Onyo la Tom Barrack kwa Lebanon Dhidi ya “kuregea Bilad Al-Sham”! Kukiri kwa Siri kwa Marekani kwamba Mradi wa Kuunganisha Ummah Kupitia Usimamishaji wa Khilafah ndio Hasimu Pekee wa Kweli wa Mradi wa Marekani katika Kanda hii
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Mnamo 12 Julai 2025, katika mahojiano na Arab News, Mjumbe Maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Tom Barrack, alizindua mfululizo mpya wa taarifa zinazofichua mradi wa Marekani katika eneo hili na kuthibitisha kina cha mgogoro ambao utawala wa Marekani unakabiliana nao katika kutekeleza mradi wake wa “Mashariki ya Kati Mpya”.



