Ijumaa, 16 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Kuinusuru Gaza “Palestina ilipotea baada ya Kuvunjwa Khilafah, na Kurudi kwake itaregea kama Khilafah kwa Njia ya Utume”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia iliandaa matembezi “Palestina ilipotea baada ya kuvunjwa Khilafah na kurudi kwake itaregea kama Khilafah kwa Njia ya Utume” baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu, ambapo watu wa Tunisia Al-Zaytouna waliyaitisha, wakiwasili katika Barabara ya Al-Thawra katikati ya umati mkubwa wa watu, ambapo mabango manne yaliinuliwa. Kichwa cha matembezi hayo kiliandikwa kwenye bango la kwanza, "Palestina ilipotea baada ya kuvunjwa Khilafah, na kwa kurudi kwake itarudi kama Khilafah kwa Njia ya Utume,” na la pili, “Anasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)... basi itakuwepo na Khilafah kwa Njia ya Utume.” Na la tatu liliandikwa, “Je, miaka 100 haitoshi kuvunjwa Khilafah na kupotea kwa Waislamu?” “Waislamu” na kwenye bango kuu la nne liliandikwa: “Palestina ilifunguliwa na Khalifa Umar na kuhamiwa na Khalifa Abdul Hamid, na jeshi la Khilafah Rashida kwa njia ya Utume litaikomboa, kwa hiyo kuweni miongoni mwa askari wake.”

Matembezi hayo yalijumuisha kauli mbiu zilizoimbwa na umati wa watu licha ya mvua kubwa kunyesha, kama vile: “Enyi watawala wa aibu, Gaza Inaungua.” “Songeni mbele, Songeni mbele kwa ajili ya Gaza hakuna kuisalimisha.” “Enyi ndugu zetu wa Jordan, Abdullah, ni mlinzi wa umbile la Kiyahudi. Enyi ndugu zetu wa Kinana, Al-Sisi ni nembo ya khiyana.”

Haya ni pamoja na kuyataka majeshi kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina). Matembezi hayo yalihitimishwa kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir ambapo aliwakumbusha watu juu ya ushindi wa Al-Omari na msimamo wa Sultan Abdul Hamid kuelekea Palestina.

Kwa kuendelea na matembezi haya ya kila wiki, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inataka kuinua kiwango cha ufahamu miongoni mwa watu wa Tunisia kuhusu kadhia ya Palestina na kuhusu suluhisho msingi la kadhia hii, na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu afungue njia kati yetu na watu wanyoofu miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi kwa ajili ya kusimamisha upya utawala wa Mwenyezi Mungu duniani.

Ijumaa, 20 Sha’aban 1445 H sawia na 01 Machi 2024 M

- Sehemu ya Amali ya Matembezi -

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu