Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 482
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 482
Vichwa Vikuu vya Toleo 482
Katika mwezi wa Rajab Tukufu mwaka huu, 1445 H - 2024 M, inarudi kwetu kumbukumbu ya uchungu ya miaka 103 H na 100 M ya kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu na wahalifu wa Kiarabu na Kituruki, ambayo iliasisiwa na Bwana wa Mitume Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu (ra), na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H, sawia na 03/03/1924 M, na ardhi iliyobarikiwa (Palestina) ilipotea kwa kupotea Imam ambaye ni ngao, Khalifa wa Waislamu ambaye kwaye wanapigana nyuma yake na kujihami..
Hizb ut Tahrir/Amerika inaandaa Kongamano la kila mwaka la Khilafah kwa mwaka huu wa 2024 chini ya kichwa:
“Gaza: Migogoro na Suluhisho - Dori ya Waislamu wa Amerika”
Katika matangazo ya moja kwa moja kwenye Chaneli ya Al Jazeera mnamo Jumatatu asubuhi, Februari 12, 2024, msemaji wa Wizara ya Afya, Ashraf al-Qudra, alizungumza na Al Jazeera akielezea uharibifu uliotokea huko Rafah na nyumba zilizolipuliwa, ambazo zilikuwa zinakaliwa na wakaazi na watu waliohamishwa makao yao.