- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Makala Mbalimbali kutoka Gazeti la Ar-Rayah Toleo la 601
Vichwa vya Habari
(Imetafsiriwa)
Yaliyo Juu ya Ukurasa wa Mbele
Hakika, sisi katika familia ya Gazeti la Ar-Rayah tunatoa pongezi zetu za dhati kwa Ummah wetu wa Kiislamu kwa mnasaba wa Idd al-Adha iliyobarikiwa. Tunamwomba ﷻ aifanye Idd hii kuwa mwanzo wa kheri na baraka kwetu, ili Idd ijayo ije huku tukiishi chini ya heshima, ushindi, na tamkini, tukiwa tumehifadhiwa chini ya bendera ya Khilafah Rashida bendera ya (لا إله إلا الله محمد رسول الله) “La ilaha illa Allah, Muhammadur Rasul Allah” “Hakuna mungu wa haki ila Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu ﷻ. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) amesema, «... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ» “…Kisha kutakuwa na utawala wa dhulma, na utabakia kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwe kisha atauondoa anapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.”
===
Ukurasa wa Mbele
Ni Lini Majeshi Yetu Yatasonga Kuwanusuru Wanawake Wenye Heshima wa Palestina?!
Klabu ya Wafungwa wa Palestina ilisema kwamba mamlaka za uvamizi zimeongeza uhalifu wao dhidi ya wafungwa wanawake katika Gereza la Damon katika maeneo yanayokaliwa kimabavu, hasa katika kasi ya ukandamizaji wa kiserikali. Katika taarifa moja, Klabu hiyo ilielezea kwamba Gereza la Damon ni miongoni mwa magereza maarufu zaidi ambayo yameshuhudia kuongezeka kwa shughuli hizi, kwani linawashikilia wafungwa wengi wa kike 88, pamoja na idadi kadhaa mengine katika vituo vya mahojiano na uzuizi.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa vitengo vya ukandamizaji vya idara ya magereza ya uvamizi vilifanya angalau operesheni kumi za ukandamizaji katika kipindi cha Machi na Aprili 2026, zikiambatana na vipigo vikali, vikiwalazimisha wafungwa wa kike kulala chini huku mikono yao ikiwa imefungwa nyuma ya migongo yao, na kuwashambulia kimakusudi katika mkao huu, na kusababisha majeraha kwa idadi kadhaa yao.
Kuhusu hali hizi mbaya zinazowakabili wanawake waheshimiwa wa Palestina iliyobarikiwa na jinai zinazofanywa na Mayahudi dhidi yao, taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir ilisema, “Mandhari inayoogofya na isiyodirikika: vipi kundi la wanawake huru wa Kiislamu wanaweza kukamatwa, kudhalilishwa, na kuteswa, huku Ummah wa Kiislamu na majeshi yake wakijua, lakini damu yao haichemki kwa uharaka wa kuja kuwasaidia na kuwalipizia kisasi?!"
Taarifa hiyo ilisisitiza kwamba kile wanawake wa Palestina wanachoteseka katika magereza ya umbile la Kiyahudi ni doa la aibu kwa majeshi ya Ummah wa Kiislamu ambayo yameshindwa kuwanusuru. Ilisema, "Kile ambacho dada zetu wanavumilia katika magereza ya uvamizi ni fedheha kwa Ummah wa Kiislamu na doa la aibu kwenye paji la uso la majeshi yote ya Waislamu ambayo yanabaki bila kuchukua hatua kuwahami."
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari pia ilithibitisha kwamba yote haya yanatokana na kukosekana kwa dola ya Khilafah, ngao ya kinga na ngome iliyoimarishwa kwao na kwa Waislamu wote. Ikasema, “Wanawake hawa huru wa Kiislamu wasingelipatwa na yale waliyoyastahimili lau Waislamu wangekuwa na dola na kiongozi (Imam) Mtume Muhammad (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujilinda kwaye” Kiongozi wa Waislamu ni ngao ya watoto wa kiume na wa kike wa Ummah.”
Ama kuhusu sababu ya ujasiri wa Mayahudi waliosifiwa kama viumbe waoga zaidi dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa, kupitia mauaji na kujeruhi, kukamata na kutesa, kufunga na kunyanyasa, kuhamisha na kulazimisha kuhama, taarifa hiyo ilisema, "Lakini baada ya Mayahudi kuona jinsi watawala wa Waislamu walivyowafunga Ummah na majeshi yake, wakiwazuia kuinusuru Palestina na watu wake hata katika nyakati za giza na mbaya zaidi, wakawa na uhakika kwamba bila kujali wangefanya nini, kulikuwa na walinzi wa mipaka yao na umbile lao ambao wangehakikisha kwamba Ummah na majeshi yake yangezuiliwa (kuwashambulia). Kwa hivyo, hawakujali tena kuhusu mwitikio wa Ummah au majeshi yake, mradi tu waliona kwamba viti vya enzi vya watawala vilibaki imara na imara mahali pake."
Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kilihitimisha taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa kuregelea njia ambayo suluhisho liko la kuwanusuru wafungwa wa kiume na wa kike wa Palestina, kuisafisha Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na Mayahudi, kukomboa ardhi zote za Waislamu zinazokaliwa kimabavu, na kuwanusuru Waislamu wanaokandamizwa kila mahali. Ilisema, "Mwanzo na njia ya mabadiliko huanza kwa kuwaondoa watawala wa Waislamu, ambao wanawakandamiza Waislamu, na kisha kutoa kiapo cha utiifu kwa khalifa mmoja, muongofu kwa Ummah kuuongoza na majeshi yake ili kusimamisha Dini, kuwanusuru wanaokandamizwa, na kuikomboa Palestina na ardhi zengine za Waislamu zinazokaliwa kimabavu. Kwa hili tunakulinganieni, Enyi Waislamu! Hivyo, fanyeni haraka...haraka!"
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum 4–5].
===
Juu ya Kichwa Kikuu
Salamu za Idd al-Adha 1447 H
الله أكبر الله أكبر الله أكبر لا إله إلا الله... الله أكبر الله أكبر ولله الحمد
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd
Mtume (saw) amesema: «إِنَّ أَعْظَمَ الْأَيَّامِ عِنْدَ اللَّهِ يَوْمُ النَّحْرِ» “Siku tukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni siku ya kuchinja.” Kwa mnasaba huu uliobarikiwa, na katika kuadhimisha ibada za Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[ذَلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ]
“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” [Al-Hajj:32].
Licha ya majanga ambayo Ummah wa Kiislamu unapitia chini ya watawala ambao wameufelisha na kuukabidhi kwa adui yake, wakijaza nyoyo zetu maumivu na huzuni, bado tunapaswa kutoa pongezi na baraka zetu za dhati kwa Ummah wetu mpendwa wa Kiislamu, wenye subira na wanaotafuta thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwenye Idd al-Adha iliyobarikiwa, tukimwomba Mwenyezi Mungu azifanye siku hizi za Idd kuwa za baraka, ushindi, na heshima.
Pia tunafurahi kutoa pongezi zetu, pamoja na zile za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi. Tukimuomba Mola wetu Mtukufu kwamba Ummah karibuni umpe Bay’ah ya Khilafah Rashida ambayo itahitimisha zama za udhalilifu ambao Ummah unaishi ndani yake, na kuanzisha zama za ushindi, ukombozi, na tamkini, katika kutimiza kauli Yake Mtukufu:
[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Nur: 55].
Mwaka huu, Idd al-Adha inakuja huku Ummah wa Kiislamu bado ukiugua chini ya mzigo wa ukoloni, ambao unauletea mateso makali, bila kuuachia furaha ya Idd wala furaha katika riziki - nchini Palestina, Lebanon, Sudan, Iran, Yemen, Ash-Sham, na kwengineko - ukiunyima furaha ya Idd na furaha ya siku zenye baraka: [وَلَيَالٍ عَشْر] “Na kwa masiku kumi.” [Al-Fajr: 2].
Donald Trump huyo mwenye kiburi anakasirika na kutishia, akiwapiga mabomu Waislamu na ardhi zao na kuwatishia kuzimu isipokuwa wajisalimishe kwake. Na mshirika wake wa karibu na mwenzake Benjamin Netanyahu ananguruma na kudhulumu katika nchi za Waislamu, akitishia kuiunda upya Mashariki ya Kati kulingana na ruwaza na ndoto zake.
Ama kuhusu dola zilizobaki za kikoloni, ima zinaunga mkono pande hizi mbili - zikiwaunga mkono na kuimarisha azma yao - mradi tu tubaki kuwa wahanga, na gharama inalipwa na sisi, si wao; kama vile Uingereza, Ufaransa, Australia, Ujerumani na nyenginezo — au wanaweza kuona hili tu na wasifanye chochote kuwasaidia waliokandamizwa au kuwasaidia walio na shida. Ama kuhusu watawala wa Waislamu, wao hata ndio wabaya zaidi wanapopanga njama dhidi yetu badala ya kusimama nasi; wanalisha kiburi cha Amerika, na kusaidia uhalifu wa Mayahudi. Bora zaidi kati yao ni yule anayetazama kutoka mbali na kuwahesabu waathiriwa, au kutoa lawama za kimaneno na shutma kutokana na unafiki mtupu.
Haya ni baadhi ya mambo yanayotia giza maisha yetu na kuvuruga furaha yetu. Hata hivyo, bishara njema bado zinaonekana kuhusu afueni ya karibu na mwamko ambao utapindua meza ya ukoloni na kuunda upya mandhari ya kisiasa kwa njia ambayo itawafurahisha waumini. Umma wa Kiislamu unaongezeka katika azma siku baada ya siku na unaonyesha uthabiti ambao Magharibi haikutarajia. Umewakataa watawala wake wahalifu na sasa kwa kuwa nyuso zao za halisi zimefichuliwa — na uchi wao wa maadili na usaliti kuwekwa wazi — baada ya kuutelekeza katika saa zake za giza na chini ya dhurufu ngumu zaidi, imani hii pekee inatosha kuleta mchakato wa mabadiliko yanayotarajiwa.
[إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra‘d:11]. Tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba siku hiyo iwe karibu.
Mtume (saw) amesema: «مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهِنَّ أَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ. فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ ﷺ: وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ، إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ» “Hakuna siku ambazo amali njema ndani yake inapendwa zaidi na Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi kumi.” Wakauliza: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema: “Hata Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu akitoka kwa nafsi yake na mali yake, kisha kusirudi nafsi wala mali.”
Hii, basi, ni fursa kwa kila mja mcha Mungu kuzishika siku hizi zenye baraka—wakiunganisha mikono na juhudi zao kwa zile za wabebaji Dawah—kujitahidi kufikia utekelezaji wa faradhi kubwa zaidi ya zama zetu: kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ili, tuweze tena kuwa "Umma bora zaidi kuwahi kutolewa kwa ajili ya wanadamu," na kupata heshima kupitia Uislamu.
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah...
Allahu Akbar, Allahu Akbar, wa lillahi Alhamd
===
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Ulikutana na Amiri wa Makabila ya Hausa mjini Port Sudan
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alhamisi, 21/5/2026, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Sudan, ukiongozwa na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, Ustadh Nasser Ridha, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mratibu wa Kamati ya Mawasiliano, walikutana na Amiri wa makabila ya Hausa katika Wilayah ya Port Sudan, Ustadh Salih Abdul Rahman, nyumbani kwake. Watu wafuatao pia walikuwepo katika mkutano huo:
1- Nour El-Din Mohammed, Mkuu wa Makabila ya Hausa katika Wilayah ya Bahari Nyekundu.
2- Hassan Osman Youssef, mzee wa kabila.
3- Dkt. Abdullah Hassan Abdullah, mzee wa kabila na profesa wa chuo kikuu.
4- Dkt. Amir Ahmad Osman, Katibu Mkuu wa kabila hilo.
Baada ya utambulisho, Ustadh Nasser Ridha alielezea kwamba lengo la Hizb ut Tahrir ni kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kudhihirisha Dini, akisisitiza ufaradhi wa kufikia hili na kuwanusuru wale wanaofanya kazi kuelekea hilo.
Pia alisisitiza uhusiano wa udugu wa Kiislamu na umoja wa Ummah na dola mbele ya mradi wa kikoloni wa kikafiri unaotaka kuuchana Ummah kupitia umwagaji damu na ukabila.
Kila mtu alithibitisha na kusifu pendekezo hilo, akikubali kwamba watu wa Hausa wana mila ya Kiislamu ya muda mrefu na wanawakilisha ardhi yenye rutuba kwa mradi wa Kiislamu, na pia kuwa ulinzi muhimu kwa umoja wa nchi na muundo wa kijamii.
Walikaribisha mkutano huo, wakisisitiza thamani yake na umuhimu wa ushirikiano endelevu katika mradi huu kwa manufaa ya nchi na watu wake.
===
Je, Haujakuja Wakati kwa Ummah wa Kiislamu Kuwaondoa Watawala Wake Wasaliti Walioketi Kifuani Mwake?!
Watawala wa Waislamu ni wale walioiwezesha Amerika kuvamia ardhi zetu na kuziingia. Wao ndio waliozifungua ili kuhifadhi kambi za kijeshi ambazo sasa zinafikia makumi. Wao ndio waliofanya amani na umbile la Kiyahudi, wakahalalisha uhusiano nalo, na kuanzisha miradi nao, wakiruhusu kuingia katika ardhi za Waislamu. Hivyo, baada ya haya yote, imekuwa kawaida kwamba ardhi zetu zigeuke kuwa kawanda na uwanja wa michezo kwa wahalifu hawa, ambapo wanatekeleza mipango na miradi yoyote wanayotaka kuimarisha udhibiti wao.
Watawala wa Waislamu walishirikiana na Amerika katika uvamizi wake wa Iraq na Afghanistan, na katika kutekeleza miradi yake huko al-Sham na Yemen, wakiiwezesha huko. Wanaendelea kuipatia na umbile la Kiyahudi usaidizi wote wa kifedha, vifaa, kijeshi, na kisiasa unaohitajika ili kufikia malengo yao ya kikoloni. Katika haya yote, waathiriwa ni Waislamu, ardhi zao, na rasilimali zao.
Kwa hivyo, Ummah utakaa kimya hadi lini chini ya uongozi wa wasaliti hawa? Je, haujawadia wakati wa kuwaondoa juu yake na kumteua Khalifa mmoja atakayeunganisha safu zake, kuziunganisha, na kukata mkono wa ukoloni kutoka katika ardhi zetu, ili uwe tena Umma wenye heshima unaojenga izza, sio Umma dhaifu na jukwaa la matukio?
Ndiyo, Wallahi, wakati umefika.
===
Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu! Je, Nyinyi Sio Ngome Isiyoweza Kupenyeka ya Nchi Zenu?
Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu: Mtakaa kimya kwa muda gani juu ya matendo ya Ruwaybidha (wasio na maana) wafisadi? Je, nyinyi si ngome isiyoweza kupenyeka ya nchi zenu? Je, wajibu wenu sio kulinda Ummah na watu? Au je, Aqida yenu imebadilika kwa kisingizio cha kuwatii watawala, huku mkijua kwamba hakuna utiifu kwa kiumbe chochote katika kumuasi Muumba? Na kwamba wale mnaowatii leo watawakana Siku ya Kiyama, na hamtaweza kuwakana katika kisimamo hicho muhimu mbele ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mtukufu? Jueni kwamba mnawajibika kwa makosa ya watawala katika nchi zenu, na kwamba mna uwezo wa kuyabadilisha. Kwa hivyo, chukueni hatua kabla hamjajuta, wakati majuto hayatakuwa na faida!
Enyi Waislamu: Wakati umefika wa kujikukuta vumbi la udhalilifu kutoka kwenu ule udhalilifu uliosababishwa na watawala wenu Ruwaybidha katika utiifu wao kwa mabwana zao kutoka kwa dola kafiri za kikoloni. Wakati umefika wa nyinyi kubadilisha maovu yao. Kwani mbali na maovu ya wazi na ukafiri unaolindwa na katiba zao zilizotungwa na wanadamu, wamegeuza ardhi kuwa jukwaa kwa majeshi ya dola kafiri za kikoloni zile zisizokutakia mema, zinazopora utajiri wenu na mali za umma, na zinazowazuia kujitahidi kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutabikisha sheria Yake na kupeleka ujumbe Wake kwa watu, kama vile Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Maswahaba zake (ra), na Makhalifa baada yake walivyofanya.
Enyi Waislamu: Siku na matukio katika miaka ya hivi karibuni yamekuthibitishieni kwamba mna uwezo wa kukabiliana na maadui zenu, na kwamba adui yenu bila khiyana na njama za watawala wenu dhidi yenu hawezi kufanya chochote katika nchi zenu. Kumbukeni kwamba nyinyi ndio Umma bora zaidi kuwahi kutolewa kwa ajili ya wanadamu, kwa Iman yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt), kuamrisha mema na kukataza maovu. Kwa hivyo, fanyeni haraka kwenye mabadiliko halisi ambayo kiongozi mkuu, Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, inakuiteni. Jitahidini nayo kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume, ili majeshi ya makafiri yafukuzwe kutoka katika ardhi zenu, au ili mzifanye makaburi yao.
===
Njia za Maji katika Ardhi za Waislamu ni Utajiri wa Kimkakati
Hali ya Trump haiko tu katika maumbile ya maadui zake, bali katika maumbile ya eneo lenyewe. Mlango-Bahari wa Hormuz si njia ya maji tu; ni sehemu ya shinikizo la kimataifa inayoweza kugeuza mzozo wowote mdogo kuwa mgogoro wa kimataifa.
Kwa hivyo, Amerika inajikuta imenaswa kati ya machaguo mawili magumu: kupanda kwa uchumi, ambako kunaweza kuwasha eneo lote, au kupungua kwa uchumi, ambako kunaweza kutafsiriwa kama kurudi nyuma kutoka kwa semi zake za kuwa na nguvu. Mwishowe, mgogoro wa Hormuz unafichua ukweli thabiti katika siasa za kimataifa: nguvu za kijeshi, bila kujali ni kubwa kiasi gani, hazitoshi kila wakati kutatua migogoro hasa wakati jiografia inapoingiliana na uchumi na hesabu za kikanda na kimataifa zinazidi kuwa ngumu.
Katikati ya mabadiliko haya, ukweli usiopingika unaibuka: njia za maji zilizo katikati ya ulimwengu wa Kiislamu si mipaka ya kijiografia au njia za meli tu, bali ni utajiri mkubwa wa kimkakati uliotolewa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa Ummah huu. Kuanzia Mlango-Bahari wa Hormuz hadi Bab al-Mandab, kutoka Mkondo wa Suez hadi Mlango-Bahari wa Malacca na njia zengine muhimu, Waislamu wamekuwa wakishikilia funguo za biashara na mtiririko wa nishati duniani kwa muda mrefu. Hata hivyo hawajafanikiwa hadi leo katika kubadilisha baraka hii kuwa nguvu ya kiuchumi na kisiasa inayowahudumia watu wao na kuhifadhi uhuru wao.
Mifumo hii ya maji si mzigo wa kisiasa kama wengine wanavyoielezea. Badala yake, ni fursa ya kihistoria ya kujenga nguvu ya kiuchumi duniani ikiwa Waislamu wataweza kuiwekeza ipasavyo ili kuregesha hadhi na heshima yao iliyopotea.
===
Mataifa Hayainuki Kwa Kutochukua Hatua kwa Uzembe, Wala Hali Yao Haibadiliki Kwa Kutoa Nyudhuru
Kupuuza wajibu wa Sharia wa kunusuru Uislamu hakukufungika na kuachana na mapigano au misimamo muhimu. Inaweza kuanza na mambo ambayo watu huyaona kuwa madogo: kukaa kimya kuhusu munkar (uovu) kwa kuogopa ukosoaji wa watu, kupuuza kuwalingania wengine kwenye ma’ruf (wema) kutokana na uzembe au shughuli za kidunia, au kujiwekea mipaka kwa Swala na matendo machache ya ibada huku wakipuuza wasiwasi na mambo ya Waislamu. Inaweza pia kuonekana kama kuacha kujitahidi kwa ajili ya Dini kwa kisingizio cha kuwa na shughuli nyingi na kazi na maisha ya kila siku. Baada ya muda, ukwepaji unakuwa ndio tabia, na moyo huzoea kuhalalisha uzembe hadi unapopoteza hisia yake ya upungufu.
Maswahaba (ra) wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), walipokosa fursa ya mema, wangehisi huzuni na majuto, kwa sababu walijua kwamba maisha ni mafupi na kwamba mtu atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuulizwa kuhusu Dini yake, wajibu wake wa Shariah kwake, na kile alichokiwasilisha kwa ajili yake. Hata hivyo, leo, watu wengi wanaposhindwa hutafuta mtu atakayehalalisha uzembe wao, badala ya mtu anayewakumbusha Mwenyezi Mungu (swt).
Hakika, Ummah hauinuki kupitia uzembe, wala hali zake hazibadiliki kupitia kutoa nyudhuru. Huinuka kupitia wanaume na wanawake wenye ikhlasi wanaochukua jukumu, wanaopambana dhidi yao wenyewe, na wanaojitahidi kwa ajili ya Dini yao hata kama ni kwa njia ndogo tu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ]
“Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, ataviona vitendo vyenu.”” [Surah At-Tawbah 105]
Hebu kila mara tujiulize: tumewasilisha nini kwa ajili ya Uislamu? Na je, sisi ni miongoni mwa wenye ikhlasi wanaojitahidi, au ni miongoni mwa wanaotoa nyudhuru?



