Jumamosi, 07 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Uingereza:

Kongamano “Jibuni Wito: Ikomboeni Palestina!”

Hizb ut Tahrir nchini Uingereza iliandaa kongamano kubwa kwa kichwa:

“Jibuni Wito: Ikomboeni Palestina!”

Iilihudhuriwa katikati mwa jiji la London na mamia ya wafuasi, waungaji mkono na Waislamu jumla ambao walihudhuria kutoka sehemu mbali mbali za Uingereza, ambapo kundi la wazungumzaji walitoa hotuba ambazo zililenga mambo yafuatayo:

1) Umbile la Kizayuni na natija yake ya unyakuzi wa ardhi, uhamishaji wa lazima na mauaji yanayoendelea si lolote ila ni upanuzi wa ukoloni wa Magharibi na msingi ulioboreshwa ili kulinda maslahi ya Magharibi Mashariki ya Kati.

2) Dola bandia za Waislamu leo na wale wanaozitawala na mipaka yao bandia ni urithi wa kikoloni ambao huenda kulingana na maslahi ya Magharibi na haziwezi kipeke yake kuinusuru Palestina licha ya kuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

3) Ndoto ya "suluhisho la dola mbili" ambalo Marekani inalinadi si chochote ila ni kwa ajili ya kutumikia maslahi yake katika eneo hilo na sio kwa ajili ya kupata usalama na haki katika eneo hilo. Hivyo matendo ya umbile baguzi la Kiyahudi na upanuzi wake kwa msaada wa Marekani ni ushahidi dhahiri wa hili. Na kamwe hakutakuwa na mfumo adilifu ambao Waislamu, Wakristo na Mayahudi wataishi ndani yake isipokuwa mfumo wa Khilafah, ambao umethibitisha hili katika historia yake ndefu, ambayo ilizidi karne kumi na tatu.

4) Tatizo la Palestina sio tatizo la kisiasa, bali ni wajib wa kiitikadi kwa Waislamu kupinga ukaliaji kimabavu na kuikomboa nchi hiyo, na ni juu ya majeshi ya Waislamu waamke kutoka usingizini mwao kuwatetea wanyonge na kupatikana uadilifu katika nchi za Waislamu.

5) Hakika subra ya Waislamu nchini Palestina katika matatizo yao hapana budi ushindi uwafikie, kwani hakika historia inatoa ushahidi juu ya Waislamu kupewa ushindi baada ya shida kupitia Aqida  thabiti na muongozo wa Kimungu. Na hakika sisi tuna yakini kwamba Palestina itakombolewa na itapata ushindi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

 Jumamosi, 10 Jumada Al-Akhir 1445 H sawia na 31 Disemba 2023 M

Kwa mengi zaidi Bonyeza Hapa

- Sehemu ya Hotuba zilizotolewa katika Kongamano -

Ujumbe kwenda kwa Waislamu wa Uingereza

Ujumbe kutoka kwa Mhandisi Salah Eddine Adada (Abu Muhammad)

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kuhusu Matendo yanayoweza kufanywa na Waislamu wa Uingereza ili Kusaidia katika Kuikomboa Palestina

Vipi Tutayahamasisha Majeshi?

Ndugu Saliqur Abu Issa anatoa hotuba nzito kuhusu vipi tunaweza kuyahamasisha majeshi ya Waislamu yenye utaalamu ili kuikomboa Gaza na Palestina yote inayokaliwa kimabavu.

Umbile la Kizayuni: Lengo la Kikoloni!

Ndugu Rupon Shaheed anaangazia juu ya umbile la Kiyahudi la Kizayuni – lengo la uvamizi wa kikoloni katika Mashariki ya Kati.

Kujibu Upendeleo wa Vyombo vya Habari na Propaganda za Kizayuni

Ndugu Abdulwahid azungumza na ndugu Shariff Abu Laith baada ya mkutano wake wa mwisho na Piers Morgan. Na wanajadili upendeleo wa vyombo vya habari na propaganda za Kizayuni zinazoendelea.

Musikate Tamaa na Azimio Lenu: Ushindi uko karibu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu

Ndugu Mazhar Khan anatoa hotuba ya dhati, yenye kusisitiza matumaini ya Ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt).

Matukio Maarufu na Mahojiano pamoja na Wazungumzaji wa Kongamano hilo

- Alama Ishara za Kongamano –

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#ArmiesToAqsa

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#AqsaCallsArmies

#HizbBritain

Kwa maelezo zaidi, tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut Tahrir / Uingereza:

Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir/ Uingereza
Twitter: Hizb ut Tahrir/ Uingereza
YouTube: Hizb ut Tahrir/ Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu