- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mstari Mwekundu wa Unafiki: Jinsi Mauaji ya Halaiki mjini Gaza, Yanavyofichua Nyuso
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, kitovu cha kisiasa cha Uholanzi kiligeuka kuwa chekundu. Maelfu ya watu walijiunga na maandamano jijini The Hague, ambapo mstari mwekundu wa ishara ulichorwa - mstari unaoashiria mpaka wa maadili wa kile ambacho bado kingali kinaweza kutetewa. Kichocheo hakikuwa tu ushiriki wa ‘Israel’ katika Shindano la Nyimbo la Eurovision, bali zaidi ya yote ni kuongezeka kwa hasira juu ya baa la njaa mjini Gaza na kutochukua hatua kwa aibu kwa serikali za Magharibi.
Eurovision: Muziki kama Hadaa
Kwamba Israel iliruhusiwa kushiriki katika Eurovision katikati ya uzito kamili wa mauaji ya halaiki – wakati kiuhalisi Gaza ina njaa na kuuawa – inadhihirisha unafiki wa nchi za kisekula za Magharibi. Taasisi zile zile zilizoisitisha Urusi baada ya kuivamia Ukraine sasa zinatetea ushiriki wa nchi ambayo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa huenda inatenda uhalifu wa kivita. Kwa hivyo ni upi ujumbe? Kwamba maadili ya Ulaya yanatumika tu yanapofaa kisiasa?
Hasira hii ya kuibaguzi sio uangalizi; ni mtindo. Matamshi matupu ya haki za binadamu daima yamekuwa yakitumika na yanatumika kama chombo cha siasa za kieneo, sio kama dira ya maadili.
Gaza: Ambapo Kimya Kinakuwa ni Ushiriki
Hali katika Gaza ni mbaya sana. Huku viongozi wa dunia wakijadili "kupungua uhasama" na "ukanda wa kibinadamu," watoto wanakufa kwa njaa. Sheria za kimataifa, mikataba ya haki za binadamu, Mikataba ya Geneva – zinakuwa sio zaidi ya ahadi za karatasi, wala haishangazi. Na kwa mara nyengine tena, inakuwa dhahiri: Maisha ya Wapalestina yamewekwa katika mizani tofauti.
Baa la jaa mjini Gaza sio janga la kimaumbile. Ni janga lililotengezwa na mwanadamu, lililoundwa kisiasa, lililowezeshwa na kimya na utovu wa nidhamu wa mataifa ya Magharibi. Uholanzi, Ujerumani, Ufaransa – zote zinatetea "haki ya kujilinda" ya "Israel" huku ikifumbia macho kuzingirwa kwa mamilioni ya watu. Na kinachoudhi zaidi ni kimya cha wanaojiita viongozi wetu Waislamu.
The Hague: Mstari Mwekundu Umefikiwa
Mstari mwekundu uliochorwa jijini The Hague ulikuwa zaidi ya ishara. Ulikuwa ni taarifa ya pamoja: umbali huu, na sio zaidi ya huu. Kwa wengi, maandamano hayo pia yalionyesha kuongezeka kujitenga na mfumo wa kisiasa wa Magharibi - mfumo ambao unajionyesha kama mlinzi wa uhuru na usawa, lakini kivitendo hutumika kama mlinzi wa unafiki na ukandamizaji wa kimuundo.
Katikati ya mtafaruku huu wa kimaadili, swali moja linakuwa kubwa zaidi: je, kuna njia badali? Na tunaweza kujibu swali hili kwa sauti kubwa na kwa fahari kwa "NDIYO"! Uislamu unatoa muundo wa kimaadili na thabiti ambapo haki za wanawake, watoto, maskini, na wanaodhulumiwa si kauli mbiu, bali ni wajibu wa kijamii.
Uislamu unafundisha kwamba thamani ya uhai wa mwanadamu ni takatifu – bila kujali kabila au utaifa. Haki si maadili ya kindoto, bali ni wajibu madhubuti. Badala ya ujanja wa kisiasa au uanaharakati wa kiishara, Uislamu unatoa ruwaza pana ambapo haki ya kijamii, uongozi unaowajibika, na ulinzi wa walio hatarini ni masuala nyeti.
Hitimisho
Matukio yanayoizunguka Gaza, Eurovision, na maandamano jijini The Hague yanafichua ukweli mmoja wa kimsingi: mfumo wa kisekula unashindwa kushikamana na maadili yake uliyoyatangaza. Unafiki wa mataifa ya Magharibi sio dosari katika mfumo huu – balo ndio mfumo wenyewe. Na watu zaidi na zaidi wanaanza kuuona.
Na hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote, tunahitaji kuzungumza kwa ajili ya haki, kwa ajili ya kuregea kwa Dola ya Khilafah. Uislamu kama suluhisho sio kauli mbiu ya watu wenye msimamo mkali – ni sauti ya wale wanaotafuta haki ya kweli na ya kudumu.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sumaya Bint Khayyat