Jumatano, 28 Shawwal 1447 | 2026/04/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Mwangwi wa Himaya: Uharamia wa Marekani Pwani ya Venezuela

Mnamo tarehe 10 Disemba 2025, Marekani ilimkamata nahodha wa meli ya mafuta kutoka pwani ya Venezuela, ikipanda meli hiyo na kuelekeza shehena yake ya takriban mapipa milioni 1.8 ya mafuta ghafi ya Venezuela hadi Marekani chini ya kibali cha vikwazo vya Marekani ambacho kilikuwa kinakaribia kuisha. Maafisa wa Marekani walidai hatua hii ya utekelezaji ililenga kuadhibu ukiukaji wa vikwazo vya muda mrefu vinavyohusiana na madai ya usafirishaji haramu wa mafuta. Serikali za Venezuela na Cuba zililaani hatua hiyo kama “wizi wa waziwazi” na “uharamia,” huku Cuba ikiuita “ugaidi wa baharini” ikiathiri mahitaji yake ya nishati. Usumbufu huo umeacha zaidi ya mapipa milioni 11 ya mafuta ya Venezuela yamekwama baharini, huku meli za mafuta na wafanyibiashara wakitathmini upya hatari za kubeba mafuta ghafi ya Venezuela, na kulazimisha punguzo kubwa na mazungumzo ya mikataba na wanunuzi muhimu kama vile China.

Yaonekana Mazuri, lakini Ndani Hamna Kitu!

Rais Erdoğan, katika hotuba yake baada ya mkutano wa baraza la mawaziri, pia aligusia mwelekeo wa Uturuki wa sera ya kigeni, akisema: “Uturuki imeipa dunia funzo katika haki za binadamu kupitia juhudi zake zinazolenga amani na haki katika maeneo yaliyolowa damu na machozi—Gaza, Syria, Somalia, na Libya.” Alisisitiza kwamba taifa hilo limeunganishwa kwa fungamano lisilotikisika, pasi na tofauti kati ya Mturuki, Mkurdi, Muarabu, Alevi, au  Caucassian. (Mashirika, 15.12.2025)

Ubepari kama Chanzo Kikuu cha Maafa ya Mafuriko huko Sumatra

Kimbunga Senyar kilikuwa kichocheo tu; kiwango cha uharibifu nchini Indonesia kinaonyesha miongo kadhaa ya usimamizi mbaya wa ikolojia. Sumatra imepoteza mamilioni ya hekta za misitu, ikidhoofisha maeneo ya maji huko Aceh, Sumatra Kaskazini, na Sumatra Magharibi. Maeneo ya tambarare yalikaushwa maji kwa ajili ya mashamba makubwa, na kusababisha kupungua kwa ardhi na kugeuza vizuizi vya maji asilia kuwa mabonde ya mafuriko. Makaazi ya haraka katika maeneo tambarare ya mafuriko, pamoja na usimamizi dhaifu wa matumizi ya ardhi, yaliongeza athari. Mvua kali ilipofika, mandhari haikuwa na uwezo uliobaki wa kuhimili. Maafa yanaonyesha kwamba muundo wa maendeleo wa Indonesia—unaoendeshwa na uchimbaji na usimamizi duni wa mazingira—umefanya hali mbaya ya hewa kuwa hatari zaidi kuliko inavyopaswa kuwa. (news.mongabay)

Enyi Waislamu: Kufunga Vyumba vya Ibada ni Shambulizi kwa Uislamu na Lazima Kukabiliwe kwa Upinzani Mkali, wa Pamoja wa Kisiasa

Baada ya mwelekeo hasi wa kisiasa kwenye vyumba vya ibada, idara ya Chuo Kikuu cha Copenhagen iliamua mwishoni mwa Novemba kufunga kile kinachoitwa “vyumba vya utulivu,” ambavyo Waislamu walikuwa wakivitumia kwa zaidi ya miaka ishirini, bila matatizo yoyote, na wanafunzi na wafanyikazi kuswali swala za kila siku. Uamuzi huu kwa mara nyingine tena umezua mjadala kuhusu vyumba hivi na kuhusu kama kunapaswa kuwepo na nafasi kwa Waislamu kutekeleza swala zao katika taasisi za elimu.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu