Utumiaji kama Silaha wa “Chuki dhidi ya Mayahudi” kunyamazisha Nusra ya Ukombozi wa Palestina
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na mijadala mingi nchini Uingereza ikiashiria kuwepo mafungano kati ya maandamano ya Palestina na kuongezeka kwa chuki dhidi ya Mayahudi na mashambulizi dhidi ya Mayahudi nchini humo. Kabla ya kumbukumbu ya mwaka wa 2 wa shambulizi la Octoba 7 la Hamas dhidi ya umbile la Kizayuni, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, aliwataka wanafunzi wasijiunge na maandamano yanayoiunga mkono Palestina siku hiyo, akionya juu ya “kuongezeka chuki dhidi ya Mayahudi katika barabara zetu”, na kwamba “sio tamaduni ya Uingereza kuwa na heshima ndogo kwa wengine” kwa kufanya maandamano juu ya kumbukumbu hiyo, na kuongeza kuwa maandamano yametumiwa na baadhi kama “udhuru wa kuchukiza kuwashambulia Mayahudi wa Kiingereza”.



