Ijumaa, 16 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Al-Waqiyah TV: Naveed Butt, Mbebaji Ulinganizi wa Khilafah, Nembo ya Upinzani dhidi ya Uvamizi wa Kiamerika Aliye Zuiliwa katika Korokoro za Siri za Ukandamizaji za Vyombo vya Usalama!

 Mnamo tarehe 11 Mei 2020 M, ilisadifu kuwa ni kumbukumbu ya nane ya kutekwa nyara Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, ukamataji wake ulitimia katika korokoro za siri za ukandamizaji za vyombo vya usalama. Pamoja na hilo, serikali ya Bajwa/Imran ilimwachilia huru rubani wa Kihindi (Abhinandan) ambaye alikiuka mpaka wa udhibiti huku akijaribu kuishambulia Pakistan, baada ya kupita siku moja pekee. Kama ilivyo fanya maandalizi serikali hii ya mkutano maalum wa kidiplomasia baina ya jasusi gaidi wa Kihindi (Kulbhushan Jadhav), pamoja na mkewe. Pamoja na hilo, serikali hii ingali inamnyima Naveed Butt mawasiliano ya aina yoyote na familia yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

﴾ مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ﴿

"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." [Al-Fath:29].

Basi ni jinsi gani hii ndio hali ya watawala vibaraka wa Amerika?! Hakika wao ni wapole mno kwa makafiri maadui na wanabadilishana hisia za mapenzi na huruma na upole, huku wakiamiliana pamoja na Waislamu kwa mkono wa chuma, hata pia wakiwatumilia lugha ya moto na mabomu, hii ni licha ya maneno Yake (swt) katika Hadith al-Qudsi ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِياً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»  

"Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Yeyote anaye onyesha uadui kwa kipenzi (wali) changu, basi nimetangaza vita dhidi yake" (Bukhari)

Jumatatu 18 Ramadhan Iliyo Barikiwa 1441 H sawia na 11 Mei 2020 M

Kwa mengi zaidi Bonyeza Hapa

#FreeNaveedButt

#MwacheniHuruNaveedButt

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 14 Mei 2020 16:33

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu