Alhamisi, 29 Shawwal 1447 | 2026/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Baada ya Mashambulizi ya Umbile la Kiyahudi kwa Sumud Flotilla Wito wa Dharura kwa Maafisa na Askari katika Majeshi ya Waislamu Jeshi Husagwa sagwa na Jeshi Pekee

Enyi Wanajeshi: Mumeshuhudia shambulizi la umbile la Kiyahudi dhidi ya Sumud Flotilla iliyosafiri bahari ili kuvunja kuzingirwa kwa kaka na dada zenu mjini Gaza, na mkasikia vilio vyao vya kuomba msaada, na mkaona kwa macho yenu uovu wa watawala, ufisadi wao, ukosefu wao wa hisia, na kufeli kwao kuinusuru Gaza na wanaharakati wa flotilla. Imekudhihirikieni pia kwamba watawala hao walimfanyia khiyana Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwaangusha Waumini walipoangusha hadharani kile walichokiita “chaguo la vita” kwa kunyenyekea matamanio ya viongozi wa ukafiri.

Rais wa Lebanon Atoa Wito wa Kuidhinishwa Haraka kwa Mpango wa Trump wa Gaza!

Enyi Watu wa Lebanon, Enyi Watu wa Palestina, Enyi Umma wa Uislamu: Rais wa Lebanon alitoa wito wa kuidhinishwa haraka kwa mpango wa Trump wa kusimamisha vita mjini Gaza, akijua kwamba ni mpango wa kufikia maslahi ya umbile la Kiyahudi, ambalo limeshindwa kulazimisha kupitia nguvu ya silaha, kama vile kujisalimisha kwa mujahidina, kuachiliwa huru kwa wafungwa wa Kiyahudi na malengo mengine. Ili kufikia malengo haya kwa umbile halifu kupitia ujanja wa Trump.

Simama pamoja na Watu Wasioteteleka wa Gaza, Sio na Trump Mwenye Kiburi!

Miaka miwili imepita tangu mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Gaza, ambalo liliyafanya ili kuficha kushindwa kukubwa lilikokupata mnamo Oktoba 7, 2023. Miaka miwili ambayo kila siku ilishuhudia mauaji mapya na ukatili usioelezeka, na dunia nzima imeshuhudia ukatili wa Mayahudi wanyakuzi ambao unakinzana na akili. Watoto, watoto wachanga, nyumba, shule, misikiti na hospitali zililengwa. Watawala wa nchi za Kiislamu walikutana mara kwa mara, wakazungumza, wakalaani, na kisha kutawanyika. Kila shutma iliwashajiisha Mayahudi kufanya uvamizi na mauaji makubwa zaidi. Umbile la Kiyahudi lilifikia hatua ya kuzuia kuingia kwa kipande cha mkate au tama la maji ndani ya Gaza kwa miezi mingi mirefu.

Katika Ziara ya Amerika: Yote yako Pamoja – Kufedheheshwa, Kusihi, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!

Ziara ya Rais Erdoğan wa Uturuki nchini Marekani kushiriki katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa mandhari ya kufedhehesha, sio kwake tu bali kwa viongozi wote wa dola pia. Rais mwenye kiburi wa Marekani Donald Trump alitoa hotuba mbele ya Baraza Kuu ambapo alitangaza kwamba “Marekani imebarikiwa kuwa na uchumi imara zaidi, mipaka yenye nguvu zaidi, jeshi lenye nguvu zaidi...” na kwamba ndani ya miezi minane ya utawala wake aliitoza dunia kodi ya ziada ya kiasi cha dolari trilioni 17, na kwamba Marekani iko katika nafasi nzuri huku nchi zengine “zinaenda kuzimu.” Alisema kuwa maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayana maana, na kudai kwamba alimaliza vita saba ndani ya miezi saba. Aliitaja tarehe saba ya Oktoba 2023 kama “unyama wa magaidi wa Hamas,” akizingatia kuwa suluhisho liko katika kuachiliwa huru mara moja kwa wafungwa, na kuongeza kuwa dini inayonyanyaswa zaidi duniani ni Ukristo.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu