Jumanne, 14 Shawwal 1445 | 2024/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ripoti ya Habari 30/03/2023

Katika muendelezo wa amali za hadhara zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, kuhamasisha Umma wa Kiislamu na kunoa azma yake ya kusimamisha tena Dola ya Khilafah Rashida, kwa kuunda rai jumla yenye kufahamu hukmu za Uislamu na masuluhisho yake. Hizb ilifanya amali nyingi za hadhara katika maeneo mbalimbali ya nchi, zinazogusia mihadarati na hatari yake kwa jamii, na matatizo ya kiuchumi, na uadui wa Mayahudi kwa waumini, na mwezi wa Ramadhan ni moja ya madhihirisho ya Umoja wa Waislamu, na mada nyinginezo.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika vyuo vikuu watenga kona ya mazungumzo na majadiliano yenye kichwa: "Kuongezeka kwa ushuru, katika utekelezaji wa maagizo ya Benki ya Dunia, kwasababisha bei za juu na Khilafah ndio suluhisho", mnamo Machi 01, 2023 katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Mafunzo ya Kiuchumi na Kijamii, ambapo Ustadh Yasser Ahmed alizungumza, ambaye alianza mazungumzo yake kuhusu marekebisho Katika ushuru wa forodha ulioathiri bidhaa 103, ongezeko hilo ni kati ya 10% - 40%, na kwamba ongezeko hili linatokana na utekelezaji wa maagizo ya Benki ya Dunia ya kulipa mikopo yenye riba ambayo ndio sababu ya bei za juu, na kwamba serikali hii haizingatii maslahi ya watu wa nchi ambao ni wanyonge.

Mnamo Machi 4, 2023, semina ilifanywa katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Al-Qabas katika jiji la Port Sudan, yenye kichwa: "Mihadarati na Vita vya Kizazi cha Tano." Wanafunzi na walimu waliingiliana nayo kwa njia bora. Ustadh Shariq Youssef alizungumza kuhusu aina za mihadarati na hatari yake kwa mtu binafsi na jamii. Alitahadharisha juu ya haja ya jamii kukabiliana na vita hivi vilivyoanzishwa na Magharibi kafiri kupitia vibaraka wake, kwa kuamrisha mema na kukataza maovu, na kuwahimiza watawala na kuwawajibisha kutekeleza dori yao katika kuyalinda makundi yote ya jamii kutokana na hatari hiyo.

Katika kipengele chengine, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mtaa wa Madani walitoa hotuba ya kisiasa yenye kichwa: "Wajibu wa dola kutoa kazi na kutoa ujira wa kutosha", katika soko kubwa mbele ya Dula la Dawa la Al-Khair mnamo Machi 5, 2023. Spika alionyesha kwamba serikali na tawala za sasa za kidhalimu zinafanya kazi ya kuwaondoa wafanyikazi, kwa kisingizio cha ubinafsishaji, au kuwapa ujira ambao haulingani na manufaa ya kazi wanayofanya, bali hata hautoshi kukidhi mahitaji ya kimsingi kwa muda wa wiki moja, na kuwaacha watu wakiteseka na dhiki, mahitaji na matakwa, kwa kumalizia mzungumzaji huyo alisema kuwa dola ya Khilafah, Mwenyezi Mungu akipenda, itatoa kazi na kutoa ujira unaotosheleza, na itakuwa makini kuhakikisha mahitaji ya kimsingi ya raia wake ambao hawawezi kuyakidhi, na watu wanaishi maisha ya staha chini ya ulinzi wake.

Katika muktadha wa dawa za kulevya, hatari zake, na kampeni iliyozinduliwa na hizb ili kupambana nazo, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Nile Mashariki walitoa hotuba kubwa ya kisiasa mnamo Machi 8, 2023, katika kituo cha Qalabat, ambapo Bwana Hammad Al-Dhai alizungumzia hatari ya dawa za kulevya, aina zake, na jinsi zilivyoingia nchini, kisha akazungumzia kuwa lengo kuu la dawa hizo ni kuziangamiza akili za vijana katika Umma wa Mtume (saw).

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika eneo la Sharq al-Nil walifanya mhadhara katika Msikiti wa Upanuzi wa Square 6 Machi 8, ambapo Ustadh Ahmed Al-Khatib alizungumzia fahamu ya utumwa, na akaeleza kwamba utumwa maana yake ni kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kuzingatia amri zake zote na kuepuka makatazo yake yote, na kutoa mifano ya uhalisia wa maisha ya watu.

Mnamo tarehe 8 Machi 2023, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan walifanya mhadhara katika mji wa Al-Obeid wenye kichwa: "Uadui wa Mayahudi dhidi ya Waumini", katika Msikiti Mkuu, baada ya swala ya adhuhuri. Iliwasilishwa na Bw. Abdul Qadir Abdul Rahman, mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan.

"Migogoro ya Sudan inayozidi kuwa mibaya, je, ina suluhu?" chini ya anwani hii, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Eneo la Omdurman Magharibi, mnamo Machi 8, 2023, walitoa hotuba ya kisiasa katika soko la Al-Qash, magharibi mwa soko la Libya, ambapo Ustadh Ishaq Muhammad alizungumza, alipoanza hotuba yake kwa mukhtasari wa serikali mtawalia ambazo zimetawala Sudan tangu uhuru, kijeshi na kiraia, na vipindi vya mpito. Na alionyesha kuwa serikali zote hizo zilifeli kulifufua taifa na kwenda kuondoka bila ya kutubu, kutokana na watu kutoridhika nazo.

"Haja ya Watu kwa Huduma ya Afya katika Uislamu", chini ya kichwa hiki, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mji wa Al-Obeid walifanya jukwaa lao la kawaida mnamo Jumamosi Machi 11, 2023 katika afisi ya Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Obeid. Ustadh Hussein Al-Hadi alizungumza katika jukwaa hilo akionyesha kudorora kwa hali halisi ya uchungaji imefikia Afya kwa upande wa watumishi wa afya, mazingira ya afya, huduma za afya na matibabu, akielezea huduma mbovu za afya kutokana na kufeli kwa mfumo wa kibepari uliojengwa juu ya msingi wa manufaa na ukosefu wa ubinadamu.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika eneo la Khartoum walifanya kongamano la kisiasa katika uwanja wa Jumuiya ya Matarajio ya Vijana mnamo Machi 17, 2023, lenye kichwa: "Hatari ya Mihadarati kwa Vijana wa Umma", ambapo Dkt. Muhammad Abdel Rahman alizungumza, ambaye alianza mazungumzo yake kuhusu dawa za steroid ambazo baadhi ya wachezaji hunywa katika shughuli mbalimbali za michezo, kwani ni mlango wa kuingia kwa madawa ya kulevya na sehemu yake, na upigiaji mnada wa vichocheo hivi kwa vijana kwani huwapa nishati na nguvu. Kisha akazungumza juu ya uraibu wa dawa za kulevya na kuenea kwake nchini kwa njia tofauti, na idadi kubwa ya watumiaji wa dawa za kulevya na mkusanyiko wao kati ya umri wa miaka 14-24, na kesi za kila siku zinazofikia vituo vya matibabu ya ulevi katika mji mkuu, Khartoum, zimefikia kesi 1,350, jambo ambalo linaashiria kuenea kwa mihadarati miongoni mwa vijana. Na alionyesha jinsi ya kukabiliana na hatari hii, ambayo inaanzia na mtu binafsi mwenyewe na kujitolea kwake kwa hukmu za Sharia, na dori ya familia katika kuwafuatilia watoto wake na kujua ni nani wanaosuhubiana nao, na dori muhimu zaidi liko kwa dola iliyofungua vivuko na sehemu mbalimbali za kuingilia dawa hizo.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mji wa Al-Obeid walifanya mhadhara katika Msikiti Mkuu Machi 25, 2023, baada ya swala ya Adhuhuri, uliowasilishwa na Ustadh Al-Nazir Muhammad Hussain, kwa anwani: “Kufunga Ramadhan ni Dhihirisho la Umoja wa Waislamu,” akionyesha kuwa Umma wa Kiislamu ni Ummah mmoja ambao funga yake lazima iwe moja na isiwe ni somo katika mipaka ya kitaifa katika kuthibitisha ruwaza, na kupitia hotuba yake risala tatu zilitumwa. Ya kwanza ni kwa wanavyuoni na mahakimu: Ni lazima waliangalie suala hilo kwa mtazamo wa Uislamu, na uthibitisho wa mtazamo wowote kutoka kwa baraza lolote unawakilisha hoja ya wao kutoa hukmu juu ya uthibitisho wa mtazamo au ukamilisho. Risala ya pili ni kwa Waislamu wote: kwamba watimize wajibu wa kushikamana na hukmu ya Shari’a na kuwawajibisha wale wanaohusika na ukiukaji wao wa hukmu. Na ya tatu ni kwa watawala: Katika mwezi huu, lazima wamche Mwenyezi Mungu, watubie Kwake, wautekeleze Uislamu, na wajikomboe kutoka katika utumwa.

Pia katika mji wa Al-Abyad, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan walifanya mhadhara katika Msikiti wa Soko la Karima Kaskazini mnamo Machi 26, 2023, ambapo Ustadh Ahmed Wada’ alizungumza kuhusu uchamungu, na kusema kwamba hekima ya kufunga ni uchamungu, na Muislamu lazima amche Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika mji wa Al-Abyad walifanya muhadhara wenye kichwa: "Ramadhan ni mwezi wa ufunguzi na ushindi" uliowasilishwa na Hussain Al-Hadi Muhammad, mnamo Machi 29, 2023, baada ya swala ya adhuhuri katika Msikiti wa Soko la Karima la Kaskazini, akitaja mifano ya ufunguzi wa Kiislamu ambao Waislamu waliufanya katika mwezi wa Ramadhan na jinsi maisha yalivyokuwa kwa Waislamu kutoka kwenye izza na kupandishwa daraja, na pindi ufunguzi huo ulipokosekana, vipi maisha ya watu yalibadilika na kuwa udhalilifu na udhalilifu, na kuhalalisha hili kwa kukosekana Dola ya Kiislamu, akionyesha wajibu wa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili tuweze kuregesha ufunguzi huo na kufurahia maisha ya staha duniani na Akhera, kama apendavyo Mola wa walimwengu wote kwa Umma wa mbora wa Mitume.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu