاَفَةِ عَلىَ مِنْهَاجِهِ، وَمَنْ جاَهَدَ فِيْ سَبِيْلِ اللهِ حَقَّ جِهاَدِه. آمين

Rehma za Mwenyezi Mungu (swt) na Baraka zake zitushukie sote, na Allah awajazi kheri kwa kuhudhuria kwenu katika mkao huu.

Dada zangu, Wahudhuriaji Waheshimiwa, na Wanaharakati Vijana

Ni lazima tutambue kwamba ukombozi mkubwa umetafutwa na nchi za Kimagharibi dhidi ya watoto na vijana Waislamu nchini Indonesia. Magharibi imekuwa ikiunda mikakati ya kiulimwengu na mipango kadhaa ili kuziteka nyoyo, akili, na utiifu wa vijana Waislamu, ili wawe waaminifu kwa fikra ya usekula, maadili huru, mfumo wa Kimagharibi na nidhamu yake. La kusikitisha, mipango hii inarahisishwa na serikali na kwa sasa inaendelea. Natija yake, msimamo wa vijana Waislamu ulio fafanuliwa na Uislamu, kama waanzilishi wa mabadiliko halisi na walinzi wa Uislamu kwa sasa umetoweka, na uwezo na nishati yao zimepotea.

Mkakati wa Kimagharibi wa kuwafanya huria watoto na vijana Waislamu uko wazi katika waraka “mpango wa kivitendo wa kuzuia misimamo mikali” ulio tabanniwa na Umoja wa Mataifa na kuzinduliwa mnamo Februari iliyopita 12, 2016. Kuna vitu viwili ambavyo twapaswa kuvikashifu. Cha kwanza, kuna juhudi za kuwaweka vijana Waislamu mbali na kuufahamu Uislamu halisi. Cha pili, kuna juhudi za kunyakua uwezo na nishati ya vijana Waislamu ili kuhifadhi utawala wa mataifa ya kirasilimali ya Kimagharibi hususan Amerika – ambayo iko nyuma ya UN.

Juhudi za kuwaweka vijana Waislamu mbali na kuufahamu Uislamu halisi zinajitokeza katika mpango wa kivitendo wa kuwapa vijana uwezo ili kuzuia misimamo mikali. Katibu Mkuu wa UN anataja matunda ya tangazo la vijana jijini Amman mnamo 2015, akisema kuwa vijana wanapaswa kuwa waanzilishi katika uwekaji amani wa kiulimwengu na kuwa wachangamfu katika kuzuia misimamo mikali. Lakini kwa muda mrefu kabla ya hili, Magharibi imebuni hadithi ya kusukuma fikra kuwa wahalifu wa ghasia ni makundi ya Kiislamu. Kuanzia ulipuaji wa majengo ya World Trade Center mnamo 2011 hadi shambulizi la Paris la hivi majuzi, bomu la Ankara, bomu la Sarinah, na ulipuaji wa hivi karibuni zaidi jijini Brussels mwaka huu, wahalifu daima huhusishwa na makundi ya Kiislamu.

Na mkakati wa Kimagharibi wa kupambana na misimamo mikali hauna wasiwasi tena na vita vya kimwili, bali na vita vya kifikra na kisiasa. Kwa pendekezo la shirika la Rand Corporation, Amerika imeunda mtandao wa Waislamu poa kama washirika wake. Zaidi ya hayo, washirika hawa kipaumbele wanajumuisha wasomi Waislamu wa kihuria na wa kisekula, pamoja na wasomi na wanavyuoni vijana wenye misimamo ya kati na kati. Mtafiti mkuu katika kampuni ya Rand Co. Angel Rabasa anawafafanua Waislamu poa kuwa ni wale wanaokubali makundi ya watu wenye matakwa tofauti, utetezi wa wanawake, usawa wa kijinsia, ulinganiaji demokrasia, ubinadamu, na makundi ya kijamii.

Dada zangu, Wahudhuriaji Waheshimiwa, na Wanaharakati Vijana Rahimakumullah

Serikali ya Indonesia kwa sasa imejihusisha na ulinganizi mkubwa wa Uislamu poa ikiangazia vyuo vikuu, shule, na pesantren (shule za mabweni ambazo kitamaduni ni za Kiislamu). Hivi majuzi, Rais Jokowi alimualika sheikh mkuu wa Al-Azhar na kumuomba kueneza mfumo wa Uislamu poa. Fauka ya hayo, serikali hiyo, kupitia Wizara ya Mambo ya Kidini, itabadilisha mtaala wa elimu ya Kiislamu na kutumia jina Uislamu wa amani au Uislamu Rahmatan lil ‘Alamin. Waziri wa Mambo ya Kidini alisema waziwazi kuwa mtaala huu umeandaliwa kwa lengo kuwa wanafunzi watapewa mafunzo ya Uislamu kwa njia ambayo inaheshimu zaidi matabaka ya watu tofauti tofauti, ili kuimarisha usalama na uvumilivu, na kuimarisha demokrasia.  Kulingana na yeye, muundo huo pia utakuwa ni njia ya kuzuia kuenea kwa misimamo mikali, ambayo yaweza kuibuka katika taasisi za elimu. Wizara ya Ulinzi inapanga utoaji ushauri wa kitaifa wa ‘ulinzi wa nchi’, hususan kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, na wanafunzi wa pesantren (santri). Inalenga kupanda utaifa katika vijana ili kupambana na fikra za misimamo mikali za kimataifa zinazo ingia nchini humo.   

Uislamu poa kimsingi ni itikadi ya kukubali kila kitu kilicho kinyume na mafundisho ya Uislamu. Sio tu kukubali uhalisia wa tofauti, bali ni lazima waikubali fikra yenyewe ya tofauti. Waislamu poa ni wale ambao hawaisumbui jamii ya LGBT na kuwakubali viongozi wa kikafiri kwa jina la haki za kibinadamu; wanafurahika kuhudhuria misa kanisani, na kulegeza msimamo kwa ada za kikafiri kwa jina la makundi ya watu wenye matakwa tofauti tofauti. Hatari ya fikra ya Uislamu poa imedhihirika waziwazi. Shauku jumla imekuwa ikiibuka miongoni mwa Ummah wa Kiislamu. Ummah umegawanywa katika makundi ya Waislamu wenye misimamo mikali na Waislamu poa. Hakika, vijana Waislamu ni lazima wakuzwe ili wawe na utambulisho halisi wa Kiislamu pamoja na Aqeedah imara ya Kiislamu na akhlaqi njema, pamoja na hamu juu ya matatizo yanayo ukabili Ummah huu. Lakini juhudi hii kwa sasa inalemazwa. Vyama vya wanafunzi Waislamu katika shule, vyuo/vyuo vikuu, na pesantren vinashukiwa kuwa matundu ya magaidi. Natija yake ni, ili kizazi cha vijana kiwekwe mbali na ufahamu sahihi wa Uislamu. Na wabebaji da’wah wenye ikhlasi wanao ng’ang’ana kusimamisha hukmu za Mwenyezi Mungu (swt) wawekwe mbali na Ummah au kutuhumiwa kuwa wenye misimamo mikali. Ukweli ni, Ummah unahitaji Uislamu kisiasa ili kutatua matatizo katika nyanja kadha wa kadha yanayo sababishwa na utabikishaji nidhamu ya kihuria ya kidemokrasia na uchumi wa kirasilimali. Lakini, Magharibi inataka Waislamu kuwa na uadui na Shari’ah na watetezi wake. Magharibi inataka vijana Waislamu – kama wenye uwezo wa kuwa viongozi wa Ummah huu – kuwa Waislamu poa, kwa sababu Waislamu poa hawatatishia uwepo wao.        

Dada zangu, Wahudhuriaji Waheshimiwa, na Wanaharakati Vijana Rahimakumullah

Kadhia ya pili hatari ni kuwawezesha vijana katika nyanja za kiuchumi na kijamii, ambapo kikweli ni sehemu ya juhudi za Kimagharibi za kuuteka nyara uwezo wa vijana Waislamu. Katika waraka huo huo ‘Mpango wa Kivitendo wa Kuzuia Misimamo Mikali’, Umoja wa Mataifa umesema kuwa vichocheo vya ghasia – kando na malengo ya kidini – ni kutelekezwa kijamii na ufukara. Ili kuzuia hili, UN imeunda kitendo cha ufuatiliziaji unaolenga vijana juu ya kadhia za elimu, utoaji ujuzi, urahisishaji ajira, mawasiliano ya kistratejia, tovuti, na mitandao ya kijamii.

Katika kadhia ya elimu, mojawapo ya nukta tunazo hitaji kuzieleza ni umuhimu wa vijana kupata nafasi katika vyanzo vya elimu ya kiufundi na kulea talanta ya ujasiriamali. Muundo wa nidhamu ya elimu ya kirasilimali ni wa kivitendo na unaoendana na masoko; haulengi tena kuzalisha wanasayansi bali kuzalisha wafanyikazi. Wahitimu wa shule za kiufundi, diploma na shahada wametayarishwa kuwa wafanyikazi wa makampuni ya warasilimali wa Kimagharibi. Mwelekeo wa utafiti katika vyuo vikuu hauelekezwi tena na dola katika kujenga uchumi huru wa taifa bali unaelekezwa katika maslahi ya kampuni. Na kiukweli, tatizo la umasikini lenyewe kihakika limesababishwa na utekelezwaji wa nidhamu ya kilafi ya kiuchumi ya kirasilimali.    

Katika kadhia ya mawasiliano, tovuti na mitandao ya kijamii, kwa kisingizio kuwa huduma hizi zimetumiwa na wenye misimamo mikali kueneza mfumo wa ghasia na wameweza kusajili vijana, UN itasaidia maelfu ya wanaharakati na wasanii vijana kote ulimwenguni katika kupambana dhidi ya misimamo mikali kwa kutumia vyombo vya habari vya mtandaoni kupitia muziki, sanaa, filamu, vikaragosi, na vichekesho. Wakati huo huo twajua kuwa katika karne iliyopita ni nchi za Kimagharibi ndizo zilizo ongoza uvumbuzi katika teknolojia ya habari na mawasiliano. Wameifanya teknolojia hii chombo cha upandaji thaqafa ya kihuria. Kupitia kupigia debe muondoko wa kimuozo, wa kimada, wa kiutumizi, wa kibinafsi, na wa uhuru wa kimaisha, wamewaangamiza vijana Waislamu.   

Katika zama za leo za uchumi uliojengwa kwa msingi wa elimu, kampuni za kirasilimali zinazo tengeza ala za mawasiliano na teknolojia ya habari za kidijitali zinazo tumiwa, zilinufaika pakubwa kutokana na kutumika kwake kwa kuvuna faida kubwa, sera ya moja kwa moja. Ruwaza ya Jokowi ya Indonesia kama soko kubwa kwa uchumi wa kidijitali Kaskazini Mashariki mwa Asia, linalo lenga dolari bilioni 130 mnamo 2020, limemfanya kuwataka Mawaziri wake kudumisha mahusiano mazuri na Bonde la Silicon, kitovu cha sekta ya ubunifu nchini Amerika. Lakini, ni nani haswa anaye likalia bonde hilo, aghalabu likiitwa ‘bonde la matumaini’? si mwengine isipokuwa kampuni za kiteknolojia zinazo pigia debe muondoko wao wa kimaisha wa kihuria.

Vyombo vya habari vimewaburuza watoto Waislamu na matineja. Wakati wao mwingi hutumika kujadidisha ‘status’ zisizo kuwa na maana, ‘kuchat’ na marafiki hususan wa jinsia ya pili, kuzungumza umbea kuhusu muondoko wa kimaisha wa msanii ambaye ni kiigizo chao. Fikra ya ofa ya kuvutia katika biashara ya burudani; au njia ya haraka ya kupata utajiri kupitia kuwa muigizaji wa kike au muimbaji, imewafanya watoto na vijana Waislamu kuwa tayari kusimama katika foleni ndefu wakati wa hali ya anga ya joto na baridi kwa ajili ya usajili wa matukio kadha wa kadha ya talanta. Bila ya kutaja vipindi vya kuendelea vilivyokuza muondoko muovu wa kimaisha na msimamo huru wa wazazi na watoto, ambavyo vimewafundisha watoto kutowaheshimu wazazi wao na kuunda mitazamo kinyume na akhlaqi za Uislamu.        

Huu ndio mkakati wa kiulimwengu na ajenda ya Kimagharibi ya kuviweka mbali vizazi vya Waislamu kutokana na Uislamu halisi na kuuteka nyara uwezo wao. Wamekuwa ni mabalozi wa uhuria na wakati huo huo waathiriwa wa maadili na miondoko ya kimaisha ya Kimagharibi pamoja na nidhamu zake. Vijana wanao usoma Uislamu kwa hamu wanaelekezwa kuwa Waislamu poa kwa manufaa ya fikra, maadili, na nidhamu za Kimagharibi. Huku wengine wakielekezwa kuwa kizazi cha ‘alay’ kinacho ugua migogoro ya utambulisho, na mustakbali wao umeangamizwa kupitia fikra ya uhuru ya kutenda wapendavyo. Na hivyo wanaporomoka katika giza la ulimwengu, kujihusisha na mihadarati, uzinifu, unywaji pombe, ukahaba, na tabia nyenginezo potofu.

Kwa hakika kupitia mbinu hizi, tumepoteza hazina yetu ya thamani. Na tunaona kuwa imenyakuliwa na mabepari wanao chukia kheri ya Ummah huu. Tunapaswa kuwaokoa, kwani huu ni upotovu wa kihakika. Mtume Muhammad (saw) asema:

«مَنْ رَأَى مِنْكُمْ مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ»

“Yeyote atakaye uona uovu miongoni mwenu, basi na aubadilishe kwa mkono wake; na ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake; na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake -– na huo ni udhaifu wa imani.” [Imesimuliwa na Muslim] Hili ni jukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) juu yetu. Kuondoa munkar na kutafuta kuregesha msimamo na dori ya vijana kama inavyo takikana na Uislamu. ni lazima wawe viongozi wa mabadiliko, walinzi waaminiwa wa Uislamu. Kama pale Mtume (saw) alipokabiliwa na changamoto za da'wah kutoka kwa Maqureish, vijana ndio waliokuwa safu ya mbele ya wanajeshi walio jihami dhidi ya ukafiri. Vijana ni lazima wawe mabalozi wa Uislamu kama wanavyo onyeshwa na Mus'ab bin Umair (ra), aliyeagizwa na Mtume (saw) kuibeba da'wah hadi Yathrib na hivyo akawa balozi wa kwanza wa Kiislamu. Mus'ab aliachana na fahari yake bandia katika dunia na kuibadilisha kwa izza ya kikweli ya Akhera. Na kwa sababu ya mvutano huu, kwa muda chini ya mwaka mmoja takriban watu wote wa Yahthrib walikuwa wamesilimu, Masha Allah... Allahu Akbar.     

Ili kuregesha msimamo, uwezo, na nishati hii ya watoto na vijana Waislamu, ni lazima kuwepo na harakati inayo bebwa na chama cha kisiasa cha Kiislamu ili kunyanyua utambuzi wa vijana Waislamu. Endapo haita bebwa na chama cha kisiasa cha Kiislamu kilicho jengwa juu ya msingi wa mfumo (mabda) – fikra na njia – wa Uislamu, basi lengo la kuregesha msimamo na nishati ya vijana Waislamu kuambatana na Uislamu halita patikana. Litapatikana pekee kwa chama cha kisiasa cha Kiislamu kitakacho fichua njama ya Kimagharibi ya kuangamiza kizazi kichanga cha Uislamu, na kufichua kufeli kwa mfumo wa kisekula wa kirasilimali na demokrasia huru ambayo imesababisha mateso tu pekee katika maisha ya wanadamu.

Hakika, dori hii muhimu ya vijana itaimarishwa tu ndani ya mujtama unaotekeleza Uislamu wote (kaaffah). Ni Khilafah kwa njia ya Utume ndiyo itatayarisha kila kitu kinacho hitajika kwa ajili ya kuwawezesha vijana. Nidhamu za kielimu, kijamii, kiuchumi na kisiasa zinazo tekelezwa na Khalifah zote zitasaidia kupatikana kwa uwezo wa vijana kama walinzi waaminiwa na watetezi wa Uislamu, ambao utaleta maendeleo katika hadhara ya ulimwengu na kuhifadhi maslahi ya Ummah. Akili na nyoyo zao daima zitafungamanishwa na Uislamu na izza ya Ummah. Hivyo basi, mwelekeo wa leo wa uimarishaji fikra na uwezeshaji vijana Waislamu unalenga kusimamisha Khilafah 'ala Minhajin Nubuwwah.

Hatimaye, nawalingania vijana Waislamu kwa neno la Mwenyezi Mungu (swt) katika Surah Kahf ayah 28:

 [وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا] “Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimtii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mipaka.”

والحمد لله رب العالمينوالسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Imeandikwa na

Umm Fadhiilah - Indonesia

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:33

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu