Jumanne, 08 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uzbekistan: Baada ya Miaka Ishirini Ndugu Ghazif Abdul Hamid Aachiliwa Huru kutoka Magereza ya Madhalimu!

Kutoka kwa Saad bin Abi Waqas (ra) amesema: "Nilisema, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni watu gani walio na balaa zaidi?" Akasema: "Manabii, na wema kisha mfano wao kwa mfano wao. (Maana ni kwamba) mtu atapewa mtihani kwa mujibu wa kiwango cha dini yake. Ikiwa katika dini yake yuko imara, ataongezewa balaa zake, na ikiwa katika dini yake ni hafifu, atahafifishiwa balaa, na balaa hazitaacha kuwepo kwa muumini mpaka atatembea juu ya ardhi ilhali hana makosa juu yake."

Miongoni mwa wanaume hawa ambao wamethibitisha dini yao ya Uislamu ni ndugu yetu, Abdulmajid Gaziev, mnamo mwaka wa 1999 alikuwa mwanachama wa Hizb ut-Tahrir, na akaanza kulingania Uislamu na kutafuta kusimamisha dola ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alituahidi ndani ya Qur'an Tukufu na akaitolea bishara njema Mtume wake (saw) katika Hadithi Sahih.

Lakini hamu yake ya kukutana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Pepo haikumkinaisha tu kulingania Uislamu katika nchi yake pekee, kwa hivyo alisafiri kwenda Uzbekistan. Huko alilingania haki kwa nguvu sana mpaka huduma za usalama za Uzbek zikamkasirikia. Na katika mwaka huo, walimtuhumu kwa makosa ya jinai na wakamhukumu kifungo cha miaka ishirini gerezani, kulingana na Kifungu cha 159 na mfano wake. Ndugu yetu alifungwa katika Gereza la Chirchiq, Gereza la Zangi Ota, Gereza la Koson Soy, Gereza la Andijan, miongoni mwa mengine. Akaahidiwa kwamba angeachiliwa huru iwapo angewaomba msamaha, lakini alithibiti katika haki na kuwapa mgongo.

Baada ya kumalizika muda wa kifungo chake, alihamishwa kwenda nchini mwake, Kyrgyzstan, na watu wa "Qarasu" walimkaribisha mkaribisho wa mashujaa kama anavyostahili, kwani yeye alifungwa kwa dhulma sio kwa sababu ya watoto wake au mali yake, bali kwa sababu ya dini lake; Kwa sababu alisema kuwa mbingu na ardhi ni za Mwenyezi Mungu (swt), kwa hivyo hapana budi tuhukumu kwa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), yaani kwa sheria za Uislamu …

Mtu mmoja miongoni mwa wale waliomtembelea alimuuliza, "Je! Huhuzuniki kwa umri wako uliokaa gerezani?" Akasema: "Ikiwa nitaambiwa je, ungeridhia miaka mia mbili ya umri  badala ya miaka ishirini na ukawa hukufungwa? Nikasema: Hapana, kwa sababu miaka hii itakuwa ni kivuli kwangu katika kivuli cha kiti cha enzi siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli chake, Mwenyezi Mungu akipenda, na natumai Mwenyezi Mungu ataniokoa kwayo kama ujira kutoka kwake na ataniingiza Peponi kwa rehema zake.

Maadamu kunapatikana wanaume kama hawa miongoni mwetu, maadui hawataweza kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa vinywa vyao wala kwa nguvu zao ... na dua yetu ya mwisho ni Ewe Mwenyezi Mungu, tunakuomba utukirimu kwa dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo kwayo Uislamu na watu wake watapata izza na kwayo  ukafiri na watu wake watadhalilika na utujaalie miongoni mwa wale wanaofanya kazi katika utiifu wako na walinganizi wa njia yako na waenezaji wa dawah yako na wenye kunusuru dini yako, na Rehema na Amani ya Mwenyezi Mungu zimshukie bwana wetu Muhammad na jamaa zake.

Jumatatu, 15 Rabi' ul-Akhir 1442 H sawia na 30 Novemba 2020 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 01 Disemba 2020 16:25

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu