Alhamisi, 29 Shawwal 1447 | 2026/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Unyanyasaji wa Kimpangilio wa Kijinsia Dhidi ya Wanawake wa Sudan Hautoi Jibu lolote kwa Kukosekana kwa Dola Inayojali Heshima ya Mwanamke Mwislamu

Mnamo Alhamisi tarehe 11 Disemba, shirika, ‘The Strategic Initiative for Women in the Horn of  Africa’, liliripoti kuwa limerekodi karibu matukio 1300 ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake katika majimbo 14 nchini Sudan tangu vita vianze nchini humo mnamo Aprili 2023, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikilaumiwa kwa 87% ya visa hivi. Lilielezea unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ukitumika kama silaha ya kimfumo katika mzozo huo, likisema “umeenea, unarudiwa rudiwa, unakusudiwa na mara nyingi unalenga”. Ubakaji ulichangia robo tatu ya matukio yaliyorekodiwa, huku visa 225 vikihusisha watoto, baadhi wakiwa na umri wa miaka 4. Matukio yalitokea majumbani, maeneo ya umma na pia yalijumuisha kizuizini cha muda mrefu cha wanawake ambao waliteswa, kubakwa na genge na ndoa za kulazimishwa. Mnamo Jumapili tarehe 7 Disemba, vikundi vya matibabu vya Sudan viliripoti kwamba watoto na wanawake kadhaa walinyanyaswa kingono na kubakwa walipokuwa wakikimbia kukamatwa kwa El Fasher huko Darfur na RSF Oktoba hii.

Je, Vikosi vya Kiislamu vya Jeshi la Pakistan Sasa, Chini ya Uongozi wa Jenerali wa Marekani, Vitawalinda Mayahudi na Kuupokonya Silaha Upinzani wa Palestina?

Gazeti la Dawn liliripoti kwenye tovuti yake mnamo tarehe 13 Disemba, 2025 kwamba majeshi ya Waislamu huenda yakatumwa kuanzia mwezi ujao kwa ajili ya “Kikosi cha Kimataifa cha kuleta Utulivu” mjini Gaza. Hapo awali, mtawala kibaraka wa Marekani Shehbaz Sharif alikuwa tayari ametoa idhini “ya kikanuni” kwa kutumwa kwa vikosi vya Pakistan huko Gaza. Hata hivyo, wakiogopa upinzani mkali wa umma, watawala wa Waislamu mmoja baada ya mwengine wamekuwa wakionyesha kutokuwa na msaada kwao mbele ya Amerika. Hivyo sasa shetani Trump na wafuasi wake, watawala wa Waislamu, wanaunda njama mpya za kutumia vikosi vyetu vya Waislamu vya mujahid kuwalinda Mayahudi na kuwanyang'anya silaha Hamas na vikosi vyengine vya upinzani vya Palestina.

Hukumu ya Kifo kwa Hasina: Udhalimu wa Kisekula Uliomuunda Hasina Ungalipo

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa hukumu ya kifo ya kihistoria dhidi ya mtawala wa Bangladesh aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina. Kwa watu waliokandamizwa wa Bangladesh, uamuzi huu unatoa uthibitisho wa kiishara uliochelewa kwa muda mrefu na unasimama kama shtaka lenye nguvu kwa utawala uliokanyaga ubinadamu wa kimsingi. Lakini uamuzi huu unahitaji tafakari ya kina, sio sherehe tu. Haki ya kweli inahitaji mabadiliko ya kimfumo, sio adhabu ya mtawala dhalimu tu. Chanzo kikuu ni mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, ambao unahubiri demokrasia huku ukitekeleza ‘mantiki ya siasa za kijiografia’.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu