Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Hizb ut Tahrir / Amerika:

Kongamano la Khilafah 1443 H – 2022 M

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo 28 Rajab Tukufu 1342 H, Hizb ut Tahrir / Amerika iliandaa kongamano kubwa kwa anwani:

"Mpango wa Mustakbali"

Waliohadhiri katika kongamano hili ni ndugu:

Ustadh Ali Merchant

Dkt. Ayman Hamed

Ustadh Haitham ibn Thabit

Dkt. Abdul Raafi

Jumapili, 02 Shaaban 1443 H - 06 Machi 2022 M

Mnamo tarehe 6 Machi 2022, Hizb ut Tahrir/Amerika ilifanikiwa kufanya Kongamano lake la kila mwaka la Khilafah, kama sehemu ya kampeni ya kimataifa iliyoandaliwa kuhusu kuondolewa kwa Khilafah (Ukhalifa) mwaka 1924. Ni ulinganizi wa kimataifa kwa Waislamu kote duniani kusimama na kutimiza Wajibu wa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt), kupitia kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Mtume (saw).

Dori ya Uislamu katika mfumo wa kiliberali wa kisekula wa kiulimwengu imekuwa jambo la mjadala katika karne nzima iliyopita. Baada ya Mapinduzi ya Kiarabu, nchi za Magharibi na vibaraka wake katika ulimwengu wa Kiislamu zimetumia hatua mbalimbali za makabiliano ili kuzuia kukua kwa Uislamu na dori yake katika siasa. Haswa, suala la kusimamisha tena Khilafah limelengwa.

Hakuna haja ya mtu kuhesabu kufeli kwa Urasilimali na fikra zake za kiliberali ya kisekula. Sote tunaweza kuona na kuhisi matokeo yake sio tu katika ulimwengu wa Kiislamu, bali kote barani Asia, Afrika na Amerika Kusini. Hata katika nchi za Magharibi, kengele za tahadhari zinalia ili kulinda kanuni za mfumo wa kiliberali wa kiulimwengu na kudumisha maadili yao. Mengi ya kuchukiza Magharibi na vibaraka wake, mawazo ya Khilafah, Uislamu wa kisiasa, kutoridhika na uliberali wa kisekula na Urasilimali yamekita mizizi katika akili za Waislamu. Mwamko wa Ummah uko juu yetu.

Hivyo basi, kongamano la mwaka huu lenye kichwa ‘Mpango wa Mustakbali’ lilitumia matarajio, matamanio, na haja ya Khilafah inayochemka ndani ya Ummah hadi kwenye Mpango sahihi na wa vitendo ambao unaweza kujengwa juu yake. Kongamano hili lilianza kwa kusoma aya za Quran Al-Majeed na kufuatiwa na tafsiri yake na ujumbe wa ufunguzi. Hii ikifuatiwa na hotuba nne zenye mada: ‘Utawala wa Dola ya Khilafah’, ‘Kujenga Nguvu za Kiuchumi za Dola Kuu’, ‘Kusuluhisha Tofauti na Kujenga Jamii ya Kiislamu’, na ‘Kuhusu Hizb-ut-Tahrir – Kazi na Ruwaza Yetu’. Hafla hii ilihitimishwa kwa jopo la wazungumzaji kujibu maswali kutoka kwa wahudhuriaji.

Katika hotuba ya kwanza, 'Utawala wa Dola ya Khilafah', Ali Merchant alielezea muundo wa kina, mahitaji, idara, na taasisi zinazounda muundo wa Dola ya Khilafah akitoa moja kwa moja kutoka kwa kazi za uangalifu za Hizb ut Tahrir kuhusu suala hilo. Kuanzia kwenye taasisi ya Khalifah, Jeshi, Idara ya Viwanda, hadi Majlis-al-Ummah, na yote hayo yalibainishwa kama mwongozo wa kivitendo na unaotekelezeka kwa Ummah.

Katika hotuba ya pili, 'Kujenga Nguvu ya Kiuchumi ya Dola Kuu', Dkt. Ayman Hamed alieleza kwa ufasaha zaidi Mfumo wa Kiuchumi katika Uislamu na haswa juu ya kile ambacho haswa kinaufanya kuwa wa Kiislamu, wa kipekee tofauti na mifumo mingine yote, wa kivitendo katika uhalisia, na wenye mafanikio makubwa katika kutatua tatizo la kiuchumi la wanadamu.

Katika hotuba ya tatu, 'Kusuluhisha Tofauti na Kujenga Jamii ya Kiislamu', Haitham ibn Thbait kwa shauku aliwasilisha historia tukufu ya Uislamu na kanuni za Kiislamu zenye kuhakikisha mshikamano wa kijamii tangu kuanzishwa kwake chini ya Uongozi wa Mtume wetu (saw) katika Dola ya kwanza ya Kiislamu kwa historia kubwa ya Uislamu. Wananchi (Waislamu na wasiokuwa Waislamu), kama inavyoshuhudiwa na historia na kulindwa na Katiba ya Dola kufurahia usalama/ulinzi, heshima na fursa na pia ni ruwaza ya hizb.

Katika hotuba ya nne na ya mwisho ya kongamano hilo, 'Kuhusu Hizb ut-Tahrir-Kazi na Ruwaza Yetu', Dkt. Abdur-Rafay aliweka wazi kisa, mafanikio, na kujitolea kunakojulikana kwa Hizb ut-Tahrir, waja wenye bidii wa Ummah na chama cha kisiasa cha kimataifa ambacho mfumo wake ni Uislamu na lengo lake pekee ni kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah. Hotuba hiyo ilihusisha historia, usomi, muhanga, ukakamavu wa kisiasa usio na kifani, kanuni na ruwaza ya hizb.

Hizb ut Tahrir ni chama cha siasa kisicho na vurugu kilichojifunga katika kazi ya kifikra na kisiasa pekee ili kufikisha ulinganizi wa Kiislamu wa kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume katika nchi za Kiislamu. Hii ni kutokana na kushikama vikali kwa hizb na manhaj ya kisiasa ya Mtume Muhammad (saw) ambaye alifanya kazi ya kifikra na kisiasa pekee ili kufikisha Ulinganizi wa Kiislamu na kusimamisha Dola ya Kiislamu. Hizb haitumii aina yoyote ya shughuli za vurugu na huu ni ukweli unaojulikana.

- Alama Ishara za Kampeni

#أقيموا_الخلافة

#الخلافة_101

ReturnTheKhilafah#

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

#TurudisheniKhilafah

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Amerika:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Amerika

Ukurasa wa Instagram wa Hizb ut Tahrir / Amerika

Akaunti ya Twitter ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu