Jumapili, 25 Shawwal 1447 | 2026/04/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Marekani Yaendesha Uharibifu... Na Watawala ni Watiifu kwa Miradi Yake ya Kikoloni!

Mamlaka zilizofuatana juu ya nchi yetu hazikujiepusha na kutii mashinikizo ya Marekani, kwa kukubali kushiriki katika kuimarisha mkakati wake wa kikoloni katika kuitawala dunia nzima, ikiwemo kanda yetu ya Waarabu na eneo letu la Afrika. Hii ni kama vile kusainiwa na utawala wa Sebsi juu ya uamuzi wa Barack Obama wa kuipa Tunisia hadhi ya Mshirika Mkuu Asiyekuwa mwanachama wa NATO, au kufungua nchi yetu kwa mpango wake barani Afrika kwa kuandaa, kwa mwaka wa nane mfululizo, mazoezi ya kijeshi ya African Lion 2025, ambapo Jenerali Dagvin Anderson, kamanda wa Kamandi ya Marekani ya Umoja wa Mataifa Afrika (AFRICOM) alisema mbele ya Kamati ya Huduma za Silaha katika Bunge la Congress la Marekani kwamba Morocco na Tunisia ni miongoni mwa washirika wenye uwezo mkubwa wa kusafirisha usalama barani humo.

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari yenye kichwa: “Taarifa ya Quad na Ubwana Uliopotea”

Wanaofuatilia suala la Sudan na mapambano makali ya kimataifa juu ya ardhi yake wanajua vyema kwamba vita hivi vinaendeshwa na Marekani ili kung'oa ushawishi wa Kiingereza na kuichana Sudan kwa kutenganisha Darfur, na kwamba hatua zote za kisiasa zinazofanywa na Amerika au vyombo vyake nchini Sudan zinalenga kuondoa juhudi zozote ambazo zingewarudisha watu wa Uingereza kwenye mandhari.

Al-Waqiyah TV: Khilafah Pekee Ndio Itakayoiletea Sudan Izza!

Sudan kwa sasa iko katikati ya vita vya kipumbavu ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia na kuzua mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na kuhama makaazi. Wananchi wa Sudan wamekumbwa na mizozo mbalimbali pamoja na umaskini mkubwa, udikteta, migawanyiko ya kikabila na kitabaka na matatizo mengine mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miongo kadhaa chini ya uongozi, tawala na mifumo mtawalia.

Ummah Unahitaji Khilafah Kulinda Matukufu Yake Sio Mikataba ya Ulinzi ya Kuwalinda Watawala Vibaraka

Pakistan na Saudi Arabia zimeingia katika makubaliano ya kihistoria ya ulinzi wa pande zote, ambapo uvamizi wowote dhidi ya dola moja utachukuliwa kuwa shambulizi kwa pande zote mbili. ‘Mkataba wa Kimkakati wa Ulinzi wa Pamoja’ ulitiwa saini na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif na Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammad Bin Salman katika Kasri la Al-Yamamah jijini Riyadh mnamo Jumatano, 17 Septemba 2025.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu