Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Amerika:

Kongamano la Khilafah 2023 "Migogoro na Njia Panda... Udharura wa Uislamu Kuuokoa Ulimwengu"

Hizb ut Tahrir/Amerika itaandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa mwaka huu wa 2023 chini ya kichwa:

"Migogoro na Njia panda... Udharura wa Uislamu Kuuokoa Ulimwengu"

Jumamosi, 23 Shawwal 1444 H, sawia na 13 Mei 2023 M

Toleo kutoka Hizb ut Tahrir / Amerika

Kongamano la Khilafah 2023

Jumatano, 27 Shawwal 2023 H - 17 Mei 2023 M

Bonyeza Hapa

Uislamu dhidi ya Ajenda ya LGBT

na Ndugu Zaki Tahir

Hotuba hii ya kuvutia ya Ndugu Zaki Tahir, inayotoa ufahamu wa kina wa changamoto ambazo jamii ya Kiislamu inakabiliana nazo kutokana na shinikizo linaloongezeka kutoka kwa LGBT na ajenda ya ufeministi. Hotuba yake ilitoa mikakati ya kivitendo kusaidia familia za Kiislamu kuwalinda watoto wao, na kuwapa uwezo wa kupinga fahisha inayojaribu kuiangamiza familia ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran: (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ)  “Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. [At-Tahrim:6]. Alieleza jinsi kushikamana na Qur’an Tukufu na Sunnah kutaipa uwezo jamii wa kusimamisha Dini yao dhidi ya ufisadi huu.

Mgogoro wa Kiuchumi: Mtazamo wa Kiislamu na Hatua za Kivitendo

na Ustadh Samer Abu Omar

Samer Abu Omar alizungumzia mgogoro wa kiuchumi unaoikumba Marekani na dunia hivi sasa. Akizungumzia kuongezeka kwa mwanya wa utajiri, kupanda kwa mfumko wa bei, na changamoto kwa msukosuko wa kiuchumi wa Marekani, aliangazia jinsi Uislamu unavyotoa masuluhisho yanayoweza kuhimili majanga mengi ya kiuchumi ambayo mara kwa mara yanausibu ubepari.

Wanawake wa Kiislamu Simameni dhidi ya Ajenda ya Ufeministi

na Dada Safia Rasheed

Hotuba ya Dada Safia Rasheed, “Wanawake wa Kiislamu Simameni dhidi ya Ajenda ya Ufeministi,” iliangazia nguvu na utu wa wanawake wa Kiislamu uliojengwa juu ya msingi wa Uislamu. Aliwashajiisha kusimama kidete dhidi ya nguvu yoyote inayohujumu heshima ya wanawake wa Kiislamu. Alifichua jinsi ubepari unavyomnyonya mwanamke ili kunufaisha maslahi yao ya kifedha dhidi ya maslahi ya ustawi wa familia.

Himaya Inayoporomoka: Mgogoro wa Kisiasa wa Amerika

na Ndugu Diwan Abu Ibrahim

"Himaya Inayoporomoka: Mgogoro wa Kisiasa wa Amerika," Ndugu Diwan Abu Ibrahim aliangazia jinsi Amerika inavyopambana na mgawanyiko wa kisiasa uliokithiri. Alizungumzia jinsi makosa ya sera ya kigeni ya Amerika yameongeza mzigo wa kifedha kwa deni la kitaifa na kuwezesha kuongezeka kwa ulimwengu wa nchi nyingi. Hotuba hii inaangazia jinsi Amerika inavyosimama katika njia panda muhimu, na kukabiliwa na kuanguka kwa utawala na kuhama kuelekea katika ulimwengu wa pande nyingi.

Hotuba ya Kuhitimisha Kongamano la HT

na Haitham Ibn Thbait

Kongamano hilo lilihitimishwa kwa hotuba ya kufunga ya Haitham Ibn Thbait, ambaye alisisitiza haja ya jamii ya Kiislamu kujitia nguvu kwa imani yao kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika nyakati hizi zenye changamoto. Kongamano hili litasaidia kuiwezesha jamii ya Kiislamu elimu ya jinsi ya kukabiliana na majanga ya leo.

- Video Fupi ya Ualishi wa Kongamano -

Video 1

- Video Fupi ya Ualishi wa Kongamano -

Video 2

- Alama Ishara za Kongamano -

#أقيموا_الخلافة

ReturnTheKhilafah#

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Amerika:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Amerika

Ukurasa wa Instagram wa Hizb ut Tahrir / Amerika

Akaunti ya Twitter ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu