Ijumaa, 30 Shawwal 1447 | 2026/04/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Jinsi Viongozi wa Waislamu Wanavyoitelekeza Gaza kwa ajili ya Diplomasia na Miamala

Rais wa Indonesia Prabowo Subianto alihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja kati ya 'Israel' na Hamas, na akatoa wito wa kusitishwa kwa mzozo wa 'Israel' na Iran. Akizungumza nchini Singapore na Waziri Mkuu Lawrence Wong, Prabowo alisisitiza haja ya azimio la amani kupitia diplomasia. Alionyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya vifo vya raia huko Gaza na kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati. Zaidi ya hayo, alizungumzia mzozo wa Myanmar, akisisitiza kujitolea kwa ASEAN kwa Makubaliano ya Mambo Tano ya kukomesha vurugu na kukuza mazungumzo jumuishi. Indonesia na Singapore zilikubali kuendelea kuunga mkono ushirikiano wa amani nchini Myanmar na kuzingatia kanuni za ASEAN za uthabiti wa kikanda na juhudi za kibinadamu.

Kuharibu Masoko kama vile Soko la Dokhinat ni Vita dhidi ya Watu katika Riziki zao na ni Matokeo ya Kukosekana kwa Dola ya Kiislamu ya Khalifah

Katika kitendo cha kikatili na vurugu, mamlaka za eneo la Jabal Awlia, Jimbo la Khartoum, kwa kutumia askari waliokuwa na silaha nyingi, walibomoa Soko la Tumbaku lililoko kwenye Barabara ya Jabal Awlia kwa tingatinga mnamo siku ya Alhamisi asubuhi, 12 Juni 2025, na kuvunja meza za maonyesho. Hata wale waliotoroka soko hilo na bidhaa zao hawakusazwa!

Kati ya Usaliti wa Palestina na Kashmir na Utumwa kwa Amerika Asim Munir Anafanya Nini Mbele ya Firauni Wa Zama Zetu, Trump?

Katika wakati ambapo Amerika inapigana vita dhidi ya jirani Muislamu, Iran, kwa kutumia mkono wake mchafu katika eneo hilo, umbile la Kiyahudi, Rais wa Marekani, Donald Trump, alimkaribisha Mkuu wa Majeshi wa Pakistan mnamo Jumatano, 18 Juni 2025, kwa chakula cha mchana katika mkutano ambao haujawahi kushuhudiwa katika Ikulu ya White House. Kinachotia shaka kuhusu mkutano huu, na muda wake, ni kwamba ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kumkaribisha mkuu wa jeshi la Pakistan katika Ikulu ya White House, bila ya kuwepo kwa afisa yeyote mkuu wa kiraia wa Pakistan, kuashiria umuhimu wa mkutano huo, na unyeti wa mada yake.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu