Ijumaa, 15 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Amali kutoka Kitengo cha Wanawake Zikikumbuka Kumbukumbu ya Miaka 101 ya Kuvunjwa Khilafah

Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Ardhi Tukufu ya Palestina kilifanya amali anuwai, za ana kwa ana na mtandaoni, kukumbuka kumbukumbu ya miaka 101 ya kuvunjwa Khilafah zenye kichwa, "Ni Wakati sasa wa Kudhihiri Dini yetu na Kunyanyuliwa Bendera ya Mtume wetu".

Amali za ana kwa ana zilijumuisha shughuli nyingi tofauti tofauti; kuanzia kwa semina, mikusanyiko ya jioni, vikao vya majadiliano na mazungumzo ya msikitini, ambapo video za maelezo zilionyeshwa, katika miji mingi na vijiji vya Ardhi Iliyobarikiwa: kuanzia Hebron na vijiji vyake, na Bethlehemu na miji yake ya kusini, hadi kaskazini mwa Jenin; Bidya na Qalqilya, zikipitia Ramallah na Jerusalem.

Ama amali za mtandaoni, zilitofautiana kati ya kuandika makala na mazungumzo kwenye tovuti mbalimbali na mitandao ya kijamii. Video zilitolewa ambazo zilijumuisha mazungumzo, maombi na midahalo, ambazo baadhi yake zilichapishwa katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na Kitengo chake cha Wanawake, pamoja na ukurasa wa tawi la Kitengo cha Wanawake. Vilevile, jumbe za kuunga mkono zilitumwa kwa kampeni ya Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari, "Khilafah: Yenye Kuhakikisha Hadhi, Usalama na Haki za Kisheria za Wanawake."

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aharakishe nusra yake, ufueni na ahadi yake, na kwamba hautakuja mwaka ujao, isipokuwa dola itakuwa imesimamishwa, na tuwe miongoni mwa mashahidi na wanajeshi wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

#أقيموا_الخلافة

#الخلافة_101

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#TurudisheniKhilafah

#خلافت_كو_قائم_كرو

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu