Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Kongamano la kila Mwaka la Khilafah: "Khilafah; Kadhia ya Umma na Wokovu wa Wanadamu"

Hizb ut Tahrir / Uholanzi yaandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah chini ya kichwa:

: "Khilafah; Kadhia ya Umma na Wokovu wa Wanadamu"

kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 103 H na 100 M

ya Kuvunjwa Dola ya Kiislamu (Khilafah).

Jumapili, 22 Shaaban 1445 H sawia na 03 Machi 2024 Miladia.

Mnamo tarehe 3 Machi 2024 M, miaka mia moja itakuwa imepita tangu kuangushwa kwa Dola ya Kiislamu kwa kuvunjwa Khilafah Uthmani.

Kwa muda wa miaka mia moja, Waislamu wamegawanyika katika vijidola dhaifu dhalili, baada ya karne nyingi kupita tangu wawe Umma moja katika dola moja, yenye kiongozi mmoja, Khalifa mmoja na jeshi moja.

Miaka mia hii imetuletea nini isipokuwa taabu, udhaifu, na vita, na yanayoendelea sasa huko Gaza ni ushahidi hai wa hilo, na wakati huo huo tunaona ubepari uliotawaliwa na Magharibi mkoloni ukiwapeleka wanadamu kwenye shimo. Uislamu ndio mfumo pekee wenye uwezo wa kuwatoa wanadamu katika giza la ubepari, na Umma wa Kiislamu ndilo pekee wenye uwezo wa kugeuza mizani hii. Hili ni jambo ambalo Waislamu hawana budi kulifanyia kila juhudi, na kwa mtazamo huu tunakualikeni ili mushiriki nasi katika Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa mwaka huu wa 2024 M jijini Amsterdam.

Kalima iliyorekodiwa ya Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ambayo iliwasilishwa wakati wa Kongamano la kila Mwaka la Mwaka 2024 nchini Uholanzi

Uholanzi: Mkutano wa Mwaka wa Khilafah 2024 CE "Khilafah, Suala la Ummah na Wokovu kwa Wanadamu"

Tunahitimisha kongamano la kila mwaka la Khilafah katika zama za miaka 100 M (103 H) za kumbukumbu ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu kwa kuondolewa Khilafah.

Hizb ut Tahrir/ Uholanzi ilifanya kongamano la kila mwaka mnamo siku ya Jumapili, 03 Machi 2024, jijini Amsterdam, lenye kichwa, "Khilafah, Kadhia ya Ummah na Wokovu kwa Wanadamu" Ukumbi wa mkutano ulijaa wageni wanaume kwa wanawake kutoka Uholanzi, Ubelgiji, Ufaransa, Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu (swt).

Kongamano hilo lilianza kwa usomaji wa Qur'an Tukufu.

Miongoni mwa wazungumzaji walikuwa: Mhandisi Salah Eddine Adada, Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, Haytham Seifoudin kutoka Ubelgiji, Dkt. Muhammad Malkawi, Ustadh Mazen Abdul Azim kutoka Canada na kuhitimishwa na Ustadh Okay Pala, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir/ Uholanzi. Wageni waliuliza swali kwa wazungumzaji.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ulaya

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Facebook: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Twitter: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Instagram: Hizb ut Tahrir / Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu