Ijumaa, 30 Shawwal 1447 | 2026/04/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Vyombo vya Usalama katika Mji wa Al-Qadarif Vyawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir vikiliunga mkono umbile la Kiyahudi!

Katika hotuba ya hadhara iliyotolewa na Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Qadarif, kwenye soko la Al-Qadarif karibu na hospitali ya meno, mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 23 Dhul-Hijjah 1446 H, inayolingana na 19/6/2025 M, Ustadh Awad Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza kuhusu uhalisia wa vita na umbile la Kiyahudi, furaha ya Waislamu kwa mashambulizi dhidi ya umbile hili, na kiu ya watu ya ushindi dhidi ya mkaaji huyu wa kimabavu wa ardhi tukufu—Masrah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alithibitisha faradhi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaikomboa Palestina na ardhi nyenginezo za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Hadhira iliitikia vyema hotuba hiyo, na kulikuwa na michangio tofauti tofauti kutoka kwa waliohudhuria.

Mkataba wa Yunus-Tarique wa London ni Jaribio la Kudumisha Utawala wa Marekani na Mfumo wao Kandamizi wa Kisekula wa Kibepari

Mnmo tarehe 13 Juni 2025, mkuu wa serikali ya mpito Dkt. Yunus, akiwa amkeketi jijini London, amewakatisha tamaa wananchi kwa kufanya maridhiano ya kisiasa na Tarique Rahman, kaimu mwenyekiti wa BNP (Bangladesh Nationalist Party) kwa sababu watu wa nchi hii hawajasahau historia ya utawala mbaya na ufisadi wa matabaka tawala ya BNP. Kwa hakika, maridhiano haya ya kisiasa ya Yunus-Tarique na kugawanya madaraka ni sehemu ya mpango wa Marekani, ambao kupitia kwao wataweza kutekeleza miradi ya kikoloni. Mumeshuhudia kwamba waliokuwa mabalozi wa Marekani Dan Mozena, Bernicat na Peter Hass, wote wamekaribisha maridhiano haya na kuonesha kuridhika, na kwa mujibu wa taarifa za habari, BNP pia imependekeza kumfanya Dkt. Yunus kuwa rais. Kupitia kuanguka kwa dhalimu Hasina, watu wa nchi hii walionyesha nia yao ya kutaka kuwa huru kutokana na mfumo dhalimu wa kibepari na kutawaliwa na Wakoloni makafiri wa Magharibi. Aina hii ya maridhiano si lolote bali ni usaliti kwa watu wa nchi hii.

Na Mwenyezi Mungu si mwenye Kughafilika na Wanayoyafanya Madhalimu

Tunaona kwamba vyombo vya usalama vya dola nchini Kyrgyzstan vinawakamata wahalifu ambao wamefanya uhalifu mbalimbali, na baadhi yao walishtakiwa kuwa katika genge la wahalifu, huku wengine wakishtakiwa kwa hongo, mauaji, na mashtaka mfano wa hayo. Ikiwa kweli wanahusika katika uhalifu huo, basi wanachukuliwa pia kuwa wahalifu kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu. Lakini wakati huo huo, tunashuhudia kwamba kuna wafungwa ambao hawakufanya kitendo chochote cha jinai, bali walikamatwa kwa sababu tu ya kulingania dini ya Mwenyezi Mungu na kwa kusema: “Mola wetu ni Mwenyezi Mungu”! Na pia wanakamatwa kikatili mithili ya wahalifu wa kweli na kutupwa magerezani ambako hupigwa sana na mbinu nyingine za "kisasa" za mateso. Hawa ni wanachama wa Hizb ut Tahrir, na madhalimu ni maafisa wa serikali na vyombo vyao vya usalama.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu