Jumatano, 28 Shawwal 1447 | 2026/04/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Kilio cha Haraka cha Msaada, Enyi Ummah wa Kiislamu!

Wanawake na watoto wa Gaza wanalilia msaada... wanawake na watoto wa Sudan wanalalamika... wanawake na watoto wa Uyghur huko Turkestan Mashariki wanateseka na kupiga kelele... Wanawake wa Kiislamu na watoto wao kila mahali wanapaza kilio baada ya kilio, wakiita: Je, kuna mtu yeyote wa kusaidia? Je, kuna mtu yeyote wa kuitikia wito? Je, kuna mtu yeyote wa kujibu?!

Wakati Dola ya Kibaniani Inapozivua Niqab Kwenye Nyuso za Mabinti wa Kiislamu, Warithi wa Muhammad Bin Qasim Wako Wapi Ndani ya Jeshi la Pakistan?

Mnamo Jumatatu, 15 Disemba 2025, katika sherehe moja, Waziri Mkuu wa jimbo la India la Bihar, Nitish Kumar, aliichana niqab kutoka kwa daktari mmoja Muislamu, Nusrat Parveen. Baada ya kufanya hivyo, alicheka kana kwamba kuichana niqab hiyo kutoka kwa uso wa mwanamke wa Kiislamu ilikuwa ni mzaha. Ilhali, Mayahudi walipomfunua mwanamke mmoja wa Kiislamu na kumdhihaki hali yake, Swahaba aliyekuwepo alimuua Myahudi huyo; na Mayahudi walipomuua shahidi Swahaba huyo baadaye, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alizingira kabila lote, akawakamata na kuwafunga wote, na alikuwa akitoa hukumu juu yao, lakini hatimaye, baada ya maombezi, adhabu ndogo ilitolewa: kabila lote lilifukuzwa Madina. Lakini leo hakuna dola ya kulinda heshima ya Dkt. Nusrat Parveen na kumpa Baniani huyu muovu, Nitish Kumar, funzo.

Tafsiri Al-Baqarah [Muhkam na Mutashabiha]

Jambo muhimu katika sayansi ya Quran linalohusiana na tafsiri ya aya za Mwenyezi Mungu, mbali na maana halisi na ya kimajazi, ni kuwepo kwa yaliyo wazi na yaliyo na utata katika Kitabu. Mwenyezi Mungu (saw) amesema, “Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.” 

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu