Jumatano, 22 Safar 1448 | 2026/08/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh:

Kongamano la Kisiasa “Kongamano la Bajeti ya Kitaifa - Muongozo wa Bajeti ya Kiislamu Inayojitosheleza kwa Dhati”

Hizb ut Tahrir / Bangladesh yaandaa kongamano la kisiasa lenye kichwa:

 “Kongamano la Bajeti ya Kitaifa - Mwongozo wa Bajeti ya Kiislamu Inayojitosheleza kwa Dhati”

Licha ya kuingia madarakani kwa gharama ya damu ya wanafunzi na raia, serikali ya mpito haijachukua hatua zozote madhubuti za kujenga upya uchumi dhaifu ulioachwa na utawala uliopita wa Hasina. Kinyume chake, ilisaini makubaliano ya biashara ya pande zote na Marekani dakika za mwisho, ikihatarisha uhuru wa kiuchumi wa nchi hii.

Serikali ya PPP imeidhinisha bajeti ya Taka trilioni 9.38, ikiahidi kufufua uchumi, udhibiti wa mfumko wa bei, uundaji wa ajira, na ustawi wa umma. Hata hivyo, ukweli ni kwamba bajeti hii, ikilinganishwa na bajeti zilizopita, haionyeshi mabadiliko yoyote halisi ya kimuundo, isipokuwa tofauti za nambari. Hasa, mtego wa madeni ya kibeberu na muundo wa mapato unaotegemea kodi ya kinyonyaji na VAT bado haujabadilika kimsingi.

Katika muktadha huu, kongamano hili litatoa maono ya bajeti ya Kiislamu inayolenga kufikia uchumi unaojitosheleza na kuhudumia maslahi ya watu. Mwenyezi Mungu Mtukufu (swt) asema:

﴿كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنْكُمْ﴾

ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Surat Al-Hashr: 7]

Hotuba ya 1:

Kufichua umbile la Bajeti ya Kitaifa (2026–2027) iliyonaswa katika mzunguko wa deni la kibeberu na mfumo wa kiuchumi wa kibepari unaonyonya

Hotuba ya 2:

Taswira ya Bajeti ya Kiislamu ili kufikia uchumi unaojitosheleza na kutumikia maslahi ya umma

Basi kuweni pamoja nasi…

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Bangladesh

Ijumaa, 10 Safar 1447 H – 24 Julai 2026 M

 - Wakati na Mahali -

Anwani: Kongamano la Bajeti ya Kitaifa - Muongozo wa Bajeti ya Kiislamu Inayojitosheleza kwa Dhati

Siku na Tarehe: Ijumaa, 10 Safar 1448 H – 24 Julai 2026 M

Wakati: 04:30 PM (Majira ya Madina) 07:30 PM (Majira ya Bangladesh)

Muda: Saa Moja na Nusu

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano -

https://www.alwaqiyah.tv/index.php/video/12046/national-budget-conference-blueprint-for-a-self-reliant-islamic-budget/

- Matangazo ya Moja kwa Moja kutoka kwa Tovuti ya Odysee -

//odysee.com/@AlWaqiyahTV:5/BConf24072026">https://odysee.com/@AlWaqiyahTV:5/BConf24072026

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangaldesh:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangaldesh

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu