Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mbinu ya Amerika na Kupunguza Kisiasa Wanajeshi ndani ya Afghanistan

Na: Saifullah Mustanir*

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amesema katika jukwaa la kiulimwengu la kiuchumi lililofanyoka Davos, kwamba serikali ya Afghan haitapata matatizo baada ya vikosi vya kigeni kujiondoa kutoka nchini humo; hata hivyo, kama mazungumzo yataendelea na Taliban badala ya serikali yake, vita vitachukua awamu nyingine.

Tukifuatilia kwa karibu mchakato wa mazungumzo ya amani ya Amerika na Taliban, serikali ya Rais Ghani imejipata mbele ya milango iliyofungwa pekee na hana njia yoyote ya kufikia hata habari ndogo ya kuaminika kuhusiana na meza ya mazungumzo, hali ilikuwa ya majonzi kabla kufutiliwa mbali kwa msururu wa mazungumzo ya amani hapo awali, kiasi kwamba Zalmai Khalilzad, mjumbe maalumu wa Amerika katika mazungumzo ya amani, alimkubalia Rais Ghani kusoma kutoka kwa nakala ya chapa kielelezo cha mpango wa amani aliyoombewa  kwa dakika chache. Hii ni kwa hakika kwamba Amerika inaimani chache sana kwa vibaraka wake walioko Kabul na serikali ya Afghanistan haijatambua asili ya ukoloni, ambao vibaraka hawaruhusiwi kuwa na usemi juu ya masuala makuu.

Katika mpango uliopendekezwa na Donald Trump, idadi ya majeshi ya Amerika itaondoka kutoka Afghanistan mpaka uchaguzi wa Amerika wa 2020; 4000 watatolewa katika awamu ya kwanza. Hii ni kwa sababu vita vya Afghanistan vimebadilika kuwa kidonda cha kuvuja damu na vita virefu zaidi katika historia ya Marekani. Chuki ndani na nje ya Amerika zinazidi dhidi ya vita vya Afghanistan na raia wa Amerika wanavichukulia vita hivi vimefeli. Hivyo basi, Amerika inalenga kupunguza vikosi vyake ndani ya Afghanistan ili kuficha kushindwa kwao kwa upande mmoja na kufanikisha ushindi wa Rais Trump katika uchaguzi ujao kwa upande mwingine.

Mpango wa Amerika wa kupunguza vikosi ndani ya Afghanistan in ujanja wa kisiasa, hivyo kutokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mazungumzo ya amani yanayo endelea, vinginevyo, hilo litachukuliwa kama kushindwa kwa Amerika ndani ya Afghanistan. Hivyo, mara kwa mara tunasikia wanasiasa wa Amerika wanakataa kuwa na uhusiano baina ya kuondolewa kwa vikosi na mazungumzo ya amani. Hii ndio sababu Mark Espier, Katibu wa Ulinzi wa Amerika, ametangaza kwamba kuondolewa kwa vikosi kutoka Afghanistan si kwa sababu ya mazungumzo, kama au la mazungumzo yanaendelea.

Hivyo basi, hakuna sintofahamu kati ya taarifa ya Rais Ghani juu ya kuondolewa kwa vikosi vya Amerika na taarifa ya bwana wake. Yeye ni mdogo kuweza kuamua au kutoa maoni juu ya asili ya kujitoa kwa vikosi. Rais Ghani na timu yake hakika wanahofu juu ya kuondolewa kwa vikosi na maisha yao ndani ya Afghanistan baada ya kuondoka kwao, kwa sababu vikosi vya Afghanistan haviwezi kufanya uvamizi wa kijeshi wowote iwapo msaada wa kifedha na wakijeshi utakosekana.

Hata hivyo, Ashraf Ghani upande mmoja anajaribu kupigia debe kuondoka kwa vikosi vya Amerika ili awe na uhusiano wa karibu na Donald Trump -  kwa kupata msaada – lakini kwa upande mwingine, anataka mchakato wa kuondoa vikosi upangiliwe na serikali yake, kuhakikisha kudhibiti uongozi wake ndani ya Afghanistan baada ya Amerika kutoka katika uvamizi, wakati kihakika kitendo chake cha kwanza kama rais kilikua ni kutia saini kwa makubaliano ya kiusalama ndani ya saa 24 katika afisi ya urais ili kujihakikishia uongozi, na sasa anadai hatakumbwa na shida yoyote baada ya kuondoka kwa vikosi?

Ni ukweli usio na shaka kwamba Waislamu walio Afghanistan wanahasira na uwepo wa vikosi vya Amerika humo na wanajaribu kila iwezekanavyo kuwatoa nje na kumaliza huu uvamizi. Kikundi pekee, chenye hasira kwa kuondoka kwa vikosi vya Amerika, kimeundwa na wale ambao wamepata uongozi wa serikali kwa sababu ya uvamizi. Hawa ni warasilimali ambao wameregea kutoka nchi za Kimagharibi, na kupora rasilimali za watu. Hawakujipatia heshima kwa watu na hawana uungwaji mkono kisiasa na wala msaada wa umma nchini.

Matokeo yake tunaweza kubashiri kujitoa kwa kisiasa na kimbinu kwa vikosi vya kigeni ndani ya Afghanistan. Hili hata hivyo, halimaanisha kujitoa kabisa kutoka Afghanistan, bila kujali mchakato utapewa jina gani. Hii ni kwa hakika kwani Amerika haitabadilisha mikakati ya Afghan kimaeneo kwa chochote kile. Njia pekee ya kulazimisha kuondoka kwa vikosi vya Amerika na kumaliza uhalifu dhidi ya binadamu ni maandamano ya majeshi ya Waislamu chini ya Khilafah.

*Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Afghanistan

*Imeandikwa kwa ajili ya Gazeti la Ar-Rayah - Toleo 272

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 28 Machi 2020 08:36

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu