Kutambuliwa kwa Dola ya Palestina Kutambuliwa kwa Mayahudi Kunyakua 78% ya Palestina!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Uingereza, Canada, Australia na Ureno zililitambua ile inayoitwa “Dola ya Palestina,” na kufuatiwa na nchi kadhaa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika kuanzia Septemba 22-30, 2025, na ulioongozwa na Ufaransa na Saudi Arabia. Utambuzi huu ulikaribishwa na watawala Ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wa Waislamu, pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Waarabu. Jambo la kushangaza ni kwamba, ilikaribishwa pia na mashirika ya Kipalestina, ambayo yanaona kuwa ni matunda ya uthabiti wao, kana kwamba Palestina imekombolewa na na umbile la Kiyahudi kung'olewa!



