Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Malaysia Imekabidhi Andiko linaloisihi serikali ifungue tena Misikiti

Ni takriban majuma 12 sasa misikiti kote nchini imefungwa kwa ajili ya swala za Ijumaa tangu kushadidiwa kwa Amri ya Kudhibiti wa Matembezi (MCO) iliyo tolewa na Serikali. Licha ya matakwa imara kufanywa hususan na Hizb ut Tahrir / Malaysia (HTM) pamoja na sauti za kufadhaika na kutoridhika kutoka kwa Ummah ili serikali ifungue tena Misikiti pamoja na kuchukuliwa tahadhari stahiki za kiusalama, serikali hii ya kisekula bado inaendelea kupuuzia maombi haya.

Ijumaa iliyopita misikiti mingi ilifunguliwa kwa swala za Ijumaa ikiwa ni mara ya kwanza baada ya MCO hiyo, la kusikitisha ikadhibiti idadi maalum tu ya watu, ikijumuisha Imamu na kamati ya msikiti pekee. HTM inashutumu vikali yale yaliyo pitishwa na Mamlaka ya kidini juu ya suala hili, kana kwamba swala ya Ijumaa ni haki yao peke yao! Aibu iliyoje!

Kwa msingi huu, HTM imekabidhi andiko kwa Idara ya Dini ya Kiislamu kwa majimbo yote, ikiyasihi wafungue tena misikiti maramoja ili kuwawezesha Waislam wote kuswali swala za Ijumaa. Katika andiko hilo, mbali naa kuambatanisha na kuelezea hatua za kiusalama ambazo zinapasa kuchukuliwa katika kufunguliwa tena kwa misikiti, HTM imesisitiza kwamba kufungwa kwa misikiti kuliko fanywa na serikali, na kuzuia watu kutokana na swala za Ijumaa au swala za Jamaa, ni haram kabisa katika Uislamu na serikali inabeba dhambi kubwa kwa kufanya hivi.

Takriban Idara za Dini ya Kiislamu katika majimbo yote zilipokea andiko hilo kwa njia vizuri, lakini HTM ilisisitiza kwamba hivi ni vizuri ila haitoshi maadamu Nyumba za Mwenyezi Mungu (swt) hazifunguliwi kama ipasavyo.

05/06/2020

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu