Ijumaa, 30 Shawwal 1447 | 2026/04/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Mauaji na Njaa ya Watoto wa Gaza Havitakwisha Kupitia Mipango ya Wale Waliohusika na Mauaji ya Halaiki Bali Kupitia Uhamasishaji wa Majeshi ya Waislamu Pekee

Katika kipindi cha miaka 2 iliyopita, watu wa Gaza wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya mabomu, mzingiro wa kikatili na jinai za kutisha zaidi za umbile la mauaji la Kiyahudi, ambapo wanawake na watoto wamekuwa wahanga wakuu. 65,000 wameuwawa, wakiwemo zaidi ya watoto 20,000 – sawa na watoto 30 wanaouawa kila siku. Watoto wamepigwa risasi kimakusudi na wavamizi wa Kiyahudi au mashambulizi ya droni barabarani, au hata wanapotafuta chakula kwenye vituo vya misaada ambavyo vimekuwa ‘mitego ya kifo’ kwa wanaokabiliwa na njaa. Kulingana na ‘Save the Children’, watoto waliuawa au kujeruhiwa katika zaidi ya nusu ya mashambulizi mabaya katika maeneo ya usambazaji wa chakula mjini Gaza ndani ya wiki nne baada ya Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza kuanza shughuli zake.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Wito wa Haraka kwa Maafisa na Wanajeshi: Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Mnamo Ijumaa, 10 Oktoba 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia kuinusuru Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka ambapo ulinganizi ulielekezwa kwa watu wa Tunisia watoe wito wa haraka kwa maafisa na wanajeshi chini ya kichwa, “Nyinyi ndio wenye Uwezo zaidi wa Kulitokomeza Umbile la Kiyahudi!”

Ni Dhambi Kubwa kwamba Gaza Haikukombolewa Au Umbile la Kiyahudi Halikutokomezwa kwa Juhudi za Wanajeshi wa Waislamu, Bali Iliangamizwa Kabisa na Kukombolewa Kidogo kwa Mpango Wa Trump na Usaliti wa Watawala wa Waislamu!!

Serikali ya Misri ilitangaza kusherehekea utekelezwaji wa mpango wa Trump mjini Gaza. Sisi alimwalika Rais wa Marekani kusherehekea kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa mpango wa Gaza: [Rais Trump wa Marekani alisema mnamo Alhamisi kwamba mateka waliosalia wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza wataachiliwa huru mnamo Jumatatu au Jumanne ya wiki ijayo, na kwamba bado analenga kuzuru eneo hilo kusherehekea hafla hii... “Ni muhimu kutaja kuwa Rais Sisi wa Misri alikuwa amemwalika Trump kushiriki katika sherehe ambazo zitafanywa nchini Misri ili kuadhimisha kutiwa saini kwa makubaliano, akiyachukulia kuwa makubaliano ya kihistoria ambayo yanazifisha taji juhudi za Misri, Marekani, na wapatanishi katika kipindi cha hivi karibuni.” (CNN Arabic, 9/10/2025)]

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu