Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 535
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 535
Vichwa Vikuu vya Toleo 535
Mnamo Jumanne 4 Februari 2025, akiwa ameketi ubavuni mwa muuaji wa Gaza, Benjamin Netanyahu, Rais Trump wa Marekani alitangaza, "Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya kazi nayo pia." Tamko la kiburi la Trump kuhusu Gaza ni kofi kwenye uso wa watawala wa Waislamu, ambao wametekeleza kwa utiifu amri ya Marekani, na kuzuia vikosi vya majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, na hivyo kuruhusu mauaji ya Waislamu nchini Palestina. Watawala wa sasa wa Waislamu, kama wale waliotangulia, wanajifunza kwamba Marekani haiwajali wao, au viti vyao vya khiyana. Marekani itaendelea kuwadhalilisha na kuwashusha hadhi mbele ya dunia na watu wao wenyewe. Kwa hakika, kushiriki katika mfumo wa dunia unaoongozwa na Marekani, na kushikamana na sheria za kimataifa na taasisi za kimataifa, si chochote ila unyenyekevu na utiifu kwa Marekani na rais wake. Hata hivyo watawala hawa hawajali. Hata hivi sasa wanakimbilia kumfurahisha na kumtuliza bwana wao, Amerika, wakijaribu kuwasilisha kwake "mpango wa amani wa Waarabu" wao wenyewe.
Mnamo Februari 6, 2023, matetemeko makubwa mawili ya ardhi yenye kipimo cha 7.8 na 7.5, yaliyopiga kusini na katikati mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria, yaliathiri mikoa 11 na kusababisha uharibifu mkubwa na kupoteza maisha. Takriban watu 54,000 nchini Uturuki na 8,500 nchini Syria walipoteza maisha katika matetemeko haya ya ardhi huku kitovu cha matetemeko hayo kikiwa Kahramanmaraş. Jumla ya waliopoteza maisha ilizidi 62,000, na mamilioni ya watu wakabaki bila makao. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wa huru na rasilimali za ndani zinaonyesha kuwa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.
Katika kampeni yake inayoendelea dhidi ya Hizb ut Tahrir, Shirika la Kitaifa la Upelelezi la India lilimkamata Bava Bahrudeenand Kabeer Ahmed Aliyar mnamo 3 Februari 2025, baada ya miezi kadhaa ya unyanyasaji. Vyombo vya habari vya India viliripoti kwamba "walikula njama na wengine kueneza fikra ya Hizb ut Tahrir huko Tamil Nadu, ambalo ni shirika lililopigwa marufuku." Kisha mamlaka zikanasibisha kesi yao na kesi inayoendelea ya Dkt. Hameed Hussain chini ya Sheria ya (Kuzuia) Shughuli Zisizo Halali (UAPA) ya 1967!