Jumapili, 17 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Hizb ut Tahrir/ Uholanzi: Semina 

Serikali Zinahusika na Siasa za Kupinga Uislamu, Mashambulizi dhidi ya Quran

Hivi karibuni, mashambulizi dhidi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu yamefanywa upya katika nchi nyingi za Ulaya, ikiwemo Uswidi, ambapo mtu muovu mwenye chuki iliichoma moto nakala ya Qur'an Tukufu mbele ya ubalozi wa Uturuki jijini Stockholm, na kisha mtu mmoja mwanachama wa Harakati dhidi ya Kiislamu ya Pegida iliichana nakala ya Qur’an nchini Uholanzi, na kwa hivyo kwa sababu Qur'an Tukufu ni maneno ya Mwenyezi Mungu, Mtukufu, na ni sehemu muhimu ya imani yetu ya Kiislamu, na ni heshima ya kila Muislamu. Jumapili, 29/01/2023, wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Uholanzi walifanya semina yenye kichwa "Mojawapo ya matokeo ya siasa za chuki dhidi ya Uislamu:  mashambulizi dhidi ya Qur'an."

Ndugu Sharif alitoa hotuba ya kwanza ambapo alieleza jinsi Waislamu wanavyopaswa kuyaangalia matukio hayo mawili ya kuchoma moto Qur’an na kuzichana kurasa zake, yaliyotokea wiki iliyopita. Alieleza kuwa suala hilo si tukio la kibinafsi lililofanywa na mtu aliyepitiliza mipaka au mwenye chuki dhidi ya Uislamu pekee, bali ni suala la kisiasa linalofuatiliwa na nchi za Kikafiri za Magharibi.

Hotuba ya pili ilikuwa ya Ndugu Kamal Abu Zaid yenye kichwa, "Je, ni vipi kujibu vitendo hivyo?" Ndani yake aligusia umuhimu wa Qur'an kwa Waislamu na jinsi majibu yao yanavyoonyesha kwamba hakuna nafasi ya kukaa kimya wala kujadiliana kuhusu kutukana matukufu, na kwamba Waislamu wanapaswa kupaza sauti zao kwa kutangaza kupinga vitendo hivyo vya kuchukiza, vyenginevyo kitambulisho cha Kiislamu kitafifia kila sauti yao inapokuwa dhaifu na kufifia. Alimalizia kwa kusema kuwa, ukimya na mtazamo wa kupuuza vitendo hivyo ndivyo Wamagharibi makafiri wanavyotaka, ili matukufu ya Waislamu yapoteze umuhimu wake katika nyoyo zao, badali yake iwe ni utukuzaji usekula na vipimo vyake vilivyooza.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir/ Ulaya

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu