- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Kongamano Kubwa la Gaza!
Hizb ut Tahrir/Wilayat Uturuki inaandaa kongamano la halaiki lenye kichwa “Kongamano Kubwa la Gaza” jijini Ankara, ambapo suluhisho la kweli na la kudumu la kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) litajadiliwa.
Huku umbile halifu la Kiyahudi likiendelea na uvamizi na mauaji ya halaiki mjini Gaza kwa zaidi ya siku 563, viongozi wa nchi za Kiislamu wanatoa jumbe za kulaani lakini hawachukui hatua madhubuti. Hivyo, umbile la Kiyahudi linalokalia kimabavu linakuwa na ujasiri zaidi na kuharakisha kasi ya mauaji yake. Wakati viongozi wa nchi za Kiislamu wakikiri kushindwa kwa diplomasia, wanasema hawawezi kuchukua hatua kwa pamoja, kulaumiana, kukusanyika na kueneza ujumbe wa kulaani. Wanaelekeza Palestina na Gaza kwa jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.
Ingawa hakuna suluhisho lililotolewa kwa takriban mwaka mmoja na nusu mjini Gaza na miaka 76 katika ardhi zote za Palestina ili kukomesha mauaji haya na uvamizi unaowatesa wanadamu, Hizb ut Tahrir/Wilayah Uturuki inaandaa kongamano kubwa kwa ushiriki mpana kujadili suluhisho la kweli na la kudumu la kadhia ya ardhi iliyobarikiwa (Palestina).
Wazungumzaji na taarifa za programu hiyo, ambayo ilitangazwa kwa umma chini ya kichwa “Tumeishiwa maneno! Diplomasia imefeli! Kwa ajili ya suluhisho la kweli na la kudumu ... Kongamano Kubwa la Gaza,” ambalo kila mtu ambaye moyo wake unapiga kwa ajili ya Gaza anaalikwa, kama ifuatavyo.
Wazungumzaji:
Abdullah Imamoglu
Abdul Razzaq Atish
Dkt. Ali Muhiuddin Karadgi (Rais wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu)
Mahmoud Kar (Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki)
Mehmet Goktas
Muhammad Amin Yildirim
Mohammed Mishnish (Rais wa Jumuiya ya Mshikamano wa Palestina)
Mustafa Ozcan Gunesdogdu
Necmettin Irmak (Jukwaa la Mshikamano wa Kiislamu)
Dkt. Nawaf Al-Takkouri (Rais wa Umoja wa Wanazuoni wa Kipalestina)
Tayeb Elji (Rais wa Wakfu wa Wasomi wa Vyuo)
Sheikh Youssef Makharza (mwanachuoni kutoka Palestina)
Basi kuweni pamoja nasi … na mushiriki ujira na thawabu…
Jumamosi, 05 Dhu al-Qi’dah 1446 H sawia na 03 Mei 2025 M
- Wakati na Mahali -
Siku na Tarehe:
Jumamosi, 03 Mei 2025 M
Wakati:
20:30 (Kwa saa za Ankara na Madina Al-Munawwara)
Mahali:
Ankara North Social Complex, Takva Congress Center
Kuzey Ankara Külliyesi / Takva Kongre Merkezi
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Facebook: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Mtandao wa X: Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Chaneli ya Daily Motion ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki