Jumanne, 28 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyombo vya Usalama katika Mji wa Al-Qadarif Vyawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir vikiliunga mkono umbile la Kiyahudi!
(Imetafsiriwa)

Katika hotuba ya hadhara iliyotolewa na Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Qadarif, kwenye soko la Al-Qadarif karibu na hospitali ya meno, mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 23 Dhul-Hijjah 1446 H, inayolingana na 19/6/2025 M, Ustadh Awad Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza kuhusu uhalisia wa vita na umbile la Kiyahudi, furaha ya Waislamu kwa mashambulizi dhidi ya umbile hili, na kiu ya watu ya ushindi dhidi ya mkaaji huyu wa kimabavu wa ardhi tukufu—Masrah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alithibitisha faradhi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaikomboa Palestina na ardhi nyenginezo za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Hadhira iliitikia vyema hotuba hiyo, na kulikuwa na michangio tofauti tofauti kutoka kwa waliohudhuria.

Mara baada ya hotuba kumalizika, na kabla ya mkusanyiko kutawanyika, magari matatu ya vyombo vya usalama yalifika na kuwakamata watatu katika Mashababu wa Hizb ut Tahrir—ndugu: Al-Mahi Abdeen, Maysarah Yahya, na Muhammad Yahya—pamoja na mtu wa nne kutoka kwa wahudhuriaji. Waliwapiga na kuwafunga macho, kisha wakawapeleka kusikojulikana, na kukamata kipaza sauti kilichotumika katika hotuba hiyo. Hili lilitokea huku kukiwa na mshangao wa hadhira kwa tabia hii ya kushangaza. Wafungwa hao hawajaachiliwa hadi kufikia kuandikwa kwa taarifa hii!!

Kwa kujibu kitendo hiki cha kinyama, sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Tunaiwajibisha serikali kwa ajili ya usalama wa ndugu waliokamatwa, na tunawaonya wao na wapambe wao juu ya matokeo ya vitendo hivyo, ambavyo haviakisi Uislamu wala Waislamu, na badala yake vinatumikia maslahi ya Mayahudi—ndugu wa nyani na nguruwe—na washirika wao wakoloni makafiri, pamoja na watawala wa tawala za uharibifu katika nchi za Waislamu, ambao wanazingatia kila kilio dhidi yao, Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Je, wanadanganyika vipi?

Pili: Tabia hii ya ajabu na ya kutia shaka—ya wale ambao walipaswa kuwaunga mkono ndugu zao huko Palestina—inathibitisha kwamba tawala hizi, ukiwemo utawala wa Sudan, ni maadui wa Ummah, na dhamira yao ni kulinda umbile katili la Kiyahudi na kutekeleza njama za makafiri wakoloni katika nchi zetu. Vita vya kipumbavu vinavyoendelea nchini Sudan ni tokeo moja tu la kufuata mipango ya Marekani, mfadhili wa umbile la Kiyahudi na adui wa Uislamu na Waislamu.

Tatu: Khilafah, ambayo inawatia hofu Mayahudi, watawala wakoloni makafiri wa Magharibi, na vibaraka wao miongoni mwa watawala wa serikali ndogo zenye madhara katika ardhi za Waislamu-tunasema kwamba Khilafah hii inakuja bila shaka. Huu ni wakati wake, na hii ndio saa yake, kwa mapenzi na msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwa wakati huo, italipa kisasi kutoka kwa wale wote ambao wametenda jinai dhidi ya Ummah huu.

Kwa kumalizia, tunaiambia serikali inayotawala nchini Sudan na vyombo vyake vya usalama vilivyotekeleza kitendo hiki cha fedheha: waachilieni huru wabebaji ulinganizi wa haki mara moja. Mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu hatengenezi vitendo vya mafisadi. Msiwe chombo katika kuupiga vita Uislamu na wabebaji wa dawah yake, msije mkakutwa na udhalilifu duniani na adhabu kali kesho Akhera.

[الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجاً أُوْلَئِكَ فِي ضَلاَلٍ بَعِيدٍ]

Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali.” [Ibrahim:3].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu